Hizi ni nyakati ambazo wenye akili wanaogopa kuongea but wapumbavu wanajitokeza kwa ujasiri mbele kabisa kusambaza upumbavu, lakini historia itahukumu kwa haki naamini.
Hili ni tatizo kubwa sana awamu ya tano. Kuna kundi lililopewa kazi ya kusambaza upumbavu kwa kujua werevu wapo kimya.
Kila siku kuna mambo ya kusitikisha sana. Fikiria kwamba kuna watu wanaamini Tanzania pekee imepata ''Herd immunity' ya Corona. Kuna watu wanasambaza habari kuwa Tanzania kupitia dini imekabiliana na Corona. Yaani utadhani mahali kama Vatican , Meca, Brazili n.k. hakuna dini.
Hakuna anayejadili kuhusu Tanzania kupigwa pini kuingia nchi za EU licha ya matangazo kuwa hakuna Corona.
Juzi tumesikia kichekesho cha uchumi wa chini kati.
Gwajima, ana kipaji cha kufanya 'exploitation' kwa watu masikini na wenye dhiki.
Gwajima ana Chopper bado anakusanya sh 100 za watu wasiojua mlo wa siku.
Huu kama si utapeli ni nini? Yaani masikini wamchangie mafuata ya chopper
Wakati anaaminisha watu Yesu anawalinda kwa Corona na watoe sadaka, nje ya kanisa kuna kundi la 'walinzi'' likimsubiri. Akiondoka analindwa na wanadamu, si Yesu aliyewaaminisha watu wake.
Huu kama si utapeli ni nini!
Gwajima ameanisha watu Corona ni 5G iliyoletwa na Wazungu.
Anaokoteza hadithi za mitandaoni kuwalisha masikini na watu wasiojitambua. Tapeli la nguvu.
Juzi kuna video ikionekana amechukua maneno ya Martin Luther King '' I have a dream'' akisema ana ndotooo, kwamba misikiti itabadilika kuwa sunday school! .
Kisha anasema mwenye ndoto hafi hadi ndoto itimie. Tapeli limesahau MLK aliuawa kabla ya ndoto yake.
Leo tapeli anayedhulumu masikini kwa kukusanya sh 100 zao amechukua fomu kuomba Ubunge wa CCM
Kwa CCM ya leo si ajabu kabisa akapewa nafasi. Ni CCM isiyoweza kukemea vitendo na viashairia vya udini vya akina Gwajima na Bashite. Ni CCM inayoendekeza udini na ukabila, si ile ya umoja wa kitaifa.
CCM ya leo wasema hovyo, wapuuzi na wajinga wanaopandikiza chuki za Dini wana nafasi.
Ni CCM inayowaona Wapinzani kama tatizo kubwa sana la kitaifa !!
Ni CCM isiyojali umoja wa kitaifa bali matukio ya siku moja hadi nyingine.
Pascal Mayalla JokaKuu tindo