mwandende
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 11,005
- 20,805
Hili la kulazimisha kwenda kuaga mwili wa Magufuli hoja yapo imefeli vibaya sn.Siyo Rais, ni watumishi waokuza matukio yanayomhusu mkuu wa nchi kwa kujipendekeza.
Unaweza kukumbuka, wakati wa msiba wa hayati Rais Magufuli, kwa sababu ya ujinga na kujipendekeza, baadhi ya viongozi walikuwa wanahamasisha wananchi waende kwa wingi uwanja wa taifa, bila kujali usalama na matokeo yake watu walikufa na hakuna aliyejali wala kuwajibishwa.
Kwa matukio yanayomhusu viongozi wakuu wa nchi, waende wawakilishi tu, huku shughuli nyingine za ujenzi wa taifa zikiendelea, kama kufundisha shuleni, huduma za afya, biashara, kilimo,....
Hivi inawezekana hata wale wanainchi waliokuwa wanalia kwa uchungu pia walilazimishwa kulia?