Kwa wanaofuatilia habari mbali mbali nadhani mmeona skendo hiyo ikitikisa bara letu la giza.
Pamoja na jambo hilo kuonekana la kushtusha,ila watu wa jinsi hiyo wapo wengi na hata hapa kwetu Tanzania wapo.
Wasichana na wanawake hawaoni tabu kutembea na mtu maarufu na wengine ili mradi walipwe pesa tu.
Kuna maafisa wanaoishi kwa utaratibu huo na wana wanawake idadi ya kutosha kwa vile wanaweza kuwahudumia.
Kuna kundi kubwa na wasichana wamehamia Dodoma kutega wakiamini huenda wakapendwa na maafisa hao wasijue kwamba watu kama hao ni watu hatari kutokana na kutoridhika kirahisi hata wanawake wakiwa 400.
Tabia hii ni hatari na ili angalau ipungue kwenye hizi ofisi za umma,viongozi wa juu wakemee vikali na kuchukua hatua kali zikiwemo za kuwafukuza kazi maafisa hao.
Hata hivyo nakiri kuwa hii ni ngumu sana kwa kuwa wanaotarajiwa kupeleka miswada ya sheria huenda ni wanaume hawa hawa tunaowaona ni hatari.
Wanawake acheni tamaa mbaya mnajidhalilisha sana. Ombeni Mungu awape roho ya utoshelevu
Sent from my Infinix X626 using
JamiiForums mobile app