StudentTeacher
JF-Expert Member
- Jan 30, 2019
- 4,153
- 4,301
Mfano mzuri Shadraki,Meshaki na Abednego waligoma kutii maagizo ya 'kishetani' na Mungu akawa upande wao mwanzo mwisho.Mifano ipo mingi sana."Mamlaka halali".What a point!!!Hujasoma ukanielewa. Nimesema kuna wakati na yeye alikuwa muumini wa hiyo phrase ya mamlaka dhidi ya viongozi wenzake wa dini waliokuwa wakiikosoa serikali kuhusu demokrasia kipindi cha awamu ya 5. Ndiyo maana nikasema hii phrase inatumiwa vibaya na wanasiasa (out of context) kuhalalisha mambo wanayoyataka, lakini siyo fasili sahihi ya Biblia. Andiko la mamlaka kwenye Biblia halina maana mamlaka yoyote, bali 'mamlaka hahali' au 'mamlaka inayotenda haki' au inayowaunganisha watu au inayotimiza wajibu wake wa uongozi wa nchi kwa masilahi ya wote na siyo kwa masilahi ya kikundi fulani cha watu au eneo fulani la nchi. Yaani hakuna anayekuwa na ulazima wa kutii mamlaka mtu anayoona au anayoamini haitendi haki na kiongozi pekee katika kuamua ni 'certain conscience' (dhamiri yenye uhakika kuhusu jambo fulani). Hii ni aina ya dhamiri ambayo mbele ya jambo fulani na kwa wakati huo wa kuamua mtu anasikia sauti ya ndani mwake ikimwambia tenda au acha. Dhamiri ya aina hii kwa kadiri inavyokushawishi kutenda au kuacha matokeo yake huwa ni furaha (kama ukifuata dhamiri yako inavyokushawishi au huzuni kama ukifanya jambo kinyume na dhamiri yako inavyokushawishi). Baada ya kuamua kutenda au kuacha, mtu anatakiwa kujiridhisha (kujua) kama jambo alililolitenda au acha kutenda ni jema au la. Na kupata habari hapa maana yake ni kuwa na 'well-informed conscience' (dhamiri ya kweli - kuamua kutenda au kuacha kutenda jambo kwa vile unajua bila shaka ukweli au undani wake). Ukiwa na 'doubtful conscience' (dhamiri ya mashaka) hupaswi kufanya uamuzi wowote mpaka hapo utakapokuwa na uhakika wa jambo lenyewe (certain conscience).
Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app