Habari za usiku ndugu zangu naomba ushauri

kitoto wa vitoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
375
Reaction score
410
Nina mtoto wa kike ana MWAKA na mwezi 1 alizaliwa akiwa na changamoto ya kulia sana
Tulimuona Dr mara kadhaa
Dr wengi hawakuona ugonjwa Ila baadae tuligundua ana TB ya mapafu alipata matibabu Ila bado afya yake bado imedhoofika sana tumempa kila aina ya lishe
Ila bado uzito wake ni ule ule pia hajatambaa Wala kutembea
Ila anakaa tu
Watu wengi hudhan amebemendwa Ila si kweli je nifanye nini?
Nisaidieni wataalamu wa afya
 
Nenda muhimbili au hindumandal hospital zote zipo Dar... Ila anza na Hindumandal
Mungu ni mwema aendelee kuimarisha afya ya mtoto, usiogope mtumainie Mungu muweza yote
 
Kubemendwa ni nadharia tu ila hakuna kitu kama hicho, jitahidi umpate Daktari mzuri specialist wa watoto na pia usitake matokeo ya faster faster...mtoto atapona na kuwa mzima kabisa
 
Ana uzito wa kilo ngapi jwa sasa maana kwa Mtoto wa umri huo hutakiwa kwa wastani awe na kilo7-11, pia jitahidi Mama ale vizuri amnyonyeshe Mtoto maziwa ya kutosha na kwa umri huo huebda hashibi unaweza kumuongezea na uji mwepesi sana wa dona
 
Nina mtoto wa kike ana MWAKA na mwezi 1 alizaliwa akiwa na changamoto ya kulia sana
Tulimuona Dr mara kadhaa
Dr wengi hawakuona ugonjwa Ila baadae tuligundua ana TB ya mapafu alipata matibabu Ila bado afya yake bado imedhoofika sana tumempa kila aina ya lishe
Ila bado uzito wake ni ule ule pia hajatambaa Wala kutembea
Ila anakaa tu
Watu wengi hudhan amebemendwa Ila si kweli je nifanye nini?
Nisaidieni wataalamu wa afya

Pole sana.

Mojawapo ya madhara ya TB ni mtoto kuwa na ukuaji hafifu (uzito mdogo nk). Naamini atakuwa amepimwa pia magonjwa mengine ya maambukizi na hata yale ya kuzaliwa nayo.

Kwa umri wa mwaka mmoja hatembei ni tatizo kubwa ambalo mpaka sasa ulitakiwa wewe kama mzazi umekwishaelewa kwa nini yuko hivyo. Sijajua kama alipozaliwa alipata shida yoyote ( alichelewa kulia baada ya kuzaliwa?).

Ni muhimu sana umpeleke mtoto wako hospital kubwa ili akaonwe na daktari bingwa wa watoto (pediatrician) ili aweze kuchunguzwa na kufanyiwa vipimo ili kuweza kubaini ugonjwa unaomsumbua.

Kila la kheri.
 
Hi, vipi mtoto ameanza kuongeza? Ukijatibu kuongea naye je anaelewa baadhi ya maneno like kuita baba, mama, acha nk?
Kama jibu ni ndio basi kwa 50% yupo vizuri kwenye ustawi wa ubongo.
Pia kunahaja yakumpima matatizo ya tumbo hasa utumbo ndogo ili kujiridhisha, Unahitaji kumboreshea lishe na mazoezi ni DM
 
Nenda muhimbili au hindumandal hospital zote zipo Dar... Ila anza na Hindumandal
Mungu ni mwema aendelee kuimarisha afya ya mtoto, usiogope mtumainie Mungu muweza yote
Ameni
P
Kila la kheri.

Pole sana.

Mojawapo ya madhara ya TB ni mtoto kuwa na ukuaji hafifu (uzito mdogo nk). Naamini atakuwa amepimwa pia magonjwa mengine ya maambukizi na hata yale ya kuzaliwa nayo.

Kwa umri wa mwaka mmoja hatembei ni tatizo kubwa ambalo mpaka sasa ulitakiwa wewe kama mzazi umekwishaelewa kwa nini yuko hivyo. Sijajua kama alipozaliwa alipata shida yoyote ( alichelewa kulia baada ya kuzaliwa?).

Ni muhimu sana umpeleke mtoto wako hospital kubwa ili akaonwe na daktari bingwa wa watoto (pediatrician) ili aweze kuchunguzwa na kufanyiwa vipimo ili kuweza kubaini ugonjwa unaomsumbua.

Kila la kheri.
Tumeanzia hospili ya icc tukaandikiwa hospitali kubwa ya mount meru
Wakampima tukaandikiwa hospitali ya moyo ya jk napo tulienda alipimwa kila kitu Ila hawakumkuta na shida yyte japo kwa Arusha tuliambiwa moyo wa mtoto upo sehemu ambayo siyo yenywe
Tukarud Arusha bila suluhisho anaendelea kuumwa tukampeleka NSK ndo wakaenda kugundua ana TB ya mapafu tukianza tiba Ila mambo mengine kama kuchangamka kula na kupunguza kulia Ila haongezeki uzito
 
pole kwa kuuguza, ukipata nafasi jaribu kwenda regency medical centre umuone daktari raheem.
 
Back
Top Bottom