Reli zetu hatujengi kuwanufaisha majirani, tunajenga kwa manufaa yetu wenyewe kwanza, halafu majirani wanapata makombo yetu. SGR haikujengwa kwenda Rwanda, bali ilijengwa kwenda Mwanza, na Kigoma baadaye. Rwanda, Uganda, Burundi na DRC watajiunganisha kwenye SGR yetu kwa kushirikiana nasi siyo kuwa tumawajengea.
TAZARA ilijengwa mwaka 1970 kwa ajili ya kuifanya Zambia isiwe tegemezi kwa nchi za Rhodesia, Mozambique, and South Africa ambazo zilikuwa hazijapata uhuru wakati huo. Baada nchi zote tatu hizxo kupata Uhuru, Zambia imekuwa haiitegemi TAZARA sana kwani inaweza kutumia bandari za Beira, Maputo, Richards Bay na Durban. TAZARA ilikuwa ni ubia kati ya Tanzania na Zambia kwa mkopo kutoka China; kwa hiyo uamuzi wowote wa kuboresha TAZARA siyo wa serikali ya Tanzania tu, ni lazima Serikali ya Zambia ihusike pia. Uamuzi wa kuboresha reli za TRC ni wa serikali ya Tanzania tu; tutaamua kwa wakati tunaoona unatufaa