Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Nyama ya nguruwe.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.

“Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.

Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.

“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule

Nyama yoyote isipoiva vzuri huleta madhara
 
View attachment 195801 Ni mojawapo ya aina nyingi ya wanyama wafugwao, mnyama huyu alianza kufugwa na mwanadamu zaidi ya miaka 2000 kabla ya yesu kuja hapa duniani, mnyama huyu amejizolea majina mengi sijui ni kwanini labda tu ya umaharufu wake,wengine humwita noah,mkuu wa meza ,hata kitimoto na mjomba mnene!! Cha kushangaza pia katika vitabu kama injiri na quraani pia vimemzungumzia mnyama huyu kila kitabu kimemzungumzia kwa kumtaja jina , tofauti na wanyama wengine kwani hata mwenyezi mungu katika vitabu takatifu nilivyovitaja hapo juu katika injiri ya yesu kristo ameonywa mwanadamu kutokula wanyama wasiocheuwa tena injiri ilikwenda mbali zaidi na kumtaja jina yaani Na NGURUWE!!!! Pia hata katika quraan mnyama huyu ametajwa kama afai kutumika kama kitoweo yaani ni haramu katika surat' tul- meda aya ya 3 mwenyezi mungu amekataza kabisa matumizi hata kufuga huyu mnyama, pia madaktari na watafiti wa magojwa yamebaini aina fulani ya mnyoo ambae upatikana katika huyu mnyama ambae usababisha ugojwa wa KIFAFA kwa mwanadamu endapo atakuwa na mazoeya ya kumtumia kama kitoweo

Acha story za magenge ya kahawa na kashata
 
Nyama ya nguruwe.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Akizungumza na mwandishi hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo.

“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii.

“Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.

Alisema athari za kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.

“Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha Profesa Lekule

Mungu alikataza nguruwe isiliwe et oooooh mbuzi katoriki
 
Mungu alikataza nguruwe isiliwe et oooooh mbuzi katoriki
Wanaotaka kula mbuzi wa kikatoliki waache wamle tu Huyu Nguruwe wakipatwa na maradhi ya kifafa watibabu tuko na bei ya kutibu huo ugonjwa wa kifafa ni shillingi Millioni 2 wakiwa wengi wagonjwa ndipo na faida ya waganga wa kienyeji kazi kwao walaji Mbuzi wa kikatoliki Koi Jr
 
Last edited by a moderator:
Heri mimi ninayekula mara moja kwa mwezi chances ya kupata inakuwa ndogo. Ila sasa nitasimamia mwenyewe achomwe mpaka nisikie tishhhh! nitajua tayari weshakufa.
 
Walawi 11:7-8

Hakika ni kuwa Agano la Kale katika Biblia imekataza ulaji wa nguruwe na akafanywa kuwa ni haramu:

"
Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama
yao wala msiguse mizoga yao" (Walawi 11: 7 – 8).
Agizo hilo limerudiwa katika

Kumbukumbu la Shari'ah 14: 7 – 8 na pia Isaya 66: 17. Na katika Agano Jipya, Yesu naye amesema
kuwa

hakuja kutangua shari'ah na mafundisho ya manabii bali kukamilisha
(Mathayo 5: 17). Kwa ibara hiyo ni

kuwa Yesu pia aliharamisha ulaji wa nguruwe.
Hata hivyo, Nabii Paulo ndiye aliyekuja akaenda kinyume na

shari'ah hiyo kwa kutoa agizo kwa barua aliyowaandikia Warumi:
"Basi, usiiharibu kazi ya Mungu kwa

sababu ya ubishi juu ya chakula. Vyakula vyote ni halali, lakini haifai kula chakula ambacho kitamfanya

aanguke katika dhambi"
(Waroma 14: 20).
Pia, "Katika kuungana na Bwana Yesu, nina hakika kwamba

hakuna kitu chochote kilicho najisi kwa asili yake"
(Waroma 14: 14).
Paulo amesema tena kuwa kila kitu

alichoumba Mungu ni chema wala hakuna kinachohitaji kukataliwa
(1 Timetheo 4: 3 – 5). Na Mwenyeezi

Mungu ndie anayejuwa zaidi.@
FALSAFA
 
Mimi nimefanya utafiti CHINA, POLAND,LONDON, AMERICA na JAPAN kuwa supu yakichwa cha nguruwe kinaongeza akili ya ziada kwa watumiaji utafiti huu umenifanya nipate PhD yangu pia ndiyo maana watu hawa niwagunduzi wazuri
 
utafiti huo si wa kweli kwa sababu nguruwe wana vimelea wa magonjwa wengi sana na hasa retroviruses ambao hawadhuriki hata baada ya kuchemsha/kukaanga/kupika nyama yake.Wengi wa hawa viruses wanaadhiri ubongo. kwa maana hiyo akili unayopigia chapuo itatoka wapi?
 
Kitimoto iliyoandaliwa vyema haina shida..huyo mdudu aliwe tu...
 
Nchini Tanzania nyama ya nguruwe ni maarufu katika maeneo mbali mbali ya starehe na imepewa majina mengi ,kama vile mkuu wa meza, kiti moto na mengineyo mengi.

Hata hivyo utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha kilimo cha sokoine ( SUA), umebaini kuwa walaji wa nyama ya nguruwe wako katika hatari ya kupata magonjwa kama vile kifafa kutokana na mnyoo Tegu uliopo kwenye nyama ya nguruwe.

Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga amezungumza na mtafiti wa magonjwa ya binadamu na wanyama Dkt. Boa Mathias Emanuel kutoka chuo kikuu cha SUA, na kwanza amemuuliza ueneaji wa ugonjwa huu.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom