GSM yatangaza kujiondoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara

GSM yatangaza kujiondoa kwenye udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Afisa Biashara Mkuu wa GSM, Alan Chonjo amezungumza kwa niaba ya uongozi wa GSM na kusema kuwa wamejiondoa katika nafasi ya udhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ameeleza kuwa sababu kubwa ya kujiondoa ni kutokana na yaliyotokea baina ya TFF na Bodi ya Ligi, ikumbukwe kuwa lengo lilikuwa ni kukuza tasnia ya michezo, na GSM ilifanya hivyo kama mdau kukuza tasnia ya mpira wa miguu.

“Maamuzi ya kujitoa hayakuwa maamuzi mepesi kwetu, lakini tumeamua kuchukua maamuzi magumu. Tunawatakia kila la kheri na tutaendelea kuacha milango wazi kwa ajili ya kukuza mchezo wa soka Tanzania,” amesema.

Yalitokea kitu gani mbona hawajafafanua?
 
haha sawa ....wenzetu wasenegali wapo siku ya mapumziko kuwapokea mabingwa wao wa afcon.
 
kuna athari yoyote katika maamuzi haya katika soka? au wameona kwao mambo hayataenda kama walivyopanga?
 
Hahaha angalau timu ziliweza toa ushindani kwa timu kubwa, yanaenda kujirudia ya timu A kukodiwa fuso na timu B alafu wanaipiga 8 bongo ngumu mno
Kwa hizo milioni 3.5 kwa mwezi? Wacha uzwazwa
 
Kwaiyo wewe mbulula unafikiri nani anaumia? Gsm hana cha kupoteza ela yake ataielekeza kwingine, tff,bodi ya ligi na vilabu vingine ambavyo avikuwa na uwezo kujiendesha ndo wahanga wakubwa wa hili jambo, unapokenua kwamba mmeshinda ni ujinga wa kiwango cha lami
Unauhakika GSM alizitoa hizo pesa.
 
Kupitia mkutano na wanahabari uliofanyika jioni ya leo, kampuni ya GSM imetangaza kujitoa katika udhamini wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
IMG_3633.jpg
 
Mwamedi ana roho mbaya Sana imejaa uhindi mwingi sana.

Huu udhamini anadhani anaikomoa yanga kumbe anazikomoa team ndogo zinajiendesha zenyewe tu,

Hata alikiba na kile kinywaji alichokuwa partner mudi alienda kuharibu na kumchomea utambi..

Soka la bongo ni kichefuchefu sana
 
k
Kwaiyo wewe mbulula unafikiri nani anaumia? Gsm hana cha kupoteza ela yake ataielekeza kwingine, tff,bodi ya ligi na vilabu vingine ambavyo avikuwa na uwezo kujiendesha ndo wahanga wakubwa wa hili jambo, unapokenua kwamba mmeshinda ni ujinga wa kiwango cha lami
kushney babu jiiiii 😹😹😹😹

63D3FFF8-CC74-44CE-A8E5-AD973EA6D79C.jpeg
 
Back
Top Bottom