MADAM PRESIDENT 14
Niliduwaa tu nikimuangalia Jesca,
"You'll never know with women"
Niliwaza nikikumbuka kitabu Cha Hadithi Cha James H. Chase
"Jesca nimekusamehe kwasasa natafutwa Sana na Polisi naomba namna ya kuishi kwa siku kadhaa wakati naangalia utaratibu."
Nilisema
"Usiwaze Allan kwasasa uko Huru na nitakusaidia mpaka umalize Mambo yako, salama"
Alisema Jesca.
Niijaribu kuwasha Simu yangi lakini iliishaisha chaji,
Niliweka kwa muda kidogo Kisha nikaiwasha na kuangalia namba ya Jose,
Simu yangu haikuwa na salio hivyo nikaomba simu ya Jesca na kumpigia Jose
Nilivuta pumzi kwa nguvu wakati Simu ilipokuwa inaita..
Alipokea Jose akiwa katika sauti ya uchovu Sana,
Na bila shaka hakujishughulisha kusikiliza sauti ya mpigaji
Ilibidi kumstua kwa kutaja maneno ambayo tulikua tumekubaliana kuyatumia Mimi na yeye tu
"Baba namba moja hapa!"
Nilisema Jose alipiga kelele huko aliko...
"Mwana imekuwaje? Uko wapi nije?'
"Sikiliza mwana anaendeleaje Mary?"
Niliuliza
"Leo jioni nimeongea na Aida pengine wakatoka hospitali kesho....niambie uko wapi?"
"Sikiliza kesho tutaonana ,tutaongea mengi Sana"
Nilisema .
Nilipiga magoti kumshukuru Mungu Sana kisha nikamueleza Jesca Cha kufanya
Ilikua Ni saa 9 Jesca alimaliza Ile kazi saa 12 asubuhi Kisha nikakaa mbele ya kioo hakika nilitamani kucheka...
Mbele ya kioo alionekana dada mmoja hivi aliyepambwa Kama anaenda kusimamia harusi..
Nilimalizia na kuweka matiti ya bandia nikashushia na wigi la kike .
Jesca nae alijiandaa Kisha tukatoka huku nikiwa nimevaa Lile begi tukapanda gari Hadi feri Kisha kwenye pantoni kuelekea kigambon.
Hakuna mtu yoyote asubuhi Ile angeweza kudhani Ni mwanamke na mwanaume,...hakika ungeweza kudhani Ni wadada wawili wanaorudi kwenye mishe zao...
Tulishuka kwenye pantoni Kisha tukapanda dala dala na kuingia ndani zaidi tayari kulishaanza kupambazuka watu walikua wengi wakitoka kuelekea mjini Kama ilivyo harakati za watu wa Dar,
****************
Jose anasimulia..
Baada ya Isabella kutoka nilimfuata na akaonyesha hali ya furaha kuwa Allan amekubali kusaidiwa nilimpeleka mpaka kwake nikiwa na Gari ya dada Tatu,
Kisha nikamucha,
Tulikubaliana nimfuate Tena kesho asubuhi tupitie mahakamani kuchukua baadhi ya nakala Kisha twende mahabusu Tena kumcheki Allan,
Ilifika asubuhi sikuona Simu ya Isabella ikabidi niwashe Gari kwenda kwake,
Nilifika na kupiga honi lakini geti lilikua wazi tu,
Niliingiza gari ndani na kudhani labda atakuwa bafuni lakini kulikua kimya Sana,
Hakukua na dalili za mtu hata hivyo niliona dalili za vitu kuanguka anguka na baadhi ya makaratasi kusambaa,
Niliamua kutoka na kurudi nyumbani nikiwa njiani Tatu alinipigia kuwa Maiti ya Isabella imeokotwa ufukweni mwa bahari...
Tuliwahi kufika Ile sehemu na kukuta tayari polisi walishazunguusha utepe,
Baada ya taratibu zote familia ya Isabella walichukua mwili na tukaenda kuzika Gairo siku ya jumapili,..
Na siku hiyo hiyo tukarejea Dar kwa ajili ya kuwahi kesi siku ya jumatatu...
Ni usiku nikiwa nimelala Simu ikaita
Allan.
Niliipokea kwa uchovu Sana lakini nilipigwa na butwaa Sana kusikia Sauti ya Allan upande wa pili tuliongea kwa kifupi huku tukikubaliana kuonana kesho yake maeneo ya Kigamboni,
Sikuweza kulala niliwaza mengi huku nikifikiria namna Allan Alivyotoroka mikononi mwa wale Askari ambao hawakukubali hata ndugu na jamaa kumtembelea
**************
SAA mbili kasoro nilikua tayari maeneo ya Kigamboni nilichukua boda na kupelekwa kwa mchungaji msabaha,
"Kumbe Kigamboni Ni kubwa Sana"
Niliwaza tukipita mitaa mbali mbali na hatimaye kufuata kibao Cha Calvary Church Kama nusu kilometa hivi kutoka njia kuu nilimlipa Boda boda Kisha nikaelekea hapo kanisani ambapo pembeni yake kulikua na nyumba niliyofikiri moja kwa moja itakuwa nyumba ya mchungaji msabaha,
Nilifika na kugonga hodi na mama mmoja mtu mzima alinikaribisha,
Niliingia sebuleni na kukaa kwenye Kochi huku nikiuliza kuhusu Mchungaji Masabaha,
"Yupo kule ofisini na wageni bila shaka wewe Ni Jose"
Alisema Yule mama
"Ndio mama Naitwa Jose"
Alisema huku akinielekeza sehemu ya kupitia kuzunguuka kuelekea ofisini kwa mchungaji,
Nilifika na kweli nilimkuta Allan akiwa na msichana mwingine hivi bila shaka ni Yule niliyekuwa tukiwasiliana nae,
"Karibu Sana Jose naona wewe umekuja vizuri kabisa"
Mchungaji alisema akinipa mkono,
Sikuelewa chochote kuhusu kuja Vizuri..
"Wewe umekuja vizuri kabisa, wakati anakuja ndugu yako hapa kabisa nilidhani napokea wasichana wawili warembo kabisa, hata baada ya kuambiwa mmoja Ni mwanaume sikukubali "
Alisema Mchungaji
"Hahaha Pole Sana Mchungaji"
Nilisema huku nikiwa nimeshaelewa kuwa Allan alikuja akiwa amejibadilisha
Tuliongea machache Kisha Allan akaanza kuongea Sasa
"Jose na Jesca, huyu Ni Mchungaji Msabaha, Ni baba yangu mlezi alinilea Sana nikiwa kidato Cha tano na 6, wakati nikiwa mombo, hata badae alipohamia huku kwa huduma tulikua tunawasiliana na huyu ndie alifungisha Ile ndoa yangu Kama mnakumbuka,
Kwasasa nimeona Sina jinsi isipokuwa kuja kujificha hapa kwa muda naamini Mchungaji hawezi kumuuza mtoto wake kwa polisi"
Alisema kwa huzuni kidogo"
"Allan amenisimulia kila kitu na kwakweli Mungu wetu anakataa udhalimu, na uonevu, Jambo hili litafikia mwisho mzuri, ingawa Allan hujasema mnataka kufanya Nini Sasa?"
Mchungaji aliuliza.
"Hapa nitabaki mwenyewe tu Mchungaji Jose atarudi kwenda kuangalia familia yangu halafu Jesca atakua huko mjini Kuna Mambo atakuwa anafuatilia ninachoomba tu baba nikae hapa kwa muda mfupi tu"
Alisema Allan.
Tuliongea machache huku Allan akisimulia jinsi alivyotoroka wale maaskari na Sasa tulitoka nje pembeni kupanga mikakati ya kazi