Kisa cha kigogo wa serikali ya Guinea ya Ikweta, Baltasar kuhusishwa na matukio ya kufanya ngono na zaidi ya wanawake 400 huku wengi wakiwa ni wake za wakuu wa utawala katika nchi hiyo na kisha kujirekodi video kimeistua dunia na habari zake kusambaa hapa Tanzania. Mbali na kuanikwa vibaya pia mamlaka za nchi yake zimeahidi kumfukuza kazi yeye na wote waliohusika.
Kiujumla ni kisa cha ajabu, kusikitisha, kuchefua na kuhuzunisha. Lakini kwa upande wa pili ni kisa kilichojaa uonevu mkubwa dhidi ya mhusika mkuu (Baltasar) na wahusika waliotendewa (wanawake).
Kosa la Baltasar ni lipi hasa?
Kosa ni kutembea na wake za watu au wake za watu kutembea na huyo jamaa? (Kidini na kimaadili sio sawa), je kisheria ni kosa?
Kosa ni kujirekodi akifanya ngono? Kimaadili sio sawa, je kisheria ni kosa?
Uhuru wa faragha wa wahusika umelindwaje? Nani mwenye mamlaka ya kuingilia uhuru wa faragha wa mtu mwingine?
Starehe na uhuni wao wa sirini unatuhusu nini sisi?
Kwanini video na picha za matukio ya wahusika zisambazwe mitandaoni mara baada ya mhusika kupekuliwa, kukamatwa na kutajwa hadharani?
Amefanya hayo matukio kwa kipindi kirefu bila kujulikana, amemiliki hizo video kwa muda mrefu bila kusambazwa, kwanini apekuliwe na kukamatwa halafu zisambazwe? Nani anazisambaza na lengo lake ni nini?
ANGALIZO
Sio sawa hata kidogo kujirekodi au kutazama video za ngono, na sio sawa kutembea na wake za watu au kufanya ngono ovyo ovyo.