Hadithi: Madam President

Hadithi: Madam President

Haya ndiyo mambo Sasa.. Yani bampa 2 bampa..😍
 
Wakuu huu mzigo wote upo yaani ni Mimi kupaste tu,
Sema kidgo nilikua nazunguliwa na suala la bando!
Wakuu tembezen bakuli sio kukalia vya bure tuu na mpostiji anakwama bando
 
MADAM PRESIDENT 13

Haraka walinipakiza kwenye Gari yao ya polisi huku nikiwa na polisi mmoja upande wa nyuma na Dereva huko mbele,

Tayari Simu ilishapigwa na Askari wengine wangeweza kufika hospitali muda sio mrefu,

Niliangaza macho pale ndani na kuona Chuma kidogo Kama bomba Fupi,

Yule Askari alikua anachezea Simu yake kwa Kasi ya ajabu nilichukua Lile bomba na kumpiga nalo kichwani alienda chini moja kwa moja Kisha nikampiga pigo lingine tumboni akatulia..

Kutokana zile kelele dereva alipunguza Mwendo huku akiuliza Kama Kuna tatizo..

Tulishakaribia kwenye mataa kwahiyo alipunguza Mwendo kabisa, Mimi nikaruka na kujichanganya kwenye magari nikatokomoea!


Kwakuwa nilikua nimefanya mazoezi muda mfupi uliopita nilijisikia mwili kuchangamka na hatimaye nikaingia vichochoro na kutokea buguruni,

Nilitembea tembea huku nikitamani kupata Simu ya mkononi nimtafute Jose kwa haraka ilikua majira ya saa 8 kasoro usiku,

Niliendelea kutembea nikitafuta mahali pa kujificha kwa mbali nilimuona msichana mmoja akiwa ameshuka kwenye Gari,

Bila shaka alikuwa Ni kahaba akitoka kwenye biashara yake anaelekea nyumbani au anarudi kazini,

Niliwaza nikimkaribia Moyo wangu ulipiga paaa


"Jesca!?"

Ni kweli alikua Ni yeye


"Allan!"

Alisema huku akinikumbatia kwa nguvu

"Jesca, nimetoroka Polisi !"

Nilimwambia kana kwamba namueleza matokeo ya alichokifanya

"Tangu siku Ile sikuwa na amani Allan, nilikua nakufikiria vibaya kumbe maskini hata hujaiba zile pesa, lakini nilijutia kitendo changu na nimetoa msaada kwako kwa jinsi nilivyoweza!"


Alisema huku akijifuta machozi


"Allan Mimi ndio nilikua nakuletea chakula"


Alisema huku akiangalia pembeni

"Nilijiwekea utaratibu kila siku nikuletee chakula Mara Tatu hata Kama Mimi nisile"
Alisema


"Kwanini ufanye Hivyo?"

Nilimuuliza nilishangaa

"Nakumbuka ulivyoniamini kipindi kile lakini Mimi nikashindwa kuamini"


Alisema

"Jesca natafutwa nielekeze pa kutokoea"


Nilisema

"Twende kwanza Kuna kitu ukaone"

Alisema akinivuta tukaingia vichochoroni tulitembea umbali mrefu Sana Kisha tukatokea kwenye nyumba moja hivi tukazunguuka nyuma Jesca akatoa ufunguo wa akafungua tuakingia chumbani,

Kisha akafunga mlango kwa ndani akaingia chini ya uvungu na kutoka

Mfuko mmoja hivi wengi walioenda kuita shangazi kaja

Kisha ndani yake akatoa begi langu!

Macho yalinitoka....
"Jesca Hili begi si walichukua polisi?"
Niliuliza kwa mshangao,

"Siku Ile kumbuka tulivyotoka manzese nilikusaidia begi na wewe ukabeba langu, kwanza ulisema begi lako limejaa mawigi tu"

Ndio nikaona Mimi mwanamke nibebe begi lako,

Lakini kiuhalisia nilikua Nimepanga kuiba begi lako kwasababu nilikua najua unaenda kukamatwa hivyo nilijua litakua na pesa ndani" kwahyo polisi walikuchukua ukiwa na begi langu na sio la kwako"

Jesca alisema

Nilijaribu kufungua na kukuta kila kitu kipo Hadi pesa

"Sasa mbona kila kitu kipo?"

Niliuliza

"Baada tu ya kuondoka na polisi ndio Sasa Kuna dada mmoja alikua anaongea kila kitu kuhusu wewe haukua jambazi Bali Ni Mambo tu ya kimapenzi ndio ukapata kesi kwahyo Roho ikawa inaniuma Sana "
 
MADAM PRESIDENT 14
Niliduwaa tu nikimuangalia Jesca,

"You'll never know with women"
Niliwaza nikikumbuka kitabu Cha Hadithi Cha James H. Chase

"Jesca nimekusamehe kwasasa natafutwa Sana na Polisi naomba namna ya kuishi kwa siku kadhaa wakati naangalia utaratibu."

Nilisema

"Usiwaze Allan kwasasa uko Huru na nitakusaidia mpaka umalize Mambo yako, salama"

Alisema Jesca.

Niijaribu kuwasha Simu yangi lakini iliishaisha chaji,

Niliweka kwa muda kidogo Kisha nikaiwasha na kuangalia namba ya Jose,

Simu yangu haikuwa na salio hivyo nikaomba simu ya Jesca na kumpigia Jose


Nilivuta pumzi kwa nguvu wakati Simu ilipokuwa inaita..


Alipokea Jose akiwa katika sauti ya uchovu Sana,


Na bila shaka hakujishughulisha kusikiliza sauti ya mpigaji


Ilibidi kumstua kwa kutaja maneno ambayo tulikua tumekubaliana kuyatumia Mimi na yeye tu

"Baba namba moja hapa!"

Nilisema Jose alipiga kelele huko aliko...

"Mwana imekuwaje? Uko wapi nije?'


"Sikiliza mwana anaendeleaje Mary?"
Niliuliza

"Leo jioni nimeongea na Aida pengine wakatoka hospitali kesho....niambie uko wapi?"


"Sikiliza kesho tutaonana ,tutaongea mengi Sana"

Nilisema .

Nilipiga magoti kumshukuru Mungu Sana kisha nikamueleza Jesca Cha kufanya

Ilikua Ni saa 9 Jesca alimaliza Ile kazi saa 12 asubuhi Kisha nikakaa mbele ya kioo hakika nilitamani kucheka...

Mbele ya kioo alionekana dada mmoja hivi aliyepambwa Kama anaenda kusimamia harusi..

Nilimalizia na kuweka matiti ya bandia nikashushia na wigi la kike .

Jesca nae alijiandaa Kisha tukatoka huku nikiwa nimevaa Lile begi tukapanda gari Hadi feri Kisha kwenye pantoni kuelekea kigambon.


Hakuna mtu yoyote asubuhi Ile angeweza kudhani Ni mwanamke na mwanaume,...hakika ungeweza kudhani Ni wadada wawili wanaorudi kwenye mishe zao...


Tulishuka kwenye pantoni Kisha tukapanda dala dala na kuingia ndani zaidi tayari kulishaanza kupambazuka watu walikua wengi wakitoka kuelekea mjini Kama ilivyo harakati za watu wa Dar,


****************


Jose anasimulia..


Baada ya Isabella kutoka nilimfuata na akaonyesha hali ya furaha kuwa Allan amekubali kusaidiwa nilimpeleka mpaka kwake nikiwa na Gari ya dada Tatu,


Kisha nikamucha,

Tulikubaliana nimfuate Tena kesho asubuhi tupitie mahakamani kuchukua baadhi ya nakala Kisha twende mahabusu Tena kumcheki Allan,

Ilifika asubuhi sikuona Simu ya Isabella ikabidi niwashe Gari kwenda kwake,

Nilifika na kupiga honi lakini geti lilikua wazi tu,

Niliingiza gari ndani na kudhani labda atakuwa bafuni lakini kulikua kimya Sana,


Hakukua na dalili za mtu hata hivyo niliona dalili za vitu kuanguka anguka na baadhi ya makaratasi kusambaa,
Niliamua kutoka na kurudi nyumbani nikiwa njiani Tatu alinipigia kuwa Maiti ya Isabella imeokotwa ufukweni mwa bahari...


Tuliwahi kufika Ile sehemu na kukuta tayari polisi walishazunguusha utepe,

Baada ya taratibu zote familia ya Isabella walichukua mwili na tukaenda kuzika Gairo siku ya jumapili,..

Na siku hiyo hiyo tukarejea Dar kwa ajili ya kuwahi kesi siku ya jumatatu...

Ni usiku nikiwa nimelala Simu ikaita

Allan.

Niliipokea kwa uchovu Sana lakini nilipigwa na butwaa Sana kusikia Sauti ya Allan upande wa pili tuliongea kwa kifupi huku tukikubaliana kuonana kesho yake maeneo ya Kigamboni,

Sikuweza kulala niliwaza mengi huku nikifikiria namna Allan Alivyotoroka mikononi mwa wale Askari ambao hawakukubali hata ndugu na jamaa kumtembelea


**************

SAA mbili kasoro nilikua tayari maeneo ya Kigamboni nilichukua boda na kupelekwa kwa mchungaji msabaha,

"Kumbe Kigamboni Ni kubwa Sana"

Niliwaza tukipita mitaa mbali mbali na hatimaye kufuata kibao Cha Calvary Church Kama nusu kilometa hivi kutoka njia kuu nilimlipa Boda boda Kisha nikaelekea hapo kanisani ambapo pembeni yake kulikua na nyumba niliyofikiri moja kwa moja itakuwa nyumba ya mchungaji msabaha,



Nilifika na kugonga hodi na mama mmoja mtu mzima alinikaribisha,


Niliingia sebuleni na kukaa kwenye Kochi huku nikiuliza kuhusu Mchungaji Masabaha,

"Yupo kule ofisini na wageni bila shaka wewe Ni Jose"


Alisema Yule mama
"Ndio mama Naitwa Jose"

Alisema huku akinielekeza sehemu ya kupitia kuzunguuka kuelekea ofisini kwa mchungaji,

Nilifika na kweli nilimkuta Allan akiwa na msichana mwingine hivi bila shaka ni Yule niliyekuwa tukiwasiliana nae,


"Karibu Sana Jose naona wewe umekuja vizuri kabisa"
Mchungaji alisema akinipa mkono,

Sikuelewa chochote kuhusu kuja Vizuri..


"Wewe umekuja vizuri kabisa, wakati anakuja ndugu yako hapa kabisa nilidhani napokea wasichana wawili warembo kabisa, hata baada ya kuambiwa mmoja Ni mwanaume sikukubali "

Alisema Mchungaji


"Hahaha Pole Sana Mchungaji"

Nilisema huku nikiwa nimeshaelewa kuwa Allan alikuja akiwa amejibadilisha

Tuliongea machache Kisha Allan akaanza kuongea Sasa

"Jose na Jesca, huyu Ni Mchungaji Msabaha, Ni baba yangu mlezi alinilea Sana nikiwa kidato Cha tano na 6, wakati nikiwa mombo, hata badae alipohamia huku kwa huduma tulikua tunawasiliana na huyu ndie alifungisha Ile ndoa yangu Kama mnakumbuka,


Kwasasa nimeona Sina jinsi isipokuwa kuja kujificha hapa kwa muda naamini Mchungaji hawezi kumuuza mtoto wake kwa polisi"

Alisema kwa huzuni kidogo"


"Allan amenisimulia kila kitu na kwakweli Mungu wetu anakataa udhalimu, na uonevu, Jambo hili litafikia mwisho mzuri, ingawa Allan hujasema mnataka kufanya Nini Sasa?"

Mchungaji aliuliza.


"Hapa nitabaki mwenyewe tu Mchungaji Jose atarudi kwenda kuangalia familia yangu halafu Jesca atakua huko mjini Kuna Mambo atakuwa anafuatilia ninachoomba tu baba nikae hapa kwa muda mfupi tu"

Alisema Allan.


Tuliongea machache huku Allan akisimulia jinsi alivyotoroka wale maaskari na Sasa tulitoka nje pembeni kupanga mikakati ya kazi
 
Back
Top Bottom