Haijawaji kutokea mgao wa umeme mwaka mzima, awamu hii ni kiboko

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Hii nchi Sasa inapoelekea ni pabaya, Toka Awamu ya Mkapa, haijawaji kutokea Mgao mkali wa Umeme kama huu Awamu hii inayoitwa ya sita, Mgao ambao umedumu zaidi ya Mwaka Mmoja.

Hii Serikali Sasa ikibidi tu iwashe mitambo ya kifisadi ya IPTL Kwa maana mtu unawezaje kuvumilia Mgao wa zaidi ya Mwaka Mzima, mvua zinyeshe zisinyeshe Mgao upo pale pale.

Serikali itafute Namna hata kuleta Umeme waafuta watakaoweza wanunue watakaoshindwa wakae Giza.

Awamu hii ya SITA Mimi naiita Awamu ya Giza Totoro, Bodi imevunjwa mara tatu, wakurugenzi wamebadilishwa mara mbili, lakini Mgao ni ule ule
 
Tatizo la umeme ni Serikali kuu ya Mama yetu Samia Suluhu.

Hao Mawaziri wanaohamishwa hawawezi kumaliza mgao, Serikali kuu inayo-allocate resources kwenye wizara tofauti ndio inaweza kumaliza tatizo la mgao wa umeme.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue.
 
Wakati wa dharura bodi (walaji kisiasa/kiutawala) haihitajiki sana ili kupunguza gharama, urasimu na kuwatumia wataalamu moja kwa moja kuongeza ufanisi. Kuiondoa bodi ndiyo suluhu ya kidharura badala ya kuibadilisha.
Mambo mengi ya serikali hukwama kwa sababu ya urasimu zikiwemo hizi zinazoitwa bodi ambazo wakati mwingine zaweza kutotoa maamuzi yenye weledi kwa kuwa zinaundwa kisiasa zaidi.
 
Yote haya ni hii CCM na Magufuli walipoiba uchaguzi na kuharibu mfumo wa kupata viongozi bora na wakaweka hayo maboya yaliyopo kiasi hata kupata mawaziri wenye uwezo inakuwa ngumu.
Sasa tumepata kundi la mawaziri eti nao ni chawa kazi yao kusifu na kuabudu!
Huko juu kabisa ndio yuko mzenji mambo ni vijembe tuu na sifa za kugawa hela za umma kwenye mambo yasiyo na maana mfano kununua magoli ya mpira.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Samia nchi haina umeme,yeye analegeza macho kwenye tv.Hovyo kabisa.
 
Serikali ya hivyo kabisa. Kiburi Chao kipo kwenye vyombo vya Dola.
 
Wakishamaliza kupambana na marehemu ndo watakumbuka nchi inahitaji umeme
 
mnaojenga nyumba zenu Kwa sasa, solar power ni lazima kama maji tuu, msisahau kutenga budget ya panel na battery na mtumie makampuni na mafundi wanaoeleweka, mtaokoa pesa nyingi sana kuwalipa wapuuzi wa TANESCO na mtakuwa na umeme wa uhakika Kwa miaka 25 ijayo, hata wenye nyumba tayari kama mna uwezo fungeni solar system, bongo Kuna jua kuliko mahitaji mungu ametujalia kama mafuta ya mwarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…