Habari njema: SIDO Arusha watengeneza Hema la kujifukizia nyungu

Habari njema: SIDO Arusha watengeneza Hema la kujifukizia nyungu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Watanzania wameendelea kuwa wabunifu katika kujenga mikakati imara ya kukabiliana na janga hili hatari la Corona.

SIDO mkoani Arusha wametengeneza hema maalumu kwa ajili ya kujifukizia au ukipenda kupiga nyungu.
Hema hilo ni mfano wa kama kibanda kidogo cha turubai ambacho mhusika ataingia ndani yake akiwa na nyungu zake na kujifungia humo hadi nyungu zipoe.

Bei ya hema hizo inakadiriwa kuwa kati ya sh 350,000 na 400,000

Wito umetolewa kwa mashirika na taasisi zote mkoani humo kuona umuhimu wa kuwanunulia wafanyakazi wao hema hizo.

Source: ITV habari

My take; hongera mbunge wa Arusha mjini

Maendeleo hayana vyama!
 
AISEE NAOMBA LIPELEKWE MOJA KWA MOJA CHATO MKULU AKALIZINDUE
 
Sasa wewe kwa akili zako unaamini corona inakimbia mwilini kwa kupigiwa nyungu?
Kama unaamini hivyo basi mzazi/mlezi wako ada aliiharibu bure tu
Mimi nilifanya nikashusha homa na pua ikaacha kuwasha...Haitibu ila inakupa nafuu na baadhi ya dalili makali yanapungua au kupotea... Wewe jambo bado ni theory kwako,kwa wengine tushafanya fanya practical halafu unaleta kimbelembele.
 
This is devil statement, mtu mwenye akili timamu huwezi kumtukana 'maybe kiongozi flani kwa kauli kama hii'
Mbunge Lema awezi kusapoti uchawi wa mjinga mmoja aliyeko kijijini kisa corona.
 
Watanzania wameendelea kuwa wabunifu katika kujenga mikakati imara ya kukabiliana na janga hili hatari la Corona.

SIDO mkoani Arusha wametengeneza hema maalumu kwa ajili ya kujifukizia au ukipenda kupiga nyungu.
Hema hilo ni mfano wa kama kibanda kidogo cha turubai ambacho mhusika ataingia ndani yake akiwa na nyungu zake na kujifungia humo hadi nyungu zipoe.

Bei ya hema hizo inakadiriwa kuwa kati ya sh 350,000 na 400,000

Wito umetolewa kwa mashirika na taasisi zote mkoani humo kuona umuhimu wa kuwanunulia wafanyakazi wao hema hizo.

Source: ITV habari

My take; hongera mbunge wa Arusha mjini

Maendeleo hayana vyama!
Korona imekwisha wao ndiyo wanashituka, watatumia kugemea asali.
 
Back
Top Bottom