1. Alikuta marais wenye akili wameua shirika la ndege, yeye akalifufua na kununua ndege 11 tena kwa cash. Huyu ni kichaa mzuri.
2. Alikuta wenye akili wameshindwa kuja na suluhu ya kudumu ya tatizo la umeme. Kichaa huyu akajenga Bwawa la Mwl Nyerere.
3. Alikuta maelfu ya watumishi hewa na matapeli waliokuwa na vyeti feki. Kichaa akawatembezea rungu, wakaanguka chalii.
4. Alikuta Reli yakati ikiwa hoi bin taaban baada ya marais wenye akili kushindwa kuiendesha. Kichaa akaanza kujenga reli ya SGR ili wenye akili wasafiri kwa raha.
5. Alikuta changamoto kubwa ya foleni Dar baada ya wenye akili kusema kuwa foleni ni kipimo cha maendeleo. Kichaa akajenga Kijazi, Mfugale na Tanzanite ili wenye akili wawahi kufika waendapo.
6. Alikuta wenye akili wanaendelea kuendesha serikali yenye ofisi Dar wakati makao makuu ni Dodoma. Kichaa akawahamishia wote Dodoma kwa lazima na kuanzisha ujenzi wa mji wa serikali.
7. Alikuta wenye akili wanatumia ikulu waliyojengewa na wakoloni, Kichaa akaamua kujenga ikulu mpya Chamwino tena ikajengwa na Wanajeshi wazalendo.
8. Alikuta huduma mbovu za Afya. Kichaa akajenga Hospitali kubwa za kanda Njombe, Mtwara, Mara na Geita + Hospitali za rufaa 67 na vituo vya Afya 1000+. Huyu kweli alikuwa chizi.
9. Alikuta watumishi wa Afya na Matajiri wanaishi kwa mazoea na kuwadharau raia wenye hali duni. Kichaa akafanya matajiri wawaogope na kuwaheshimu maskini vibaya mno.
10. Alikuta wenye akili wanatumia saa kadhaa toka Kigongo kwenda Busisi akawajengea daraja wapite fasta.
11. Alikuta tatizo kubwa sana la maji mkoani Arusha, akawajengea wajanga wa R chuga mradi wa bilioni 500 sahivi lema anaogelea tu huku anamtukana kichaa.
12. Alipanua bandari zote na kusisitiza kuwa tunaweza kutumia akili zetu kuziendesha kwa ufanisi lakini wenye akili wakasema sisi hatuwezi wakawapa waarabu na lile tapeli la India linalotafutwa na Marekani, yes lile lililofukuzwa hapo Kenya.
Hapo sijazungumzia barabara, meli n.k