Hai, Kilimanjaro: Komandoo Adamoo na wenzake wazawadiwa ng’ombe dume kila mmoja

View attachment 2157070

Makomandoo hao ambao ni Walinzi wa Freeman Mbowe kwa kinachoitwa ( VIP PROTECTION ), waliokamatwa na kuwekwa Gerezani kwa miezi mingi , leo wamefika Hai Mkoani Kilimanjaro pamoja na Mtuhumiwa mwenzao Mbowe , aliyeenda huko kutoa Sadaka ya Shukrani kwenye Kanisa la KKKT Nshala Machame

Pamoja na kuzawadiwa ng'ombe dume wakubwa kabisa kila mmoja , pia wamepewa BAHASHA NZITO NZITO SANA kila mmoja , ambazo ndani yake haifahamiki mmewekwa nini .

Zawadi hizo zote zimetolewa na Wazee wa Machame kama sehemu ya Shukrani zao kwa Makomandoo hao kwa Uaminifu wao kwa Mbowe kutokana na kinachoitwa Kukataa kutoa Ushahidi wa Uongo ili ionekane Mbowe ni Gaidi hata baada ya kuteswa sana kuliko karibia kifo , uaminifu wa Makomandoo hawa umewapa heshima kubwa sana mbele ya Jamii .

.
Mungu wa Mbinguni awabariki sana
 
Nadhani 'red brigade' ya Chama fulani imepata wakunaji. Ulinzi na usalama wote nchini ni muhimu sana.
 
View attachment 2157070

Makomandoo hao ambao ni Walinzi wa Freeman Mbowe kwa kinachoitwa ( VIP PROTECTION ), waliokamatwa na kuwekwa Gerezani kwa miezi mingi , leo wamefika Hai Mkoani Kilimanjaro pamoja na Mtuhumiwa mwenzao Mbowe , aliyeenda huko kutoa Sadaka ya Shukrani kwenye Kanisa la KKKT Nshala Machame

Pamoja na kuzawadiwa ng'ombe dume wakubwa kabisa kila mmoja , pia wamepewa BAHASHA NZITO NZITO SANA kila mmoja , ambazo ndani yake haifahamiki mmewekwa nini .

Zawadi hizo zote zimetolewa na Wazee wa Machame kama sehemu ya Shukrani zao kwa Makomandoo hao kwa Uaminifu wao kwa Mbowe kutokana na kinachoitwa Kukataa kutoa Ushahidi wa Uongo ili ionekane Mbowe ni Gaidi hata baada ya kuteswa sana kuliko karibia kifo , uaminifu wa Makomandoo hawa umewapa heshima kubwa sana mbele ya Jamii .

.
Hawa Watu na familia zao walipitia ktk kipindi kigumu sana ila nimeamini mafunzo ya ukamandoo yanafundisha uvumilivu wa hali ya juu sana na utii. Pia ni mshauri Mbowe asiwe na kinyongo hata Kidogo na Luteni Denis Urio,alikuwa na nia nzuri sana kwake ila madhila aliyopitia Amuulize vizuri Ling'wenya ata mutamsimulia.
 
Lakini najiuliza alipo mwenzao anayesemekana alitoweka kininja ninja vile! Sijui anaitwa Lijenje?

Na Denis Urio, je, anajisikiaje? Yule mama wa mbege pale Rau?
Itabidi ianzishwe campaign rasmi ya where is Lijenje tujue alipo na kama alikufa waliomuua wafikishwe mahakamani.
 
mambo mengine yanahitaji busara sana, mashtaka mazito kama yale yanafutwaje kirahisi namna hii. DPP atoe ufanunuzi kwa wananchi
Inabidi upeleke malalamiko yako kwa DPP kwanini amekuumiza roho namna hii kwa kumuachia Mbowe.
 
Back
Top Bottom