Siyo kwamba 'hit men' wote wanaotumika kwenye Opereaheni za kidhalimu Kama kuua watu huko 'ndani ya wavaa Kaunda suti' huwa wanakuwa wameridhika kwa dhati kabisa kutoka mioyoni mwao, karibia maajenti wote Wanaotumika kwenye missions Kama hizo za 'assassinations' wanakuwa wamelazimishwa tu na wakubwa wao (makamanda wao) kwa kupewa tu amri na wao kutakiwa kuitekeleza. Nina mfano ulio hai kuhusiana na Mission Kama hiyo, jamaa mmoja anafanya kazi katikà taasisi moja kubwa alikuwa na Mgogoro wa ardhi dhidi ya 'Kiongozi mmoja wa Wavaa Kaunda suti' katikà Mkoa fulani hivi. Kiongozi huyo akatumia mamlaka/madaraka yake vibaya na kupanga Mpango wa Siri (assassination plan) dhidi ya mgomvi wake ili kumaliza Mgogoro uliokuwepo kati yao baada ya 'kiongozi huyo wa wavaa kaunda suti' kuona kwamba Mgogoro umemuelemea sana. Mpango ulisukwa vizuri Sana, tarehe ya 'mauaji' ilipangwa na hitmen wazoefu wakaandaliwa.Njia ya Mauaji (assassination method ) iliyochaguliwa na iliyopangwa ni kumuwekea sumu (Poisoning). Aidha, Surveillance kali ikaanzishwa ili kumuwinda jamaa na ili kuweza 'kumtegea mitego ya kifo.' Bahati njema Sana kwa jamaa Mungu na Malaika wote waliopo walikuwa upande wake katika kumlinda na kumtetea, jamaa akawa 'tipped' kuhusu Mpango wote ndio ikawa pona yake. Ilikuwa ni Mpango wa Mauaji wa hatari Sana, Hati ya kusafirisha maiti yake kurudishwa kijijini kwake tayari iliandaliwa, risala yake ya mazishi tayari iliandaliwa na ilikuwa auawe siku 27 kabla ya siku ya birthday yake. Ni hatari, hatari, hatari Sana kupita kiasi. Hiki ni kisa halisi kabisa na cha kweli.