Hadithi: Madam President

Hadithi: Madam President

MADAM PRESIDENT 06

Sasa nilipata picha kuwa wale waliokuja kutuvamia juzi na kupuliza dawa walikua wametumwa na madam kuja kuiba picha na Cheti Cha ndoa, pengine madam alitaka kujiridhisha baada ya kupeleleza na kujua nimeoa Sasa alitaka kupata uthibitisho...

Niliwaza Kisha nikampigia Simu mke wangu kuwa nimekosa pia ..nilibadili nguo Kisha nikaona nitumie Ile piki piki kupigia misele, niliangalia mafuta na kukuta yapo ya kutosha nikaondoka na kwenda mjini kwa Shemeji yangu Aida.

Niliwasili baada ya muda mfupi na kumkuta akiwa nae anarudi


"Haya wewe mzungu vipi Tena za siku "

Alitabasamu baada ya kuniona alifungua akaingia ndani


"Shemeji yake Mimi nimekuja kula njaa inauma Sana"

Nilisema huku nikisogea kwenye friji kuangalia kinywaji....


"Usijisumbue mwenzangu Leo walikuja hao wajomba zako wamekomba friji lote kaa hapo nikuangalizie kinywaji dukani"

Alisema Tena akiingia chumbani,
"Halafu Shemeji yake cheki samaki Basi Nina hamu na ugali samaki leo!"
Nilisema nikikaa kwenye sofa pale sebuleni baada ya dakika kadhaa Shemeji Aida alirudi na kutengeneza chakula Kisha nikamwambia kilichonipeleka..


"Shemeji yake Nina Shida kidogo Kuna kitu unisaidie, nataka nikutoe kidogo hapa mjini ukakae na mdogo wako mpaka atakapojifungua ni zaidi ya miezi miwili kutoka Sasa"

"We mwanaume ! Unaniletea balaa gani Tena, na nyumba yangu namuachia Nani Tena!"

"Hahaha Shemeji yake Sasa hapo unatakiwa ujiongeze, unajua kuwa kila nikija hapa nikikuletea Shida najua unanisaidia 100%, na kila nikija ujue Sina sehemu Nyingine ya kwenda Tena!"

Nilisema kwa upole,

"Shemu unajua kabisa naweza kukusaidia, majukumu yangu yaani na siwez kuacha nyumba bila mtu"

"Yule mdogo wako Aisha vipi kwanini asije kukaa hapa halafu wewe na wajomba muende huko mkakae ,Ni nyumba kubwa tu usijali na itakuwa poa kukiwa na watu wengi wengi, Kama itakuwa Shida pia tutafute mtu alinde nyumba tumlipe!"

Nilisema

"Mh mpaka unasema hivyo kweli umetaitika Shem, sikiliza kesho asubuhi saa 4 nitakupigia kukupa jibu"..

Alisema.

"Shemeji yake, nakutegemea sana Kuna Mambo yakimalizika salama baada ya hiyo miezi miwili utapata zawadi yako nzuri kabisa"

Nilisema.


"Kwahiyo umeshamtoa Mary hapa mjini?"
Aliuliza

"Ndio Tangu Juzi, unajua baada ya wale wezi kutuvamia nikaona hapa mjini hapamfai Tena"

Nilimalizia


******************

Nilirudi mjini na kuzunguuka zunguuka kwenye mitaa huku nikiomba Mungu Aida akubali kwenda mabatini.

Niliamua kwenda kulala nje kidgo ya mji kwa siku hii ya Leo...

"Nitaishi Kama kunguru Hadi lini"

Niliwaza nikiigia kwenye gesti hii ya lala salama.


****************

Kama nilivyowaza Shemeji Aida alikubali kwa masharti kuwa ataondoka na watoto wake kwa bahati amepata shoga yake ambaye atamuachia nyumba ...

Nilimpigia mke wangu kumueleza kuhusu ujio wa Aida na watoto wake,

Kisha nikamtafuta Jose ili jioni ampeleke.

"Sasa kazi inaweza kuanza"

Ilipita wiki moja na nikawa natembelea Ile piki piki kupiga misele tu, mwishowe nikaona siwezi kulala vichochoroni kila siku,
Siku hiyo jioni kwenye majira ya saa 12 niliingia kwenye kibanda Cha kutoa huduma za mtandao nilikua na taarifa fulani ya kutuma Wizarani..


Nilishangaa kuona ujumbe mwingine ambao kwasasa niliweza kujua umetoka kwa Jacob ...

"Wazee wa Ngwasuma"


Uliandikwa hivyo tu...

Kwa haraka nikawaza maana yake na mahali niliposikia Hilo neno


Nilimaliza kutuma taarifa zangu Kisha nikatoka nje..

Baadae nikakumbuka maneno haya anayatamka DJ Mark Yule ambaye atafsiri Filamu lakini kabla ya kusema wazee wa Ngwasuma huwa anaanza na neno "wanakuja, wazee wa Ngwasuma"


Akimaanisha watu katili, wauaji n.k...

"Kwa maana hiyo wamekuja"

Nilijisemea

Nilitembea hatua kadhaa na sikutaka kununua chakula badala yake nilitamani kwenda kupika nilipiga hatua kadhaa kwa kujiamini na tayari Giza lilikua lishaanza nilikua nakaribia mitaa ya kwangu wakati Gari lililokua na vioo vyeusi lilipopaki pembeni yangu

Upande wa dereva alishusha vioo na kuniita...


"Samahani Broo tunauliza kwa afisa Elimu bwana Ruta, "

Alisema.

"Ah hamko mbali Sana nyoosheni na njia hii hii mkifika pale darajani Kuna nyumba kubwa yenye geti jeusi mkono wa kulia ndio hapo hapo"

Nilisema huku nikitaka kuendelea na Safari yangu..

"Sasa Broo si unaelekea huko huko ingia Basi utusaidie sisi Ni wageni kabisa"

Alisema huku akifungua mlango..

Sikujiuliza Mara mbili nikaingia kwenye Gari na Sasa nilijikuta natazamana uso kwa uso na mitutu ya bunduki!

Zaidi ya dereva kulikua na watu wengine watatu ambao walifunika nyuso zao huku wakiwa na bunduki zao

Waliniweka Kati Kati na Gari ikageuzwa kurudi mjini....


"Mnafanya makosa Sana jamaa!"

Nilisema kwa kujiamini..


"Ndio tumefanya makosa maana tulitakiwa tukukamate Tangu siku Nne zilizopita mbwa wewe"

Mmoja alisema huku wenzake wakicheka..
Mmoja alinisachi mfukoni na kutoa waleti pamoja na simu zangu mbili,

Kisha wakanifunga kitambaa usoni wakati nataka kupambana nao nivue kile kitambaa nikahisi kuchomwa na kitu chenye ncha Kali mkononi na taratibu nikajikuta nalegea na Kisha kupoteza fahamu.

*******************

Nilikuja kuzinduka baadae na kujikuta Nikiwa kwenye chumba kimoja kikubwa kulikua na kiti mbele yangu na nilikua nimefungwa kamba mikononi na miguuni na kutupwa sakafuni..

Nilijaribu kufungua macho kijanja kuangalia huko na huko lakini sikuona mtu...
Nilijaribu kujinyoosha nyoosha na sikujisikia maumivu yoyote yale ...

Ni baada ya muda kidogo aliingia jamaa mmoja akaja kunifungua kamba Kisha akaninyanyua nilisimama mwenyewe Kisha akanitanguliza kwenye chumba kingine ambacho kulikua na chakula

"Kula aisee"

Yule jamaa alisema

Nilisogea pale mezani nikapiga ule msosi kwa spidi ya ajabu nilipomaliza nikapewa nguo za kubadili Kisha nikapelekwa kwenye chumba kingine nikaoga nikabadili nguo Kisha nikatolewa kwenye Ile nyumba na kuzunguuka kwenye nyumba iliyokuwa pembeni...


Sasa kulikua na jamaa mmoja mbele mwingine nyuma tukapanda kuelekea kwenye chumba kimoja kilichokua ghorofani,

Tulikaa pale sebuleni kwa dakika kadhaa baadae mngurumo wa Gari ukasikika....

"Kaa Hapo "
Mmoja alise Kisha akatoka nje ya chumba na mmoja akabaki kunilinda akiwa na bunduki mkononi,
Ya muda mfupi mlango ulifunguliwa akaingia madam Janet akiwa na walinzi wake kadhaa
Madam aliwakonyeza wale walinzi wake wakatoka nje ingawa mmoja aligoma kabisa kutoka na badala yake alisogea tu pembeni kidogo pamoja na kumuonyeshea ishara ya mkono atoke nje Yule mlinzi aligoma kabisa na ndio kwanza alikua anajiweka sawa..
"Janet siamini Kama Ni wewe uko behind this"
Nilianza kusema huku nikimtolea macho Janet


"Shut up, Allan, hivi wema wote niliokufanyia wewe ndio wa kunifanya Mimi chizi? Hivi unajua thamani ya penzi langu wewe mjinga wewe! Nakuuliza wewe mjinga wewe!?"

Alisema huku akiachia kibao kimoja kikali Sana,

Nilitulia tuli maana Sasa ningefanya chochote kile ingemaanisha kufa mapema, Hata hivyo pamoja na kumjua Janet kwa miaka yote sijawahi kumuona akiwa amekasirika hivyo..


"Sorry nipe nafasi njieleze Basi"
Nilisema..

"Wewe Mimi sio mtoto mdogo, umeoa na mtoto juu na mke wako Sasa hivi mjamzito kipindi chote kile nakuweka moyoni na kukufanyia wema wote huo unanifanya mchepuko!, Mimi ndio wa kunifanya mchepuko wewe? Nakuuliza Tena mbwa wewe! Mimi Ni mchepukoo?"
Janet Sasa aliporomosha kila Aina ya matusi nilitulia tu


Sasa leo utajua kuwa Mimi Ni Janet ,


"Hivi unajua nguvu ya Raisi wewe mbwa wewe?"


"Nataka nikufanyie kitu ambacho hutaamini Allan "

Alisema Janet.

"Okay Kama umeamua kuniua Janet then kill me with your own hands"
Nilisema huku nikionyesha dalili za kukata tamaa kabisa...


"Nikikuua Nitakuwa nimekupendelea , nataka uteseke ujute kuzaliwa " alisema Janet


"Kulikuwa na haja gani ya kunidanganya yaani Mimi nimekupa mapenzi kwa Moyo wote napata tabu kukuandalia mazingira narisk mpaka kazi yangu nakuingiza mpaka ikulu kumbe huna lolote mbwa wewe!" Alisema Tena kwa ukali akiachia kibao kingine...
"Hebu mtoeni hapa ,
Alisema Janet na wakaingia watu wawili wakaniinua na kunipeleka chumba Cha pili kulikokuwa na minyororo wakanifunga ukutani.
Janet aliingia Kisha akanisogelea..

"Sijaona mwanaume mpumbavu Kama wewe , haya nakupa nafasi ya mwisho..

Kama utakubali kumuacha huyo mke wako kipenzi Mary Dafa, ama ufe huku una jiona"


Alisema janet,

"Sijakuelewa Janet , unamaanisha Nini, unataka kuniua Janet?"

Nilisema nikitetemeka
"Kwanini nikuache hai? Huna faida kwangu, una dakika tano za kufanya maamuzi, kubali kumuacha mkeo kiroho Safi hapa tunaongozana Hadi ikulu kwa Raha zetu, ama uishie huku huku porini"


Nakupa dakika tano za kufikiria....
 
MADAM PRESIDENT 07

"Siwezi kumuacha mke wangu na watoto kumbuka wewe ulikua unanilazimisha na hukunipa nafasi ya kujieleza Kama Nina mtu au vipi!"

Nilisema baada ya Janet kurudi...

"Kwahiyo ukaona unifanye Mimi mchepuko Raisi mzima?"

Aliuliza Tena,

"Hapana hujawahi kuniuliza Kama nimeoa"
Nilisema Tena,

"Sikiliza kwa kawaida huwezi kumfunua Raisi uchi wake halafu ukabaki hai nadhani unaelewa Hilo, wakati unakuja Dar niliambiwa umeoa, lakini nikakataa mpaka nikaletewa vithibitisho ndio nikaamini kumbe wewe mshenzi ulioa muda mrefu tu,


Nasikitika Sana kwamba hii Ni kwaheri ya kuonana"


Alisema Janet huku akitoka nje baadae nilisikia Gari ikiondoka..


Nilivuta pumzi ya kukata tamaa na kukaa pale kusubiri kifo.


******************

Sehemu ifuatayo anasimulia Shem Aida.

Nilijiuliza maswali mengi Sana kwani sikutegemea Allan angeweza kuwa mbali na familia yake kwa miezi miwili , "lazima Kuna Jambo"

Niliwaza Hata hivyo wakati tunaelekea mabatini nilijaribu kumuuliza Jose Kama anajua chochote,

Jose alijibu Ni Mambo ya kikazi tu...

"Sasa mbona tunakwenda usiku?"

Nilimuuliza Jose

"Kwakweli ingetakiwa nikupeleke mchana lakini nilikua bize Sana kuna mtu nilikua nambebea mizigo yake!"
Jose alisema lakini machoni Kuna kitu alikuwa anaficha kabisa kwa kumuangalia...

Tulifika mabatini na Mary alinipokea vizuri ,
Nilishangaa kuona Allan akiwa na nyumba kubwa na nzuri Sana mitaa Ile..

Hakika ilipendeza Sana

Tuliendelea kuishi
Siku moja usiku saa 1 tulikua tunataka kuagiza baadhi ya vitu tulimpigia Simu yake ikawa haipatikani,

Haikuwa kawaida kutopatikana mwishowe tuliamua kumpigia Jose ambaye aliahidi kumtamfuta,

Lakini Hadi kufika saa 6 usiku Simu yake haikupatikana na Jose alisema bado hakufanikiwa kumpata!


Nilimsihi Mary alale lakini aliendelea kulia tu

***********************

Sikujua maagizo gani Janet ametoa kwa walinzi wake,

Nilitamani Kama ningekuwa na uwezo nimpigie Jose Simu aharakishe kwenda kule nyumbani kwangu kuchukua boksi ambalo nimemuagiza na afanye kila kitu Kama nilivyomwambia..

"Ee Mungu msaidie Jose afanye Kama nilivyomwambia"
Niliwaza huku nikiomba walau muujiza utokee niweze kutoka hai...

Walikuja jamaa wawili wakiwa wamejiziba nyuso zao na kunifungua pale na kuniongoza kutoka nje ya Ile nyumba kwa haraka ilikua Ni usiku Sana, na walifanya kazi haraka haraka na kuongea kwa ishara.


Baadae tuliingia katika Gari dogo na kutoka nje ya Geti na kufuata barabara ambayo sikuelewa..


"Labda wanataka kwenda kuniua huko Porini"
Niliwaza..


"Jamani Mimi Ni mwanaume mwenzenu jamani, mke wangu Ni mjamzito jamani nitawapa pesa yoyote mtakayohitaji mniachie jamani nilisema "

"Oya huyo jamaa anatutia gundu mjue"

Alisema dereva huku akizidi kuendesha Gari..

Hakuna aliyejali na Sasa tulizidi kuingia porini na tukatotekea kwenye nyumba moja hivi ilichochakaa walishuka haraka wakanikokota kuelekea kwenye hiyo nyumba Kisha dereva akarudi haraka walinifungia kwenye chumba kimoja peke yangu bila shaka walisubiri agizo lingine kutoka kwa madam...


********************


Sehemu hii anasimulia Jose.
Nilikua nimetoka kupeleka mzigo wa fenicha za Mwalim mmoja wakati naegesha Gari ili nirudi nyumbani Simu yangu iliita, kwakuwa nilikua nimechoka sikupokea Hadi ilipokata ,

Baada ya muda mfupi Simu iliita Tena alikua Ni Aida..

Alisema Allan hapatikani na wanashida na baadhi ya mahitaji,

Basi nilimwambia anitajie vitu ambavyo walikua wanahitaji Kisha nitamtafuta Allan kwenye simu kesho nitawapelekea..
Kwa jinsi tulivyokuwa na heka heka hivi karibuni sikutegemea Allan angeweza kwenda sehemu ya mbali bila kunitaarifu, Ni kweli familia yake wanajua amesafiri kikazi lakini kiuhalisia mjuba tulikua nae hata jioni ya siku Ile...
Nilijaribu kupiga Simu yake haikupatikana, niliamua kwenda Hadi nyumbani kwake na sikuona dalili za yeye kuwepo, sikua na namna isipokuwa kwenda Hadi halmashauri anakofanyia kazi ambapo mlinzi alisema Allan alitoka saa kumi kasoro hivi,

Na hakurudi Tena..

"Nilipatwa na Mshtuko na wasi wasi na kutokana na kuwa mke wake alikua mjamzito sikuwa na namna zaidi ya kuwadanganyana"
Hivyo ilipofika saa tano niliwaambia kuwa Allan alienda mashewa sekondari na kwa eneo lile hakukua na mtandao na pia hata umeme hakuna kwahiyo labda hata chaji itakuwa imemuishia

Hili kidogo ilisaidia kuleta utulivu hata hivyo nilikua nawaza kesho yake endapo asingerejea....
 
MADAM PRESIDENT 08

Nikiwa pale chumbani nilianza kufikiria namna ya kujiokoa nilijaribu kuangalia Kama naweza hata kutokea dirishani lakini sikuona uwezekano huu nilizunguuka zunguuka mle chumbani na nikaanza Tena kumbuka Tena kukutana kwangu na Janet,


Niliamua kukaa chini na kutulia hatimaye asubuhi ikafika na niliweza kuchungulia nje na kuona msitu mnene sikuweza hata kuwa na wazo kuwa Niko msitu gani nilijaribu kutingisha mlango na kujikuta unafunguka!

Moyo ulipiga paaa! Niliufungua pole pole Kisha nikachungulia pole pole sikuona mtu nikanyata na kusogelea mlango wa kwenda nje ambapo nao ulikuwa haujafungwa..


Niliufungua pole pole na kuchungulia nje naam
Niliwaona wale jamaa wawili wakiwa wanafanya mazoezi huku bunduki zao zikiwa pembeni, nilifungua mlango pole pole Sana huku nikiomba Mungu wasinione nilitoka upande upande nikatembea kwenye ukuta kuzunguuka nyuma ya nyumba Kisha nikatambaa pole pole kuelekea vichakani nilipona naweza kusimama na kukimbia bila kusikika nilianza mbio kukimbia kuelekea nisikojua..

Sikua na saa Wala Simu hivyo nilijaribu kukadiria tu muda ule Kama saa 12 kasoro hivi, nilikimbia umbali mrefu kwa kukadiria ilikua zaidi ya masaa mawili, kwa mbali nilisikia Kama mngurumo wa Gari nikazidi kuongeza mbio na nikaona kijinjia nikakifuata na bila Kuamini macho yangu nikatokea kwenye barabara ya lami!

"Asante Mungu"

Nilisema nikipiga magoti kumshukuru Mungu,


Sikuelewa natakiwa kuelekea upande gani hata hivyo niliamua kuomba msaada kwa yeyote atakayejitokeza niliona gari kubwa la mizigo kwa mbali nikasimama kuomba lift na Mungu alikua upande wangu jamaa walikua wawili wakanifungulia mlango....


"Mzee baba sehemu hatari Sana hii kusimama, Bora ungesimamia pale mbele"

Alisema dereva...


"Samahani naomba maji ya kunywa Broo"

Nilisema nikitweta..


Walinipa maji nikanywa, akilini nikawa najaribu kutunga uwongo wa kuwaambia endapo wangeniuliza..

"Braza samahani Broo mji unaofuata hapa Ni wapi"

Niliuliza maana sikutaka kuwakera kwa kuwauliza wanaenda wapi...


"Ah hapo tunatokea mbezi Muda si mrefu!

Vipi kwani mgeni njia hii? Maana husomeki kwanza Ile mitaa ya mabwepande tuliyokukuta Ni mitaa hatari watu wanatekwa Sana na kuuwawa ujue umetokea wapi Kwani?


"Ah Kuna Mzee alipeleka shambani kwake huko nikaangalie shamba Sasa Mambo yamekwenda ndivyo nampigia Simu haipatikani na Mimi vitu vimeisha nikaona nirudi mjini kwanza"

Nilisema


Baada ya muda kidogo tuliingia mbezi kwa Yusufu, tulipofika kibanda Cha mkaa nikaomba waniache nikawashukuru Kisha nikashuka kuingia vichochoroni...


Niliingia vichochoroni nikikumbuka mitaa vizuri ya kuelekea matosa, nikipita matosa kwenda kwa masawe, nikatokea mtaa wa amani ...

Ndani ya dakika 40 nilikua nje ya geti moja jekundu nikagonga hodi.


***************

Jose anaendelea kusimulia..

Usiku mzima nilijaribu kupiga Simu ya Allan haikupatikana,

Mwishowe nilipitiwa na usingiz,

Nilizinduka usiku wa manane Kama saa 9 hivi nikaendelea kupiga Simu yake bado haikupatikana!


Baadae nilikata tamaa na kuamua kurudi chumbani kulala huku nikipanga mipango ya kesho..


Kulipopambazuka nilifika nyumbani kwake lakini hakukuwa na mtu nikasubiri mpaka saa moja na nusu nikaenda halmashauri kuuliza nikaambiwa hajatokea na wao wanamtafuta!


Sasa nilichanganyikiwa na nikajua tayari yupo mikononi mwa watu wabaya...


Sikuwa na namna nilinunua Yale mahitaji yote ambayo Shemeji Aida aliagiza Kisha nikawapelekea,

Wakati naingiza Gari kwenye geti wote walinikimbilia wakidhani labda nimekuja na Allan ...

Hata hivyo nilionyesha tabasamu na kuwaambia jamaa yupo salama sema TU Simu zake zimetumbukia mtoni wakati anakwenda kijijini hizi habari nimepewa na mratibu wa kata ya mgwashi ambapo ndio wameweka kambi ya wilaya...


Sikua na jinsi zaidi ya kuwadanganya..

Ningeanzaje kuwaambia Allan kapotea?


Sikutaka kukaa nao Sana kwani Moyo ukizidi kuniuma nikageuza kurudi mjini,.

Hata hivyo waliendelea kuwa na huzuni ingawa kidogo maneno yangu yaliwapa uhai...

***************************"

Alikuja kufungua Vailet


"Haaaa uncle Allan Karibu, ha uncle leo umekuja kwa miguu halafu unatoka jasho uncleee"


Vailet alisema huku akicheka,.

Nilikua nakuja Mara nyingi Dar kikazi huwa nalala pale kwa dada Yangu Mama Vai ,

Kwenye familia yetu tulibahatika kuwa na dada huyu pekee na katika ndugu zake wote ambao alikua akipendana nao Sana Basi Mimi nilikua mmoja wapo..


Baada ya kusikia Vailet akinitaja haraka Dada alitoka akiwa na James mtoto wake mdogo kwanza alicheka Sana kuniona katika Hali niliyokuwa nayo...lakini baada ya kuniona sicheki alinikimbilia na kunishika mkono na kuniingiza ndani...


"Naomba kwanza chakula sister"

Nilisema na haraka akanipashia viazi ambavyo walibakisha wakati wa chai asubuhi,


Nilikula kwa haraka Kisha nikaomba niende bafuni kuoga...

Kwa bahati Mara ya mwisho niliacha nguo zangu za mazoezi suruali mbili na tusheti mbili, hivyo baada ya kuoga nikavaa na kutoka sebuleni,


Dada alikua na hamu ya kutaka kujua kila kitu nilimkonyeza awatoe watoto

"haya nendeni huko chumbani kwenu mkajiandae muende kwa Bibi.."

Aliwaambia Akina Vai

Nilivuta pumzi kwanza nilimjua dada Yangu Tatu jinsi alivyo hivyo sikutaka kuharibu Mambo hivyo nilimdanganya tu
Uongo karibia na ukweli..


"Sister tumevamiwa na majambazi nilikua na wenzangu Jana usiku tulikua tunaleta vifaa vya michezo kwa bahati nikafanikiwa kutoroka nikapata lifti mpaka kibanda Cha mkaa , wamechukua Simu pesa na Gari la ofisini dada sijui wenzangu wako katika Hali gani"

Nilisema..dada aliangua kilio huku akifoka Kwanini nimetembea usiku..

"Dada naomba kiasi cha pesa hapo niende mjini nikajaribu kutafuta Simu na kufanya Mambo mengine nitakurudishia"

Nilisema huku nikirudi kule chumbani ambako nilitoka na kibegi kidogo hivi

Dada alinipa laki mbili,


Nikatoka nje Kisha nikachukua piki piki Hadi stendi ambapo nilipanda dala dala mpaka kariakoo....


Nilitafuta Simu ya Bei rahisi pamoja na line mbili

Kisha nikanunua kofia pamoja na wigi moja na nguo za kike na miwani.

Nilitafuta notebook ndogo na kalamu Kisha nikaingia kwenye huduma ya mtandao nikaingia kwenye barua Pepe yangu nilikua na sehemu nimehifadhi namba za Simu nyingi nikanakili namba kadhaa
Baada ya hapo nilipanda Gari Hadi posta nikashuka nikatembea kwa miguu kuelekea baharini,

Nilienda umbali mrefu pembezoni ambako hakukua na watu wengi Kish nikaweka namba ya Jose na kuipiga...

Ilikua majira ya kumi kasoro hivi Jose alipiga kelele za furaha baada ya kusikia Sauti yangu alinihadithia yote jinsi alivyowadanganya na Mambo mengine...

Sikuwa na muda mrefu wa kuongea nilimwambia kuwa Vita ndio imeanza na chochote kinaweza kutokea...

"Kaka sijui itakuwaje Jaribu kwenda kule halmashauri ujue halafu usiku nipigie" nilisema nikikata Simu..

"Asante Sana Jose"

Nilijisemea Kisha nikarudi mbezi kwa sister...

Mume wa Dada yangu Bwana Issa alikua mfanyabiashara wa spea za magari na alifuata mzigo nje ya nchi Mara nyingi hakuwepo nyumbani....

Nilipanga kukaa pale halafu kesho yake niondoke sikujua naenda wapi ingawa sikua tayari kurudi Mlandizi...


Ilikua imetimia saa 2:00 usiku na wakati wa taarifa ya habari

Nilipigwa na mshangao bado kidogo nizimie pale mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Pwani Bwana Mziray akiwa amezunguukwa na waandishi wa habari

"Mnayemuona pichani Ni alikua afisa michezo wetu wa Wilaya kwasasa tunamtafuta vikali baada ya kuiba hapa ofisini kiasi Cha shilingi million 50 pamoja na komputa mbili ambazo zilikua kwenye ofisi yake, sambamba na Hilo Ameitia ofisi ya mkurugenzi hasara ya milioni 20 baada ya kufoji sahihi za ofisi, popote pale alipo tunaomba ajisalimishe kituo Cha polisi"

Nilishindwa kuongea chochote dada alinitazama huku Akitaka kuongea Mara ghafla akaanguka chini akazimia..
"Ohooooo mkosi gani Tena huu"
Nilijisemea nikimuita Roda jikoni
 
yaani unafunua hadhina ya taifa alafu ubaki salama duh!
 
Back
Top Bottom