Gwajima tapeli sana, hapo kwenye kuchanganya dini na siasa ndio simuelewi kabisa, sijui unaweza vipi kuwa mtumishi wa Mungu wa kweli halafu hapo hapo uwe unawajaza watu propaganda za kwenye siasa.
Gwajima siku zote ni msanii anaetumia fursa, hata body language yake inamuonesha kama mtu wa ulimwengu zaidi (ndio maana ana scandal za ajabu), na sio wa kiroho kama anavyotakiwa kuwa.
Sasa kaona atumie fursa ya siasa kwasababu ya jamaa yake wa nyumbani aliye madarakani, mwanzo alitumia uongo wa kufufua wafu awapate watu kwenye kanisa lake.
Akitaka heshima afanye kama alivyofanya Rais mpya wa Malawi, aache dini aingie kwenye siasa, lakini kuchanganya vyote viwili ni utapeli wa wazi.