Huo ushauri mlifaa kuutumia kujishauri, kwamba mnapoteza muda kuja kututambia huku kwenye jukwaa la Wakenya misifa mnayopewa na hao akina Ramaphosa na kusahau hayo kwa leo hayana umuhimu mkubwa, kilicho cha maana ni ajira kwa vijana wa leo ambao hata hawamjui Mandela wala huyo Nyerere. Hawana muda na hiyo misifa, wanataka fursa, vyuma vimekaza kila kukicha.
Mlifaa kukaa muwaze jinsi gani ya kutumia fursa ya uhusiano mwema na hao Wasouth kupiga biashara ya nguvu na kujikomboa kutoka kwenye umaskini, bado mnajitetea eti mpo maskini kisa mliikomboa Afrika, miaka yote hii bado mnaikomboa Afrika?
Hebu ona hii picha hapa chini bado mnatajwa ndani ya mataifa maskini wa kutupwa....sio Afrika, yaani dunia yote mpo ndani ya mataifa kumi maskini wa kutolewa nje nje, mkihojwa mnajitetea eti mliikomboa Afrika