Hadhari: Baadhi ya Barabara Morogoro zimefurika maji

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimezidi kuleta athari kubwa kwa wananchi, uchumi na miundombinu. Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza uwepo wa mvua mikoa ya Morogoro Iringa, Ruvuma, Songwe, Mbeya na Njombe nk, hivyo kama raia wema ni vyema kupeana taarifa barabara korofi ambazo zimekumbwa na mafuriko ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Taarifa nilizonazo, maeneo ya Mikese, Kwa Mangwair, Makunganya, Silwa na Mtanana, kote maji yanakatisha barabarani. Hivyo kama una safari itakayokuta kupita njia hizo vizuri ukaenda kwa tahadhari. Usidharau kabisa maji yanayokatisha barabarani.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
Ubarikiwe [emoji120]
 
Duh hizi mvua za mwaka huu balaa!
 
Mpaka El Nino imalizane na sisi kila mkoa utaonja mafuriko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…