Habari njema: Bei ya umeme kushuka kutoka Sh.600/= hadi Sh. 35/= kwa unit moja bwawa la Nyerere likikamilika

Umeongea mambo mengi ila Tanzania umeme ni ghari sana na wengi wanatumia kwa kuchaji simu na taa tuu tofauti na wenzetu ambao wanatumia kuchemsha maji na kupikia pia % kubwa watu wanakimbilia gesi kwa sababu umeme haushikiki ila baadhi ya Wafanyakazi wa Tanesco walikua wanapewa unit kadhaa bure kabisa...mikataba ya hovyo ndio inapelekea umeme kuwa ghari huko kwingine ni mbwembwe tuu...
 
Kwa uzoefu wangu hapa Tanzania. Usitarajie bei kushuka baada ya bwawa la umeme kukamilika kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukusanya hela kwa ajili ya kulipa mikopo iliyotumika kujengea mradi husika.

Rejea mifano ifuatayo:

1. Tuliambia miaka ya 2000 kwamba mkongo wa taifa wa mawasiliano ukikamilika utapunguza gharama za internet. Badala ya kupungua, gharama zikaongezeka baada ya mkongo kukamilika.

2. Wanasiasa walipokuwa wakiwashawishi wananchi wauelewe mradi wa gesi ya Mtwara, walikuwa wakisema umeme utashuka na gharama ya gesi ya kupikia itashuka pia. Lakini gharama za gesi zimepanda wakati gesi inachimbwa Mtwara.

3. Dangote alipoanza kujenga Kiwanda cha simenti Mtwara, wanasiasa wakasema simenti itashuka. Ikasemwa dangote alitaka kuuza simenti elfu 10. Kweli kiwanda kilianza kazi na mikoa ya ndani kabisa simenti iliuzwa elfu 14. Leo simenti katika mikoa hiyo inauzwa elfu 20.

4.. Miradi ya maji ya ziwa victoria ilipokuwa ikijengwa baadhi ya mikoa, wanasiasa walikuwa wakisema gharama zitashuka, lakini gharama zikaongezeka baada ya miradi kukamilika.

Kwa hiyo, kwa uzoefu tu wa maneno ya wanasiasa wa Tanzania tusitegemee bei ya umeme itashuka bwawa likikamilika, badala yake bei itapanda. Pia, SGR ikikamilika nauli ya treni itapanda.

Hii ndio Tanzania.
 
Mikataba ya hovyo ndio; lakini pia Production Capacity na hio Production anafanya nani, inamatter zaidi, kama tukifanya Production wenyewe wala hakuna sababu ya kuingia Mkataba na Kupe wa aina yoyote...

Kama utatumia Production ya HEP ambayo ina the cheapest running cost by none baada ya ujenzi kumalizika utaona kwamba kuna leeway kubwa zaidi ya kushusha bei....

Kama utajigeuza kuwa dalali ili ununue ili watu wapate faida ili na wewe uuze usitegemee bei itakuwa rafiki...

Hayo yote yanaweza yakawa rectified kwa Tanesco kuendeshwa kizalendo na sio sijui kufumuliwa na kusukwa upya kwa manufaa ya wachache...
 
Pana miaka kadhaa nyuma kampuni ya SA ndio ilikua inafanya ukarabati wa mitambo ya mtera wengine waliokua wanakuja kufanya hiyo Service ni Wazimbabwe na Watanzania walioajiriwa kule ukiangalia unaona hivi vitu tunaweza kufanya wenyewe ila pana mikono ya watu ipo mingi ndio maana unaona gharama zinakua kubwa kwa Nchi za SADC nadhani Nchi yetu umeme utakua ghari zaidi kupita hizo Nchi zingine..
 
Hizi sasa ni hujuma za wazi wazi kabisa
 
Kwa bei hiyo deni litalipika, au siasa inachukua nafasi yake hapa na danganya WaTz isiyoisha?
 
Kwa bei hiyo deni litalipika, au siasa inachukua nafasi yake hapa na danganya WaTz isiyoisha?
Tuseme unadaiwa Laki Moja kwa kukusaidia kununua mapipa nane ya maji ambayo yatakuwa yanajaa kwa mvua ili upate maji ya kunywa kwa mwaka mzima maisha yako yote....

Wewe kwa sasa matumizi yako ni mapipa manne ya maji, Je utawaambia majirani waje wachote maji kwa bei Tshs 100/= ili wakusaidie kulipa deni kwa kutumia hayo maji yote (ukizingatia wewe kuwapa kwako maji wanasaidia kununua hata viazi vyako kila wanapokuja) au utasema wakupe elfu 20, hivyo wewe kukosa hata hio Tshs 100/= na wateja wako wa mayai na hivyo kupelekea maji kutokutumika na kupotea bure kila mvua ikinyesha ?

In short kinachofanyika sasa ni kupigwa propaganda ili ionekane Bei unayolipa ni justified au Tanesco ndio mbaya ili iuzwe au kubinafsishwa....
 
Sio ajabu mpaka likikamilika kwa asilimia mia watanzania wote waishio sasa hawatokuwepo
 
Serikali ijikite kuunganishia watu umeme huko vijijini hadi ngazi ya kitongoji, watu hawana umeme kabisa, umeme uko mijini na kwenye vijiji vichache sana
 
N
Natabiri mradi huu utazinduliwa siku chache kabla ya uchaguzi nabaada ya uchaguzi mgao uko palepale
 
Ila kwa sasa bado haijawa habari njema, tunaendelea subiri hadi itakapokuwa habari njema yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…