blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,278
- 7,966
- Thread starter
- #181
Mkuu nawekaLeo Mkuu umetuweka sana shusha mzigo tunausubiri Kwa hamu sanaa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu nawekaLeo Mkuu umetuweka sana shusha mzigo tunausubiri Kwa hamu sanaa
Umetisha Mkuu... Umetisha sanaTumo katika pango kubwa lililo kwenda juu sana, hata kwa juu lilikuwa kadiri ya hatua mia moja. Kutoka pango hilo mapango madogo yaliingia katika mlima.
Basi tulitaka kutazama kila mahali, lakini Gagula hakutupa nafasi, yeye alikwenda mbele mpaka mwisho wa pango kubwa, tukamfuata.
Tulipofika huko tuliona mlango mwingine na Gagula akatugeukia akauliza, ‘Mko tayari kuingia katika Mahali pa Mauti?’
Tukajibu, ‘Haya tu tayari.’
Bwana Henry akasema, Mambo yanaanza kutisha sasa.’ Basi wakanipa nafasi mimi nitangulie, lakini katika roho yangu niliogopa, mpaka Bwana Good aliposema, ‘Haya, twende rafiki, au kiongozi wetu mzuri atatupoteza.’
Basi kuambiwa haya, nikaanza kuingia katika kinjia, na baada ya hatua ishirini hivi, nilijiona katika pango lingine.
Lilikuwa giza kidogo, lakini nilipozoea giza niliona meza ndefu na mwisho wa meza sanamu jeupe kubwa imekaa, na kuzunguka meza masanamu meupe mengine yenye kimo cha mtu.
Tena nikaona katikati sanamu jingine jeusi kidogo, na macho yangu yalipozoea giza nilitambua masanamu yale ni nini, nikageuka nikakimbia kutoka pango lile kadiri nilivyoweza kwenda mbio.
Kwa kawaida mimi siyo muoga sana, wala siogopi mambo ya kishetani, lakini nakiri kuwa niliyoyaona yalinitisha sana, na Bwana Henry asingalinizuia ningetoka pangoni upesi, na nisingekubali kuingia tena, hata kwa almasi zote zilizopo duniani.
Lakini Bwana Henry alinikamata baraabara, na kwa hivyo nilisimama, Lakini, mara na yeye macho yake yalizoea giza na yeye aliona yale niliyoyaona mimi, mara akaniacha akaanza kujifuta jasho usoni.
Bwana Good akashangaa kabisa, na Foulata akamkumbatia huku akilia tu. Gagula tu ndiye aliyecheka sana.
Mambo tuliyoyaona yakawa ya kutisha mno. Maana mwisho wa meza ile ndefu tuliona mifupa ya mtu mrefu sana, urefu wa futi kumi na tano au zaidi, naye ameshika mkuki mkononi, akawa kama sanamu za hayo Mauti yenyewe.
Nikasema, ‘Je, hi! Ni nini?’ Na Bwana Good akaonyesha wale waliokuwa wamekaa mezani akasema, ‘Na hawa ni nani?’
Na Bwana Henry akaonyesha Yule mweusi kidogo akauliza, ‘Na huyu ni nani?’
Gagula akacheka, ‘Hee!Hee!Hee! Maovu yanawajia wote waingiao Mahali pa Mauti. Hee! Hee!Hee!Ha!Ha! Njoo Ndovu, wewe uliye shujaa katika vita, njoo mtazame Yule uliyemuua.’
Na kizee huyu akamshika kwa vidole vyake vyembamba akamwongoza kwenye meza. Sisi tukafuata. Alipofika akasimama akamwonyesha Yule mweusi kidogo, Bwana Henry akastuka akarudi nyuma.
Maana pale mezani maiti yaTwala ilikuwepo, mfalme wa hivi karibuni wa Wakukuana, alikaa na kichwa chake amekipakata.
Na maiti huyo alifunikwa chumvi; tukasikia matone ya maji yakidondoka, tukafahamu kuwa maiti ya Twala inageuzwa kuwa jiwe, yaani kwa dawa iliyomo katika yale maji yanyodondoka.
Tukatazama masanamu yale mengine na tukafahamu Maiti za wafalme wa zamani zimekaa kuzunguka meza, na maiti ya mfalme Twala imekaa juu ya meza imepakata kuwa wale ni maiti wafalme wa zamani, na sasa wamekwisha geuka kuwa masanamu ya mawe kwa ile dawa.
Tukahesabu masanamu ishirini na saba, na ile ya mwisho ilikuwa sanamu ya baba yake Ignosi, na kila moja limegeuka jiwe.
Tukaona kuwa desturi hii ya kuweka maiti za wafalme hapa ni ya zamani sana. Lakini sanamu ile kubwa iliokaa mwisho wa meza tuliona kuwa ni kazi ya mikono ya watu wale waliochonga Wale Watatu Walio Kimya.
Hahaah Gagula ni noma sanaUmetisha Mkuu... Umetisha sana
Shukran, Karibu sana mkuu
Noma mkuu, wacha nitafune sura ya 15Hahaah umekutana na Gagula nini?
Bwana Good alilala masaa 18 [emoji23] [emoji23] [emoji23], noma ssna MakumazahnLakini niliona kuwa siha zake kwa Bwana Henry zilikithiri, baadaye tulikuja kujua kuwa askari hawakumfananisha Bwana Henry na mwanadamu wa kawaida.
Walisema kuwa hapana mwanadamu aliyeweza kupigana na Twala kama yeye alivyopigana naye, na hasa baada ya siku ya vita kama vile, maana Twala alisifiwa kuwa si mfalme tu lakini ni askari shujaa kupita wote.
Na pigo lile alilompiga hata kumkata kichwa likawa kama methali, yaani pigo lolote lililozidi nguvu likiitwa, Pigo la Ndovu.
Infadus akatuarifu kuwa askari wote wa Twala wamejiweka chini ya amri ya Ignosi, na wale waliokaa mbali wanafika sasa kujitoa. Kufa kwake Twala kwa mkono wa Bwana Henry kumemaliza kabisa vita katika nchi, maana Skraga aliyekua mrithi hata yeye amekufa.
Baadaye Ignosi akaja kutuamkia amevaa ile almasi ya kifalme juu ya kipaji cha uso. Nikamtazama alipokuwa akija, nikajaribu kumfananisha na Yule aliyekuja kwetu, akiomba tumpe kazi miezi michache nyuma.
Basi alipokaribia nikanyanyuka nikasema, ‘Hujambo, Ewe mfalme!’
Akajibu, ‘Sijambo, Makumazahn, mimi ni mfalme kwa nguvu za mikono yenu.’ Akatuarifu kuwa mambo yote yanaendelea vizuri, naye alitumaini kufanya karamu baada ya juma mbili apate kuonekana mbele ya watu wake.
Nikamuuliza atamfanya nini Yule Gagula, akajibu, ‘Yeye ni kama waziri mwovu katika nchi, na lazima nimuue, pamoja na wachawi wote.
Ameishi sana duniani, hata hapana anayejua miaka mingapi, naye ndiye aliyewafundisha wachawi wote na kufanya nchi iwe mbaya mbele ya Mungu.’
Nikajibu, ‘Kweli, lakini anayo maarifa mengi, na ni rahisi kuharibu maarifa kuliko ‘kuyapata!’
Akajibu, ‘Kweli, ni yeye peke yake ajuaye siri ya Wale Watatu Walio Kimya, na palipozikwa wafalme.’ Nikasema, ‘Ndiyo, na usisahau kuwa almasi zipo. Usisahau, Ignosi, yale uliyoahidi kuwa utatuongoza mpaka mashimo ya almasi, hata kama itakulazimu umwache Gagula aishi.’ Akajibu, ‘Mimi siwezi kusahau, Makumazahn, nami nita yafikiri maneno uliyosema.’
Ignosi alipoondoka nilikwenda kumtazama Bwana Good, nikamkuta ameshikwa na homa kali sana. Kwa siku mbili tulifikiri kuwa lazima atakufa, tukawa na mioyo mizito sana, lakini Foulata hakukubali, akasema kuwa lazima atapona.
Usiku wa tano wa ugonjwa wake nilikwenda kumtazama usiku kabla ya kwenda kulala, nikaingia chumbani pole pole sana, na kwa mwangaza wa taa nilimwona Bwana Good, lakini hakuwa akigaagaa kama siku zote, alilala kimya kabisa. Basi nilifikiri huu ndio mwisho, na nilikaribia kulia kwa uchungu.
Mara nilisikia sauti, ‘Sh! Sh!’ Nikatambua nikaenda karibu nikaona kuwa amelala usingizi wala hakufa, Alilala hivyo kwa muda wa saa kumi na nane, na wakati huo wote ameshika mkono wa Foulata, naye hakuweza kuondoka kwa sababu aliogopa atamwamsha.
Akakaa hivi bila kujinyosha na bila kula; lakini kwa kweli alipoamka ikawa lazima kumchukua, maana hakuweza kwenda kwa sababu viungo vyake vilikufa ganzi.
[emoji39] [emoji119] [emoji119]Baada ya hivi, hakukawia kupona, lakini Bwana Henry hakumwambia habari za vitendo vya Foulata mpaka alipokuwa karibu ya kupona. Bwana Good akasema, ‘Mwambie kuwa ameniokoa, nami sitasahau kabisa wema wake.’
Nikamwambia Foulata maneno aliyosema Bwana Good na Foulata akafurahi sana, akamtazama kwa macho ya mapenzi akasema, ‘Sivyo, bwana, labda bwana wangu amesahau kuwa yeye ndiye aliyeokoa maisha yangu, na mimi ni kijakazi wa Bwana.’
Baada ya siku chache Ignosi akafanya baraza kuu akakubaliwa na wakubwa wote wa nchi. Ikawa sherehe kubwa sana, na askari wale waliobaki katika jeshi lile la Wajivu waliwekwa mbele wakapewa shukrani za mfalme kwa kazi nzuri na ushujaa waliofanya katika vita.
Kila mtu alipewa zawadi ya ng’ombe na wote wakapandishwa kuwa wakubwa katika jeshi jipya ambalo vile vile liliitwa kwa jina la Wajivu.
Tena Ignosi alithibitisha maneno yale aliyotuahidi, mbele ya watu wote, yaani, watu hawatauawa tena bila ya kuhukumiwa, naya kuwa desturi ile ya kuwafichua wachawi itakoma mara moja.
Baraza ilipovunjika tulimsuburi Ignosi tukamwambia kuwa sasa tuna hamu ya kuzifichua siri zile za Mashimo yale ya Sulemani ambayo yalikuwepo mwisho wa Njia Kuu ya Sulemani; tukamuuliza kama amekwisha pata habari yoyote, akajibu, ‘Rafiki zangu, nimepata habari kuwa ni pale wanapokaa Wale Watatu Walio Kimya, ambao Twala alitaka kumuua Foulata awe ndiye mhanga wao.
Tena ni pale katika shimo kubwa wafalme wanapozikwa; ndipo mtakapoona maiti ya Twala amekaa pamoja na wale waliomtangulia. Na hapo lipo shimo lililokwenda chini sana lililochimbuliwa na watu wa zamani sana, labda kwa makusudio ya kutafuta mawe ya thamani uliyotaja.
Hapo ndipo Mahali pa Mauti, na humo kuna chumba ambacho hakijulikani. Ila na mfalme na Gagula. Twala alikijua lakini sasa amekufa, nami sikijui, wala sijui nini kilichomo.
Lakini imesimuliwa kuwa zamani mtu mweupe alivuka milima, akaongozwa na mwanamke mmoja, akaonyeshwa chumba kile cha siri, akaonyeshwa hazina.
Lakini kabla hawajaweza kuzichukua, akampitia kinyume na kuwaambia adui zake, akafukuzwa na mfalme wa wakati ule, na tangu siku ile hapana mtu aliyeingia katika mahali hapo.’
Nikasema, ‘Hadithi hiyo ni ya kweli Ignosi, maana tuliona maiti ya huyo mtu katika milima.’ Akajibu, ‘Ndiyo, tulimwona, na sasa nimeahidi kuwa kama mnaweza kukifikia chumba hicho, mna ruhusa kuchukua mawe yale ikiwa yapo.’
Nikasema, ‘Hicho kito unachovaa juu ya kipaji cha uso kila siku chathibitisa kuwa yapo.’ Akasema, ‘Labda, kama yapo mnayo ruhusa kuchukua kadiri mnayotaka, yaani ikiwa ni lazima mniache, ndugu zangu.
’Nikasema, ‘Lazima, lazima tukitafute hicho chumba .’ Akajibu, ‘Yupo mtu mmoja tu anayeweza kutuonyesha, naye ni Gagula.’
Nikasema, ‘Na kama hatakubali kutuonyesha itakuwaje?’
Akasema, ‘Basi atakufa. Nimemwacha hai kwa kusudio hilo tu. Tumwite tuone kama atakubali.’
Akatuma mtu kumwita. Baada ya kitambo akaletwa na askari huku akiwatukana. Mfalme akamwambia askari wamwache, na mara alipoachiliwa akakaa chini, na macho yake yakang’aa kama kito, akasema, ‘Wataka nini kwangu, Ignosi? Huthubutu kunigusa, ukinigusa nitakuua papo hapo ulipokaa. Jihadhari na uchawi wangu.’
Ignosi akajibu, ‘We mbwa jike, uchawi wako haukumwokoa Twala, wala hauwezi kunidhuru mimi.
Sikiliza, nataka utwambie habari za siri za mawe yale yanayong’aa’.
Gagula akacheka, akasema, ‘Ha!Ha! Hapana ajuaye ila mimi nijuaye siri hizo, nami sitakwambia kamwe.
Mashetani weupe hawa watakwenda zao mikono mitupu.’
Ignosi akasema, ‘Lazima utaniambia. Nitakushurutisha.’ Akajibu, ‘Kwa namna gani, Ewe mfalme? Wewe kweli ni mkubwa mwenye nguvu lakini nguvu zako zinawezaje kuukamua ukweli kutoka kwa mwanamke?’
Ignosi akajibu, ‘Najua ni vigumu, lakini nitafanya.’ Gagula akasema, ‘Ndiyo, lakini kwa namna gani?’ Ignosi akasema, ‘Hivi, ikiwa huniambii, utakufa kwa mateso ya pole pole.’
Gagula akalia, akasema, ‘Kufa? Hutothubutu kunigusa; wewe hujui mimi ni nani.
Umri wangu wadhani ni miaka mingapi? Mimi niliwajua baba za baba za baba zako. Nchi ilipokuwa mpya, mimi nilikuwapo; nchi itakapokuwa imechakaa mimi nitakuwapo. Siwezi kufa ila kuuawa kwa ajali, maana hapana anayethubutu kuniua.’
Ignosi akajibu, ‘Ndiyo, lakini nakwambia kuwa mimi nitakuua.’ Akashika mkuki wake akamsimamia juu tayari. Yule kizee akasema, ‘Sitakuonyesha kabisa; huwezi kuthubutu kuniua, huwezi kabisa. Atakayeniua mimi atalaaniwa milele.’
Pole pole Ignosi akashusha mkuki hata ncha yake ilimchoma kidogo, na mara Gagula akaruka juu kwa sauti kali, kisha akaanguka chini akagaagaa, huku akisema, ‘Basi, basi, niachilie niishi nami nitakuonyesha.’
Ignosi akasema, ‘Vema. Nilihisi’ kuwa nitapata njia ya kukufanya ukubali. Kesho utafuatana na Infadus na ndugu zangu weupe, kuwaonyesha hapo mahali, na uangalie sana usifanye makosa, maana usipowaonyesha, hakika utakufa.’
Yule kizee akajibu, ‘Sitakosa, Ignosi. Ni desturi yangu kutimiza niliyoahidi. Ha!Ha!Ha! Zamani mwanamke mmoja alimwonyesha mtu mweupe kile chumba na tazama! Alipatikana na maovu. Jina lake lilikuwa Gagula vile vile.
Labda mimi na huyo mwanamke ni mmoja.’ Na mcho yake maovu yalizidi kung’aa.
Nikasema, ‘Mwongo, hayo yalitokea zamani vizazi kumi nyuma.’
Akasema, ‘Labda, labda; mtu akiishi miaka mingi pengine husahau. Labda lilikuwa jina la mama yangu nayeye aliniambia, kwa hakika jina lake lilikuwa Gagula vie vile. Lakini, angalieni, nawaambia ya kuwa katika chumba kile yalipo hayo mawe, mtaona kifuko cha ngozi kimejaa mawe meupe.
Huyo mtu alijaza kifuko hicho, lakini hakuwahi kukichukua. Alipatikana na maovu , nasema alipatikana na maovu! Labda aliyeniambia alikuwa mama wa mama yangu! Itakuwa safari ya furaha.
Tutapita katika mahali walipopigana askari juzi, tutaona maiti waliokufa katika vita. Macho yao yatakuwa yamekwisha pofuka sasa, na mbavu zao zitakuwa zimekwisha bonyeka. Ha! Ha!Ha!’
Thanks unacho pia kile cha Umsolopagas (nimesahau title yake).....kuna kipande huyu Umsolopagas anamwambia mjivuni " wewe mjivuni mbwa, nakuahidi kwamba siku ya vita nitapambana na wewe na kukongoa viungo vyako.... "Full storyView attachment 868827
Kinaitwa Allan Quarterman'( mambo ya ajabu yaliyomkuta Allan Quarterman') View attachment Allan Quarterman'.pdfThanks unacho pia kile cha Umsolopagas (nimesahau title yake).....kuna kipande huyu Umsolopagas anamwambia mjivuni " wewe mjivuni mbwa, nakuahidi kwamba siku ya vita nitapambana na wewe na kukongoa viungo vyako.... "
Thanks mkuuKinaitwa Allan Quarterman'( mambo ya ajabu yaliyomkuta Allan Quarterman') View attachment 868939
Pamoja chiefThanks mkuu
mkuu the wiseman naomba vitabu viwiliKinaitwa Allan Quarterman'( mambo ya ajabu yaliyomkuta Allan Quarterman') View attachment 868939