AKILI TATU
JF-Expert Member
- Feb 10, 2016
- 2,659
- 2,827
Wakongwe wa tasnia ya habari akiwemo mkuu Pascal Mayalla mtanisaidia kujua ukweli wa hili.
Kwa muda mrefu redio na TV zimekuwa na hizi habari wanazoziita za kimataifa na wakati mwingine wanavuka na kuzichambua kabisa, kiukweli Sina Shaka na hilo, lakini Shaka inakuja wanatuletea habari za kimataifa ambazo hazina impact kwenye jamii yetu, mfano unakuta kuna tukio la ukabaji huko Syrian au labda ajali ya gari wamekufa watu wanne huko China, au magari yamegongana huko Afrika Kusini, sasa najiuliza habari kama.hizi Sisi wasikilizaji au watazamaji zinafaifa gani kwetu au ndio uvivu wa wahariri na upungufu wa mbinu za kutafuta habari za maana?
Lakini pia najiuliza, je huko nje ambalo tunashobokea Sana kuripotiwa habari zao nao wanashoboka kuripoti habari zetu hizi local mfano za kupanda na kushuka kwa tozo au Ile ya Rais Mwinyi kukutana na madaktari wa China juzi hapa?
Tunaambiwa miaka na miaka kuhusu habari za machafuko huko sijui wapi, lakini kila nikisikiliza najiuliza hizi habari kama hizo na zingine impacts zake ni zipi kwetu wasikilizaji, au ni lazima habari inaposomwa au kuandika lazima ziwepo hizo za kimataifa?
Au ni uvivu kwa wandishi wetu wa habari pamoja wahariri kuingia huko ndani ndani ya nchi na kutuletea habari maana akili yangu unakataa kuwa Tanzania hakuna habari mpaka kila ukifunguliwa redio au TV ukute wanatuletea hizo wanazoziita habari za kimataifa tena wakati mwingine hazina impact yeyote Ile Kwa jamii yetu au nchi kwa ujumla?