Habari hizi za kimataifa kwa manufaa ya nani hapa Tanzania?

Habari hizi za kimataifa kwa manufaa ya nani hapa Tanzania?

Leo nime sikiliza habari saa moja kamili clouds fm (habari za kimataifa) nimeipenda msomaji wa habari kasema Raisi wa congo DRC kamtuhumu wazi wazi Rwanda kwa kuvamia nchi yake.

Hii ili tokea baada ya Rwanda kuingiza majeshi yake nchini DRC kuwasaidia waasi wa M23 [emoji3] kinyume na makubaliano ya sheria ya kimataifa nime sahau sijui ni ya mwaka gani iliyo tungwa na kujadiliwa ... nimeasahau ali sema msomaji wa habari.

Hapo hapo Rwanda nao wana wa tuhumu serikali ya Tshekedi (Rasi wa DRC) kwa kufadhili kundi la waasi wa EFDL [emoji23][emoji23] ipo siku yaja hawa majirani zetu wata toana roho. [emoji30][emoji2296]

Kwa mtazamo wangu Rwanda ndio muonezi wa Congo nae ni kama ma beberu tu, ana waibia mali DRC ndio maana ana fadhili makundi kama M23 ili vita visiishe aendelee kupiga mali za DRC. Kagame ni boonge la snitch [emoji19]

NB: umbea kama huu kuupata kwenye Tv, Radio stations naona una faida kujua hali za majirani zetu na nini kinacho endelea huko over [emoji23][emoji482]
Hizi NI habari na zinafaaa ...lakini zile za sijui Rais WA Nigeria kasamehe wafungwa kwao...mara sijui Gambia wamefanya nini...nashanga Sana tukiletewa habari hizi...
 
Kwakuwa mimi siishi huko nje ni vigumu kulijibu hilo swali lakini kwa muktadha wa nguo nikivaa mimi wengine wakaifanya mjadala mkubwa nguo yangu hiyo kutokana na uzuri ama ubaya wake SI lazima nami nifanye hivyo kwa nguo zao
Lakini NI sahihi Kwa maslahi ya jamii...ukizingatia hapa.ndani tuko na mambo mengi yanafaa kuripotiwa na kufanyiwa follow up lakini yanaishia hewani...kuna kesi chungu laki na matukio ya kutosha ambavyo yangefaa kufanyiwa ufuatiliaji kuliko kujidamkisha na habari local za Sijui wapi huko...
 
In short habari ni aina fulani ya propaganda, kutoka na principal control what people know.

Kuhusu habari za kimataifa. Niliwahi kufwatilia bbc swahili kama mwezi hivi. Nilibaki nashangaa sana, na nazani hata wenzangu wengine humu mliduwaa. Yule salimu zio mzima, yeye habari zake ni kinyume na maumbile kwa kwenda mbele, akitoka mapadre anakuja mashehe, mara huku wameruhusiwa kufunga ndoa. Sijajua ni kutoka msukumo wake au mwajiri wake.
 
Hahaha.. inawezekana haswa Kwa hizi media ambazo zinakuwa owned na other countries kama DW, BBC, VoA And so far ..!
 
Wakongwe wa tasnia ya habari akiwemo mkuu Pascal Mayalla mtanisaidia kujua ukweli wa hili.

Kwa muda mrefu redio na TV zimekuwa na hizi habari wanazoziita za kimataifa na wakati mwingine wanavuka na
Ni upuuzi tu. ni kama hapa jf, kuna majuha wako bize na issue za urusi na ukraine. na wanabishana kabisa walivyo mazuzu
 
Lakini NI sahihi Kwa maslahi ya jamii...ukizingatia hapa.ndani tuko na mambo mengi yanafaa kuripotiwa na kufanyiwa follow up lakini yanaishia hewani...kuna kesi chungu laki na matukio ya kutosha ambavyo yangefaa kufanyiwa ufuatiliaji kuliko kujidamkisha na habari local za Sijui wapi huko...
Kumbuka hatuishi pekeyetu tuna rais wa hayo mataifa mengine wangependa pia kujua habari za kwao kama sisi tu tunapokuwa kwenye mataifa yao
 
Kumbuka hatuishi pekeyetu tuna rais wa hayo mataifa mengine wangependa pia kujua habari za kwao kama sisi tu tunapokuwa kwenye mataifa yao
Sawa..je media za huko nnje nako wanazingumzia hizi local news zetu kama ambavyo Sisi tunazizungumzia..!?
 
ni upuuzi tu. ni kama hapa jf, kuna majuha wako bize na issue za urusi na ukraine. na wanabishana kabisa walivyo mazuzu
Mkuu Utingo Hizi zina impacts Kwa uchumi WA dunia .so NI muhimu kujuzwa...nazozungumzia hapa NI zile local news za marekani, India kuzungumzwa hapa bongo kama habari za maana Sana kwetu...mfano WA hizo NI sijui Mbunge WA Washington amefariki dunia...mara sijui meya huko India ameoa kafanya sherekhe kubwa ...sijui mara huko afrika kusin kuna ajali ya malori,...sijui huko Canada kuna mvua imenyesha...hizi na zingine kama hizo zinafaida gani kwetu tukishajuu au kusikia..!?
 
Ndio sasa huko sio local news tena bali ni za kimataifa
Nakuelewa Sana bro . ...inamaana unataka kuniambia hizi habari za Mbunge kutumbuliwa...sijui kuzinduliwa Kwa kiwanda cha sukari bagamoyo ndio zisomwe UK au hata hapo Ghana kweli!?
 
Mkuu Utingo Hizi zina impacts Kwa uchumi WA dunia .so NI muhimu kujuzwa...nazozungumzia hapa NI zile local news za marekani, India kuzungumzwa hapa bongo kama habari za maana Sana kwetu...mfano WA hizo NI sijui Mbunge WA Washington amefariki dunia...mara sijui meya huko India ameoa kafanya sherekhe kubwa ...sijui mara huko afrika kusin kuna ajali ya malori,...sijui huko Canada kuna mvua imenyesha...hizi na zingine kama hizo zinafaida gani kwetu tukishajuu au kusikia..!?
Hazina impact tena. dunia imesha-jiadjust. kuzishupalia kama mnavyozishupalia ni kupoteza muda tu. hata news lines kama cnn na zingine hawazishobokei kama ilivyokuwa mwanzoni
 
Nakuelewa Sana bro . ...inamaana unataka kuniambia hizi habari za Mbunge kutumbuliwa...sijui kuzinduliwa Kwa kiwanda cha sukari bagamoyo ndio zisomwe UK au hata hapo Ghana kweli!?
Inategemea sina hakika
 
Wakisema habari ziwe za ndani tu, kuna muda utawaza hivi haya yanatokea kwetu tu mbona sijawahi kusikia nchi nyngine?

Lakini wakitoa na za nje inabalance habari, inasaidia kujua kumbe kuna nchi nazo ajali zinatokea pia kuna matukio ya kihalifu. Pia inasaidia kujua nchi nyingine wanatumia njia gani kupambana na changamoto zinazowakumba, hii inaweza kutusaidia na sisi kujifunza kutoka kwao.

Mwisho kabisa kuna watanzania wanaishi nje ya nchi (huenda ni kwenye hizo nchi) naye anafuatilia vyanzo vya habari vya nyumbani kwaiyo inamsaidia kupata habari za huko alipo kupitia vyombo vya habari vya Tz. Pia kama ni ajali au majanga mengine itasaidia wale watz wenye ndugu kwenye hiyo nchi husika kuwasiliana na ndugu zake kujua kama wapo salama kwenye hizo nchi.
Mkuu una akili sanaaaa.
 
Back
Top Bottom