Hadithi: Mzaha wa damu

Hadithi: Mzaha wa damu

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Wakuu! Nimerudi mapema kuliko nilivyotarajia.

Hii ni kutokana na sababu kadhaa
Mosi, nilifanikiwa kupata device nyingine japo sio yenye vile viwango nilivyotaka lakini inaweza!
Pili , watu wengi wameonyesha upendo wa Hali ya juu kwangu! Kwa hivyo, nimekuwa nikipokeaa simu na jumbe nyingi na wengine walidiriki hata kunitumia bando Ili tu kwamba tuendelee hivyo hivyo!
tatu, Kifo Cha mpendwa wetu leadermoe ,
Kilinigusa sana na kuona kwamba kama tunapata nafasi ya kutoa tulicho nacho basi tutoe.. (wema ni akiba) na kwa hivyo nikaona tumalize huu Mzaha wa Damu na Mimi nisiwe na deni humu!


MZAHA WA DAMU...... By CK Allan 0746 266 267 Utangulizi

Ulishawahi kula Tunda kimasihara? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Hapana hebu nianze vizuri tena!!

Ulishawahi kuona Mzaha ukitumbua usaha wa Damu?
Basi hii ni maalum kwenu wote mnaopenda sana utani!

Ule utani flani hivi wa kuitana 'mke, baby, honey n.k Ili Hali hakuna chochote kinachoendelea!

ANGALIZO!
Hadithi hii ni ya kubuni tu kwa ajili ya kufurahisha baadhi ya maeneo ni ya kubuni, lakini majina YOTE ya watu yaliyotumika ni majina ya watu halisi ambao ni marafiki zangu na kwa ridhaa Yao majina Yao yametumika kama yalivyo!

Basi karibuni sana tuanze!
 
MZAHA WA DAMU 01
by CK Allan 0746 266 267

“Baba njoo uone amefumbua macho yake! Ameamka! Baba Njoo!” ilikua ni sauti ya mtoto mdogo wa kike ambaye alikuwa akikimbia kutoka nje
Nilijaribu kukaa lakini sikuweza kabisa, mwili wangu ulikua unauma kila sehemu, kila kiungo nilihisi maumivu makubwa sana, nilijaribu kufungua mdomo lakini sikuweza, na sasa nilijaribu kunyanyua mkono, nilijikuta nikiishiwa nguvu!, mikono yangu yote ilikuwa imefungwa vitu vizito na sikuweza hata kujigeuza,

Wakati nikiendelea kujigeuza ghafla niliona mwanaume mmoja akiingia kwa haraka

“ohh Asante Mungu,nilisema mimi hakufa huyu! Nilisema mimi ataamka!” alisema yule mzee kwa haraka akimkumbatia Yule mtoto wake,
“Zawadi, kimbia haraka kamuite mama mwambie unko amezinduka!” alisema sasa Yule mzee huku Yule binti akitoka mbio, niliendelea kuduwaa sana!
Yule mzee alinisogelea huku akitabasamu na kisha akaniinua na kunigeuza upande wa pili ambapo sasa nilijisikia afadhali kidogo na ndipo nikashuhudia majeraha kadhaa mwilini mwangu, kwa ufupi ni kama mtu aligongwa na gari, ama kupondwa pondwa na mawe
Nilijikuta naishiwa nguvu na kufumba macho yangu kujaribu kukumbuka chochote
Nilijikuta sikumbuki chochote na kadri nilivyojilazimisha kufikiri ndivyo maumivu yalizidi

“ah usijali utapona kabisa kijana wangu, utapona kabisa, utapona kabisa!” alisema Yule mzee huku akifungua chupa moja iliyokuwa mkononi mwake na kuweka kwenye kijiko huku akinilisha mdomoni,
Ndipo sasa nikahisi maajabu mengine mwilini mwangu, ndioo
Ladha!, sikusikia ladha yoyote mdomoni mwangu na hivyo sikuweza kujua ni aina gani ya kitu nalishwa!
“loh!” nimekuwaje?
“imekuwaje?’ nilijiuliza maswali mengi bila majibu
Ni wakati huo huo sasa Yule mzee alitoka nje ya kile chumba na kisha baada ya muda aliingia akiwa na mwanamke pamoja na yule mtoto, nilijaribu kukadiria umri wao ulikuwa kama miaka 55 au 60 hivi,
“oooh jamani, Mungu ni mwema! Ooh jamani, kijana wa watu jamani, jamani, jamani!” Yule mama sasa aliongea akinishika nywele zangu kichwani huku machozi yakimtoka
“ah kwa.. kwa… kwa… ni… ah” nilijaribu kuongea lakini mdomo hakuweza kabisa kunyanyuka
Ni kama taya zangu hazikuwa sawa, ni kama taya ya juu ilirudi chini na ya juu ikarudi chini..
“ooh umesemaje! Umeongea!” Yule mzee alishikwa na mshangao mpaka akaangusha chupa yake huku mke wake nae akisimama kwa mshangao!

“ameongea!, ameongea!” walijikuta wakisema kwa pamoja huku wakikumbatiana kwa furaha!
Sasa nilielewa kumbe kuna tatizo kubwa zaidi ya hata hili nililokuwa nafikiria,
Kwa maana hiyo hata kuongea kwangu kumewashangaza sana kama sio kuwafurahisha!

“sasa pumzika kijana! Utapona tu!” alisema Yule mama huku akitoka
“mimi nabaki na anko, mama!” alisema Yule mtoto huku akisogeza kiti na kukaa pale kitandani
“mama yangu alisema umekufa! Lakini baba akasema hujafa, utaamka, baba yangu ndie aliyekuleta ….’
“zawadiii muache anko alale kwanza utamuongelesha baadae!” aliita Yule mama na yule mtoto akaondoka zake

Baada ya wiki moja sasa maumivu yalipungua kwa baadhi ya sehemu za mwili na niliweza hata kujigeuza kitandani pasi na kuwa na msaada, ingawa bado mdomo ulikua hauwezi kunyanyuka na sikuweza kutamka maneno yaliyonyooka,
“tutaangalia namna ya kukufungua huu mkono mmoja kwanza wa kulia maana ni kama umeanza kupona hivi” alisema Yule mzee akinyanyua mkono wangu na kweli maumivu yalikua yamepungua kabisa.
Kesho yake Yule mzee alinifungua vile vipande vya miti ambavyo vilikuwa vimewekwa kwe mkono wangu kwa uangalifu mkubwa kisha akatoa kama mafuta Fulani hivi akaweka kwenye mikono yake na kisha akaanza kuuvuta kunyoosha pole pole,
Nilisikia maumivu makali sana , na kuhisi kama mkono unataka kunyofolewa, lakini Yule mzee aliendelea tu huku nikizidi kupiga kelele Yule mama alishindwa kujizuia alitoka nje, Yule mzee aliendelea tu kana kwamba alikua kiziwi, alipaka yale mafuta na kuendelea kuunyoosha na kadri alivyokuwa akiendelea sasa maumivu yalipungua, na hatimaye yakakaacha kabisa
“loh, huyu mzee mchawi nini!”
niliwaza sasa nikimkodolea macho
Aliniachia ule mkono kisha akanitaka kujaribu kukunja vidole
Vidole vvyote vilikua vinajikunja isipokuwa kidole cha mwisho kidogo
Ambacho kiligoma kabisa
“sasa fanya mazoezi, kumbuka unapona haraka, lakini utapona haraka zaidi kama utaendelea kufanya mazoezi” alisema Yule mzee akifunga zile chupa zake akatoka nje.

Hata mimi nilitaka kupona haraka ili nijue hasa kitu gani kilinitokea, kwa uhalisia sikukumbuka chochote, hata jina langu pia! Hakika sikuelewa kitu gani kinatokea katika maisha yangu, je nilipata ajali? Nilivamiwa na majambazi? Au nilikuwa mwanajeshi nimetoka vitani? Nilishambuliwa kwa bomu? Je hapa nipo wapi? Hawa wanaonihudumia ni akina nani?


Nilijiuliza maswali mengi sana yasiyokuwa na majibu nikajikuta machozi yakinitiririka tu, kila nilivyokuwa nawaza ndivyo ambavyo machozi yalikuwa yanatoka hata hivyo jambo moja ambalo nilikua na uhakika nalo ni kuwa hawa watu walikuwa wamejitolea kunisaidia kwa hali zao na mali zao pengine na kila kitu walichokuwa nacho, je nimekuwapo hapo kwa muda gani? Wiki, miezi, miaka? Nilitamani sana kujua
Nilikumbuka mzee alinihakikishia kuwa ningepona kabisa na kurudi katika hali yangunya kawaida sasa nilisubiri kwa hamu siku hiyo, siku ambayo ningesimama kwa miguu yangu siku ambayo nitaongea kwa kinywa changu, siku ambayo nitaongea kila kitu, siku ambayo nitasimulia kila kitu kilichonikuta na kila kitu kuwa hadharani.."

“ooh usiwaze sana kijana wangu, nakuhakikishia umeshapona, kesho tunafungua mkono mwingine na mguu mmoja” alinikatisha Yule mzee katika mawazo yangu
Nilitingisha kichwa tu kukubaliana nae huku moyoni mwangu nikitoa shukrani za dhati kwa mzee huyu.

Kesho yake asubuhi na mapema mzee alinifungua mkono wa kushoto pamoja na mguu wa kulia, na sasa mikono yangu ilikuwa huru na niliweza kuikutanisha tena pamoja kwa mara kwanza , pamoja na maumivu makali niliyosikia lakini niliona ni bora kuwa katika hali ile kuliko kurudishiwa ile mizigo ya miti, na hivyo nilijikaza kweli kweli, wakati mwingine nilijifanya kutabasamu wakati mzee alipokuwa akinihudumia lakini ningeugulia maumivu makali wakati mzee akiwa ametoka, hata hivyo ilikua afadhali nilikua naweza kuona mguu wangu, pamoja na mikono yangu ikiwa huru, nakumbuka siku ile nililala nikiwa na furaha sana, usiku ule niliota ndoto za ajabu ajabu na mara kadhaa nilistuka na kuamka, sikukumbuka kama niliwahi kuota ndoto kadhaa kwa muda wote nikiwa pale kitandani kama siku Ile!
hata hivyo maumivu yalikua yakipungua kabisa na kesho yake asubuhi niliweza kujigeuza na kukaa kitandani mwenyewe huku nikifanya mazoezi ya kukutanisha mikono na kuinyoosha, bado mdomo haukuweza kutoa maneno ya kueleweka ingawa nilijitahidi kabisa kuhakikisha yanatoka

Baada ya mwezi mmoja hivi ....
niliweza kusimama na kuchechemea na kutoka nje kutazama jua na kurudi ndani, sio hivyo tu bali niliweza kushika kikombe cha uji na kunywa mwenyewe, sasa ningeweza kutoka kwa kuchechemea kuzunguuka nyumba kisha ningerudi ndani bila kuwa na msaada wowote, na nilikuwa naelewa mazingira yale niliyokuwepo yalikua maeneo ya porini kabisa na sikuweza kuona nyumba yoyote zaidi ya shamba kubwa ambalo limezunguuka ile nyumba, pamoja na hayo kulikua na uzio wa seng’eng’e ambao ulizunguushiwa nyumba yote, pamoja na kuwa nyumba hii ilikua porini lakini ilikua imejengwa kisasa kwa mbao imara na kwa namna ya ujenzi wa Kijerumani hivi, na kisha kulikua na umeme wa jua ambao ulileta mwangaza katika nyumba hii, mzee huyu pia alikua na piki piki yake aina ya watco ambayo alitumia mara kadhaa kwenda kuchukua mahitaji mbali mbali...

Siku hiyo alikuja Yule mzee akiwa na furaha sana alikuja na kiboksi kidogo hivi na kukifungua kilikuwa na vidude vya plastiki hivi na kisha akanitaka niweke mdomoni na kingine nikafunga kwa juu kwenye kidevu,
Aliniambia natakiwa kuvaa kila siku labda nivitoe tu wakati wa kula tu!
, ni kweli vifaa vile vilikua vinavuta taya zangu na kuweka mdomo katika hali ya kawaida na nikaanza kutoa maneno mawili , matatu, sentensi na hatimaye ndani ya mwezi mmoja mwingine nikaweza kabisa kuongea ingawa kwa pole pole hatua kwa hatua lakini niliweza kufanya mazungumzo kabisa na kueleweka, hakika Mungu ni mwema sana na hatimaye nilikua naelekea kupona kabisa na sasa niliweza kutambua jina la wenyeji wangu hawa yaani mzee Tito na mkewe Imelda, hakika walikuwa ni watu wema sana hawa watu,
Hata kama walikuwa wameshiriki kwa namna yoyote kunifanya hivi nilivyo bado ningeweza kuwasamehe kabisa makosa yao kwa jinsi walivyonihudumia kwa namna ya pekee na kunijali kabisa bila shaka kuna mengi zaidi nataka kujua kuhusu watu hawa, hata hivyo kwasasa nilikuwa na jambo moja tu,
Mimi ni nani na nimetokea wapi? Na kwanini niko hivi nilivyo leo? Wakati mwingine nilikuwa naogopa hata kumuuliza mzee Tito kuhusu asili yangu
“isije kuwa Mzee Tito na mama Imelda ndio wazazi wangu mimi! , halafu nikawauliza kuhusu hili jambo nikazidi kuwatia simanzi” yalikuwa ni mawazo katika hisia zangu,
Hata hivyo sikuwa na namna nyingine zaidi waswahili walisema njia rahisi ya kujua jambo ni kuuliza, na mimi sikuwa na njia nyingine isipokuwa kuuliza, kwahiyo nilisubiri mpaka kuhakikisha mwili wangu umeimarika kabisa ili niweze kuanzisha safari nyingine ya kujitambua!
 
Wakuu! Nimerudi mapema kuliko nilivyotarajia..
Hii ni kutokana na sababu kadhaa
Mosi, nilifanikiwa kupata device nyingine japo sio yenye vile viwango nilivyotaka lakini inaweza!
Pili , watu wengi wameonyesha upendo wa Hali ya juu kwangu! Kwa hivyo, nimekuwa nikipokeaa simu na jumbe nyingi na wengine walidiriki hata kunitumia bando Ili tu kwamba tuendelee hivyo hivyo!
tatu, Kifo Cha mpendwa wetu leadermoe ,
Kilinigusa sana na kuona kwamba kama tunapata nafasi ya kutoa tulicho nacho basi tutoe.. (wema ni akiba) na kwa hivyo nikaona tumalize huu Mzaha wa Damu na Mimi nisiwe na deni humu!


MZAHA WA DAMU...... By CK Allan 0746 266 267 Utangulizi

Ulishawahi kula Tunda kimasihara? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hapana hebu nianze vizuri tena!!

Ulishawahi kuona Mzaha ukitumbua usaha wa Damu?
Basi hii ni maalum kwenu wote mnaopenda sana utani!

Ule utani flani hivi wa kuitana 'mke, baby, honey n.k Ili Hali hakuna chochote kinachoendelea!

ANGALIZO!
Hadithi hii ni ya kubuni tu kwa ajili ya kufurahisha baadhi ya maeneo ni ya kubuni, lakini majina YOTE ya watu yaliyotumika ni majina ya watu halisi ambao ni marafiki zangu na kwa ridhaa Yao majina Yao yametumika kama yalivyo!

Basi karibuni sana tuanze!
Shukrani niko hapa.
 
MZAHA WA DAMU 02

By CK Allan

Nilikuwa nimeshatimiza zaidi ya miezi miwili na nilikua natembea bila fimbo ya kuegemea na wakati mwingine ningeweza hata kufanya kazi ndogo ndogo vidonda vikubwa vilishapona na hata vile vidude vya kuweka mdomoni nilikuwa siweki tena, niliweza kunyoosha mikono yote na miguu isipokuwa sikuweza kuinama walau kugusa miguu, mgongo ulikataa kabisa,
Na hata wakati najitazama kwenye kioo niliweza kuona makovu makubwa usoni,
“nilipatwa na nini!”
nilikua nikijisemea kila wakati nilipokuwa najitazama kwenye kioo
Siku hiyo baada ya chakula cha usiku sasa nilivunja ukimya na kuomba mzee Tito anisimulie kila kitu kuhusu mambo yote yaliyonitokea nakumbuka mzee Tito alistuka hivi na kisha akamtazama mkewe ambaye alitingisha kichwa tu kuashiria kuwa mzee Tito aendelee kunisimulia kila kitu, na bila kusita mzee Tito akaanza,
Kunielelezea kama ifuatavyo
OCKOBA 15, 2019
Siku hiyo nilitoka hapa nyumbani kuelekea sokoni kuchuka mahitaji ya hapa ndani, wakati huo nilipanga pia kupitia dukani kuuliza baadhi ya dawa kwa ajili ya mazao yangu hapa shambani, kwa kawaida huwa natoka alfajiri sana na huwa naendesha piki piki kwa masaa zaidi ya matatu mpaka kufika barabara kuu ya lami ambapo ni mji mkubwa tu wa Manyoro, nikifika Manyoro kuna rafiki yangu mmoja ambae naacha piki piki yangu pale kwake kisha nasubiri basi ambalo linatoka Gairo kwenda Morogoro ambapo nafanya manunuzi na mahitaji yangu mengine kisha nalala asubuhi yake nageuza nalo mpaka Manyoro nachukua piki piki yangu narudi nyumbani, na kama nitakuwa na mizigo mingi basi naiacha kwa Yule rafiki yangu kisha nabeba kidogo kidogo kwa piki piki kama ujuavyo hapa hakuna usafiri wowote zaidi ya piki piki yangu,

Sasa kwanini tunaishi huku porini na kwanini tupo wenyewe na mambo mengine kuhusu sisi haya tutazungumza baadae!
Kwasasa nikueleze namna tulivyokutana!

Basi siku hiyo ya tarehe 15 mtoto wetu zawadi alikua hajisikii vizuri sana kama ujuavyo watoto wanakuwa na magonjwa mbali mbali, nilienda mjini kutafuta mahitaji na ilinibidi kufanya niwezavyo nirejee siku ile ile, niliwahi kufika Manyoro na kupata usafiri na majira ya saa 9 mchana nikawa nisharejea Manyoro tayari kabisa kurudi huku porini kwetu
Bahati mbaya siku hiyo sikumweleza mwenyeji wangu kuwa nitarudi siku ile ile hivyo akatumia usafiri wangu kwenda kijiji cha jirani na akakawia kurudi, bahati mbaya tena wakati anarejea tu kukawa na pancha ndogo kwenye tairi ya nyuma,
Mwenyeji wangu alinisihi sana kulala siku ile maana mpaka tunamaliza kutengeneza piki piki ilikua ni saa moja kasoro usiku, hata hivyo ilibidi kumueleza hali halisi ya mgonjwa wangu niliyemuacha nyumbani na hivyo baada ya kumshinikiza sana na kumsihi akaomba nipunguze mizigo na niondoke na kijana wake wa kiume ili anisindikize na kesho asubuhi nimrudishe na nirejee na mizigo mingine,
Nisingeweza kukataa, ukilinganisha kutembea katika msitu mnene na chombo cha moto usiku ukiwa mzee kama mimi halafu tena usiku, isingekuwa busara, hivyo nikakubali kuondoka na Yule kijana na nikamuachia jukumu la kuendesha piki piki na tukaianza safari yetu saa moja huku giza likiwa limeingia, na kwakuwa tulikua na mizigo hatukwenda kasi sana, tulikua tunafuata barabara ya vumbi ambayo haikutumika sana na iliishia kwenye shamba la mkonge na mara nyingi magari yaliyopita huko ni yale ya kampuni tu kubeba mkonge, baada ya hapo tunaingia kwenye njia ya kawaida ambayo ni hii inayokuja hapa nyumbani, hata hivyo wakati tunakaribia kumaliza lile shamba la mkonge tulipishana na gari ambalo lilikua na mwendo mkali, nakumbuka ilibidi kusogea pembeni ili kulipisha, na kisha tukaendelea na safari tararibu huku tukipiga hadithi za hapa na pale, ni wakati tumepita kabisa lile shamba mara ghafla mbele yetu tukaona gunia lililoonyesha kufungwa vizuri sana!
kwa kuwa barabara ilikua nyembamba sana hatukuwa na namna isipokuwa kusimama na kulisogeza pembeni ili tupite, wakati tunafika na kulikagua sasa tuliona damu zikiwa zinachuruzika pembeni,
“babu itakua mboga hii wale jamaa wameangusha labda ni wawindaji” alisema Yule kijana kwa maana ya kushawishi tufungue lile gunia, hivyo tukapaki pembeni na kufungua,
Lahaulaaa wakati tunakata zile kamba sasa wote tulipigwa na bumbuwazi baada ya kushuhudia mwili wa binadamu ukiwa katika hali ile,
Mzee Tito sasa alitulia kidogo kama anayetafuta maneno ya kusema, huku akiniangalia usoni na kisha akamtazama mkewe kana kwamba anauliza aendelee ama la,na kisha akaendelea
Kwahiyo tukatoa lile gunia na kujaribu kusikiliza mapigo ya moyo na tukashangaa sana kuona bado kulikua na uhai!

Kwa dakika kadhaa tulikaa kimya tusijue tufanyaje na mwisho tukaona tuuache ule mwili pale pale,
Tulikua na sababu kadhaa za kuacha ule mwili pale,
kwanza hakukua na uhakika wa kupona kwa hali ile, lakini pia hatukujua ni kitu kilifanya ule mwili kuwa pale,
Lakini pia tulikuwa na mizigo kadhaa na sisi wawili vipi tuchukue na huyu mtu ambaye ni nusu mfu?
na hivyo tukawasha piki piki na kuondoka,
Baada ya kwenda kama nusu kilometa hivi sasa nilipaza sauti kumtaka yule kijana asimamishe piki piki,
“tunarudi kuuchukua ule mwili!” nilisema na Bila kubisha yule kijana akasimamisha piki piki tukageuza!
na kwa bahati tukaukuta ukiwa pale pale,
Ilibidi mimi niendeshe piki piki kisha Yule kijana akaushikilia ule mwili pale kati kati yetu na safari ikaanza nakumbuka tulifika saa 6 usiku huku tukiwa tumechoka sana,
Na kila kitu kikaanzia pale hadi siku ile ulipozinduka! Alisema mzee Tito huku akifuta machozi
‘mke wangu hakuamini kama wewe ulikua hai mpaka baadae nilipomuaminisha kuwa unaweza kupona ndipo akaanza kuniunga mkono na kunisaidia kutengeneza dawa na kukutunza mpaka leo hii” alimalizia mzee Tito huku akinisihi sasa nikalale kwani kwa siku ile mazungumzo yalikuwa yametosha,
“kwa leo inatosha mwanangu, Mungu akipenda na wewe ipo siku utatusimulia hadithi yako, tuna imani kisa chako kinasisimua sana, jambo moja tu tunakuhakikishia tuko pamoja na wewe, haya kalale baba” alisema mama Zawadi!
Nilisimama na kurudi zangu chumbani kwangu huku nikitafakari maneno ya Yule mzee
“kwahiyo kumbe nilitupwa msituni kwenye gunia, je nani alifanya hivyo?” nilijaribu kuwaza huku nikiwa najaribu kufumba macho kuutafuta usingizi,
Ni wakati nikiwa nimelala ghafla niliota ndoto nilijiona Nipo kwenye ukumbi kama wa mikutano hivi nikiwa mmojawapo wa watu wengine wengi wanaume kwa wanawake, ilikua ni kama semina hivi na sikuweza kuelewa mara moja ilikua inahusu nini, kulikuwa na makelele ya watu kupita pita na kufanya kukosekana kwa utulivu pale ndani,
Mara aliingia mwanamke mmoja akiwa na walinzi huku na huku kisha sisi sote tukasimama na kumpigia makofi, Yule mama akatupungia mikono na kisha akatuashiria kukaa, mara akaanza kupita kwa mtu mmoja mmoja kumuuliza jina lake na sehemu anayotokea alipofika kwenye meza yangu nikasimama na kumpa mkono huku nikitetemeka na kisha akaniuliza jina langu
“naitwa Ephraim” nilisema huku nikitoa mkono wangu na kumpa alitabasamu kisha akasema
“mume wangu pia anaitwa Ephraim” alisema Yule mwanamke huku watu wakiangua kicheko
Mara ghafla wakaingia watu waliovaa nguo za jeshi na kuanza kurusha risasi huku na huko tukaanza kukimbia huku na huko nilijikokota na na kutafuta mlango wa kutokea na kufanikiwa kutoka nje mara ghafla mbele yangu alikua Yule mwanamke akitabasamu huku akiwa amenielekezea bastola usoni
“nakuuaaaa” alisema huku akiachia risasi, niliiona ile risasi ikiwa inakuja pole pole kama kwenye filamu ,
“hapanaaaaaaaaaaaa!” nilisema kwa sauti huku nikisimama kitandani na kukaa, jasho lilikuwa linanitoka na kwa hivi Mzee Tito na mkewe tayari walikuwa mlangoni wakibisha!

“vipi kuna shida ? tafadhali fungua!” ilikua sauti yam zee Tito
‘hakuna Shida mzee tutaongea asubuhi naombeni mkapumzike,
Niliamka sasa kisha nikachukua kidaftari kidogo ambacho nilikuwa naandika baadhi ya kumbu kumbu ambazo zilikua zinanijia na ndoto nilizokuwa naota katika siku za karibuni nikaandika ile ndoto kisha nikapanda kitandani kulala.
Kesho yake asubuhi sasa niliwasimulia mzee Tito ile ndoto pamoja na lile jina ambalo nilitamka katika ile ndoto sasa mama Tito alikuwa ameshika mdomo tu akishangaa
“inawezekana jina lako ni hilo la Ephraim, sasa je Yule mwanamke ni nani na ile semina ilihusu nini?” mzee Tito alisema
“ehee nina wazo” sasa nilisema huku macho yakiwa yamenitoka
“ndio tunakusikiliza” alisema mzee Tito na mkewe kwa pamoja
“nahitaji kupata simu ambayo inaweza kuingia mtandaoni” nilisema huku nikiwa na uhakika na wazo langu
“ngoja tulifanyie kazi kesho tutafute simu pamoja na line ya fastel nadhani huku msituni inaweza kuwa inashika nimeona kwenye matangazo yao” alisema mzee Tito.
Ni kweli kesho yake alikuja akiwa na simu nzuri ya HTC pamoja na kadi ya Fastel na kama tuliovyotegemea ilikua na mtandao mzuri kabisa…
 
Huu uzi ni wa masikini wa kutupwa.
Hivi Mimi tajiri, au mwajiliwa ntapata wapi muda wa kusoma utopolo
 
Huu uzi ni wa masikini wa kutupwa.
Hivi Mimi tajiri, au mwajiliwa ntapata wapi muda wa kusoma utopolo
Mbona roho zenu zina sumu sana? Kwani umeshikiwa fimbo usome au umelazimishwa?

huo sio uungwana kuita wenzako masikini na dharau. Hizi tabia za kukatisha wasimuliaji ni tabia za kimasikini. Pita mbali sio lazima umlatishe tamaa. .

Very pathetic 😔
 
Back
Top Bottom