Tetesi: Habari zaanza kuvuja kuhusu zilikoenda Trilioni 1.5 "zilizopotea"

Tetesi: Habari zaanza kuvuja kuhusu zilikoenda Trilioni 1.5 "zilizopotea"

Haya mambo walitakiwa wapate majibu kabla hawajawasirisha ripoti kwa wanachi. Walichokifanya utadhani ni waajiriwa wapya au hawana uzoefu na shughuli za serikali. Wanasema CAG aliwasilisha ripoti kwa rais na imekaa kwa muda wa siku 21 kabla ya kuwasirishwa bungeni. Kwa muda wote huo wangetafuta majibu ya kuridhisha kabla ya kujidhalilisha kiasi hicho.
 
Attachments

  • IMG-20180510-WA0010.jpg
    IMG-20180510-WA0010.jpg
    20 KB · Views: 32
Habari kutoka vyanzo vinavyoaminika zimekuwa zikititirika juu ya ukweli kuhusu zilikoenda zile Trilion 1.5 ambazo zilionekana kama zimeyeyuka hewani, na kutolewa maelezo yasiyoridhisha na serikali.

Habari zilizopo ni kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo zilipelekwa katika matumizi ambayo mamlaka toka juu iliamua yasiwekwe wazi, na kikubwa cha matumizi hayo yakiwa ni mambo ya ki intelijensia/usalama. Habari zimezidi kuanisha kwamba kwa mara ya kwanza toka nchi hii ipate uhuru, kumekuwa na matumizi ya kutisha katika idara zote zote za serikali zinazohusiana na mambo ya usalama zaidi sana ya fedha wanazokuwa wakitengewa.

Pia kumekuwa na ajira nyingi zisizofuata utaratibu na kuanzishwa kwa vitengo ndani ya vitengo ambavyo vingi sio rasmi na hivyo matumizi ya fedha za vitengo hivyo hayawezi kuwekwa wazi. Watu wengi wemeajiriwa katika idara hizi zisizo rasmi katika mazingira ya kibinafsi na maagizo kutoka juu badala ya kufuata taratibu rasmi za serikali, na wamekuwa wakitengewa fedha kwa ajili ya "kazi" zao.

Habari zimezidi kudai kwamba hata wakati wa awamu ya Nyerere ambapo kulikuwa na kiwango cha juu cha mambo ya intelijensia na usalama kutokana na Tanzania kuwa kitovu cha mambo ya ukombozi wa nchi za Afrika hatukufikia matumizi ya kiasi hiki. Mbaya zaidi mengi ni matumizi ambayo hayajainishwa na kufuata tarataibu za matumizi ya fedha za serikali, na hayawezi kuhojiwa na mtu yeyote wala kukaguliwa hata na CAG. Habari zimesema kuwa ni kama kwa sasa kuna "obsession" ya mambo ya usalama na intelijensia, na watu wanaotumikia katika sehemu hizi ambazo nyingine sio rasmi wamepewa uhuru wa kutumia fedha wanavyopenda.
Kumbe ni TETESI basi endelea na tetesi zako!!
 
Mkuu, tena umenikumbusha! Habari zilizopo zinasema pia kwamba pia kumekuwa na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya mambo ya kishirikina, kutia ndani waganga wa kienyeji. Nimeona nikiweka hata hilo watu watadhani ni porojo! Lakini huo ndio ukweli!
Nasikia kila tarehe 15 ya kila mwezi waganga maarufu chini ya Bashite huenda Ikulu kufanya yao... Bashite ndio mtu aliyemtafutia hao waganga JIWE... Ndio maana Bashite na Jiwe ni kama chanda na Pete
 
Mie sio mtaalam ila kwa vyovyote vile, uwajibikaji kwenye hii 1.5 T hauwezi kukwepeka. Hapo kuna mawili, CAG ametudanganya (hajui kazi yake) au serikali wanaficha kitu.

Kama manunuzi ya ndege na matumizi mengine hayakupitishwa na bunge, unategemea repoti itakuwa sawa?

Kwa vyovyote vile. Kuna upande inabidi utoe maelezo. Hii ya kusingizia vyombo vya usalama itazima mjadala kirahisi sana. Ni kama ilivyotokea ile boat ya kwenda Bagamoyo, hairuhusiwi kujadili.

Nanadhani hakujua km kuna kitu kinaitwa ukaguzi

Nauliza tuu hivi ule uwanja umeshakuwa tayari?
 
Hivi unajua kusoma? Umeambiwa sehemu kubwa ya Trilioni 1.5 wewe unakurupuka kuwa ni sehemu yote ya Trilioni 1.5. Huko zilokoenda nyingine tutawajulisha taratibu, bado tunapewa taarifa. Na nani kasema zilichukuliwa kwa miezi miwili? Hata sehemu iliyotimika kwa mambo ya waganga wa kienyeji hatutaisema. Kwani mlipewa invoice kwa huduma zao?
Hivi ulishawahi kushika zaidi ya elfu 35?

Trillion 1.5 ikitolewa kwenye system kwa uchumi kama wa Tanzania nchi lazima ifilisike Ile pesa ya escrow isiyozidi hata billion 350 ilianza kuchotwa kuanzia enzi za mwinyi hii trillion 1.5 ndio ichukuliwe kwa miezi 2?

Huu utumbo mwingine kwamba hiyo pesa inalipia mshahara ya mambo ya Usalama ndio utaahira kabisa, wafanyakazi wote Tanzania nzima zaidi ya laki 5 wanalipwa mshahara hauzidi billion 500 kwa mwezi

Nyie mataahira mnadanganyana hapa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa siri na pesa anazotoa Rais kwa wananchi ndio zimegharimu trillion 1.5

Lazima uwe maiti ndio uamini hii mavi

Kumbe zilichukuliwa ndani ya miezi miwili. Report haikusema haya wala hakuna mtu mwingine aliyewahi kusema haya. Hivyo unaelekea kuna kitu unajua, hebu funguka tusikie
 
Huo ni uongo! Ni ajira kiasi gani zimetengenezwa za kugharimu 1.5T Tzs hata kama mmenunua vifaa??? Wafanyakazi wote wa Umma wanalipwa fedha kiasi gani? Hapa mnajaribu kutengeneza mwelekeo mpya wa upepo.
 
Kama unashindwa kuona kwamba maelezo yalitengenezwa rasmi ili "uelewe na kuamini", basi wewe na wengine kama wewe ni watu wa kuhurumia sana. Jiulize kwa nini maelezo hayo hakupewa CAG, na kama alipewa kwa nini hakuyaweka kwenye ripoti yake. Licha ya hivyuo, habari zinasema sehemu kubwa ya zile Trilioni 1.5, sio zote.

Na kama ni kweli nchi ya jirani wanasaidia mambo ya usalama, ni rahisi sana kufikisha Trilioni 1.5.

unajua one point five Wewe?
 
Ha ha haaaaaa,, wizi umehamishiwa JWTZ atakayehoji ajue anahoji kifaru cha jeshi!!
 
Hizi ni propaganda za kuwadanganya watanzania, ccm imekula hio hela kwa ajili ya uchaguzi mikuu 2020
 
Habari kutoka vyanzo vinavyoaminika zimekuwa zikititirika juu ya ukweli kuhusu zilikoenda zile Trilion 1.5 ambazo zilionekana kama zimeyeyuka hewani, na kutolewa maelezo yasiyoridhisha na serikali.

Habari zilizopo ni kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo zilipelekwa katika matumizi ambayo mamlaka toka juu iliamua yasiwekwe wazi, na kikubwa cha matumizi hayo yakiwa ni mambo ya ki intelijensia/usalama. Habari zimezidi kuanisha kwamba kwa mara ya kwanza toka nchi hii ipate uhuru, kumekuwa na matumizi ya kutisha katika idara zote zote za serikali zinazohusiana na mambo ya usalama zaidi sana ya fedha wanazokuwa wakitengewa.

Pia kumekuwa na ajira nyingi zisizofuata utaratibu na kuanzishwa kwa vitengo ndani ya vitengo ambavyo vingi sio rasmi na hivyo matumizi ya fedha za vitengo hivyo hayawezi kuwekwa wazi. Watu wengi wemeajiriwa katika idara hizi zisizo rasmi katika mazingira ya kibinafsi na maagizo kutoka juu badala ya kufuata taratibu rasmi za serikali, na wamekuwa wakitengewa fedha kwa ajili ya "kazi" zao.

Habari zimezidi kudai kwamba hata wakati wa awamu ya Nyerere ambapo kulikuwa na kiwango cha juu cha mambo ya intelijensia na usalama kutokana na Tanzania kuwa kitovu cha mambo ya ukombozi wa nchi za Afrika hatukufikia matumizi ya kiasi hiki. Mbaya zaidi mengi ni matumizi ambayo hayajainishwa na kufuata tarataibu za matumizi ya fedha za serikali, na hayawezi kuhojiwa na mtu yeyote wala kukaguliwa hata na CAG. Habari zimesema kuwa ni kama kwa sasa kuna "obsession" ya mambo ya usalama na intelijensia, na watu wanaotumikia katika sehemu hizi ambazo nyingine sio rasmi wamepewa uhuru wa kutumia fedha wanavyopenda.

Sawa sawa. Lakini mimi nawasubiri hawa wafuatao watuletee habari kamili ambayo imethibitishwa:

1. Evarist Chahali

2. Mzee wa "Sauti Kubwa" kipaza sauti cha yasiyoweza kuandikwa, Ansbert Ngurumo.

Nina hakika, wako "chimbo" na amini msiamini watakuja mpaka na majina ya benki ziwe za nje ama ndani na A/C No walikoficha hizo pesa za walala hoi, Watanzania!!

Namtahadharisha Gavana wa BoT wa wakati ule (2015 - 2017), akae mkao wa kuishi maisha ya ki - Daudi Balali tuliyeambiwa "alikufa" lakini mpaka leo hielweki kaburi lake liko wapi....!!

Tanzania ya leo inaongozwa na "mumiani", acheni kabisa!!
 
Back
Top Bottom