Habarini wakuu hivi nyumba kama hii inaweza gharimu sh ngapi hadi finishings?

Habarini wakuu hivi nyumba kama hii inaweza gharimu sh ngapi hadi finishings?

Joined
Dec 22, 2023
Posts
20
Reaction score
21
Interior Design Plan 12x11m With Full Plan 3beds - Samphoas Plansearch  0E6.jpeg
Habarini wakuu hivi hii nyumba inaweza gharimu sh ngapi mpaka finishings? Je inachukua tofali ngapi? Na kwa msingi (foundation) inaweza gharimu sh ngapi (ufundi+building materials). Msaada jamani nimechoka kuishi upangajini. Mimi ni kijana mpambanaji nipo mjini daslam.
 
Hii nyumba ni ya miaka ya vita ya Kagera!! Kanopi za zege?? Tafuta ramani inayoeleweka. Konakona kibao sizizo maana. Vyumba lukuki na havieleweki. Public Toilet imetazamana na dining room, jiko sijui ndo liko wapi??

Huu ni ujinga

Tupa kule
 
Nyumba haina shida ila ndan imekatwakatwa Sana
 
Kwahiyo nyumba milioni 50 inaweza isitoshe labda kama atatumia materials cheap sana. Kuezeka tu hiyo paa inaweza kwenda mil

View attachment 2963464Habarini wakuu hivi hii nyumba inaweza gharimu sh ngapi mpaka finishings? Je inachukua tofali ngapi? Na kwa msingi (foundation) inaweza gharimu sh ngapi (ufundi+building materials). Msaada jamani nimechoka kuishi upangajini. Mimi ni kijana mpambanaji nipo mjini daslam.

Huyu aliyekuambia 50 tena kakuonea aibu. Nyumba hii ni kubwa na finishing yake ni ya kisasa.

Hesabu za haraka haraka za finishing

Tiles kama nazoziona kibarazani ni imported = nyumba nzima utatumia kwenye 15m

Kuezeka bati grade safi = 15m

Madirisha ya aluminium = weka chini sana 5m

Milango nyumba nzima = weka 5m

Ukiweka AC (Mfano) , kila chumba na sebule = 7 to 9m

Tuseme nyumba from msingi ulisimamisha kwa 35m

Jumla ndogo: 47 + 35 = 82

Hiyo landscaping hapo nje, weka 5 to 15m (sijui ukubwa wa eneo husika)

Hapa hakuna plaster, skimming, wiring ya umeme, plumbing, vifaa vya maji, umeme n.k

(Nina uzoefu kwenye kusimamia miradi ya aina hii kwa mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania).
 
Kaka umeongea ukweli mtupu,mwenye akili akusililize,nimetoka kwenye ujenzi karibuni,kila ulichoongea hapo ni ukweli,milion 50 kwa hiyo nyumba HUMALIZI.
 
Duuu....mbona parefu?
Ni zaidi ya hapo inaweza kuchukua hata zaidi ya milioni 60 kutegemea na location mtu alipo maana bei za materials hutofautiana na malipo kwa mafundi pia hutofautiana.
Hiyo milioni 50 ni kwa mtu mzoefu ambaye alishawahi kujenga anajua jinsi ya kuminyana na mafundi pia anajua wapi akanunue materials kwa bei nafuu bila kuongezewa gharama na mafundi ili kusevu pesa
 
Back
Top Bottom