Haika Lawere: Wanawake ficheni Mali Zenu, Wanaume Ni Matapeli!

Haika Lawere: Wanawake ficheni Mali Zenu, Wanaume Ni Matapeli!

Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel Bi Haika Lawere jana kwenye Kitchen Party Gala amewafundisha Wanawake kuficha mali zao Wanaume wao wasizijue kwa sababu wanaume ni matapeli hivyo wakizijua watawapeli mali hizo.

Je hii inakubalika, Na Wanaume wakificha mali zao hali itakuwaje, nini maoni yako?

NB: Serikali Ithibiti Hawa Motivational Speakers Wana leta Destruction Na Mgawanyiko Mkubwa Wa Kijinsia Na Ustawi Wa Familia
Cc @
Tuko na Ngolo Kante
 
Bwashee , wanawake wana akili sana , ukipata mwanamke anaejielewa utafurahi sana , mimi niliachana na mama wa binti yangu ila tunashindana kumlea mtoto , x wife wangu alikua mke wa ukweli sana , ndio maana kaolewa ndoa tena , ukipata mwanamke anaejielewa hata mkishindwana , utaona umuhimu wake tu
Uongooiooo
 
Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel Bi Haika Lawere jana kwenye Kitchen Party Gala amewafundisha Wanawake kuficha mali zao Wanaume wao wasizijue kwa sababu wanaume ni matapeli hivyo wakizijua watawapeli mali hizo.

Je hii inakubalika, Na Wanaume wakificha mali zao hali itakuwaje, nini maoni yako?

NB: Serikali Ithibiti Hawa Motivational Speakers Wana leta Destruction Na Mgawanyiko Mkubwa Wa Kijinsia Na Ustawi Wa Familia
Cc @
Basically huyu mtoto ni mjinga.
Kwamba amefanikiwa kwa mali ya kurithi haimfanyi kuwa mjuaji wa mambo yote.
Tunajua baba yake alifariki kitambo, mama yake ni mkristo mzuri na si muongeaji au mropokaji.

Hakuna sababu wanawake kuficha mali zao kama ni mali ni yako binafsi iweke wazi na watu wajue.
Unazificha mali unamficha nani?
 
wanawake wapumbavu ndio wanaowaficha wanaume zao mali zao
Nina mfano mzuri wa mwanamke mmoja, mwizi, aliyeolewa na Katibu Mkuu wizara fulani.
Mwanamke huyo alikuwa anachakarika, lakini kipato alikuwa hamshirikishi mume wake.
Mwanamke huyo anatoka huko huko kwa huyo akina Haika.

Mwisho wa siku kazi za serikali kutokana na maadili, ikaja gundulika mke kajenga Masaki, jengo kubwa sana.
Mume kuulizwa na watu wa Maadili akasema sijui.
Kibarua kikaota mabawa, kisa wanajumba Masaki ambalo mume kumbe hana taarifa nalo.
Huyo mama hakuishia hapo.

Baadaye mama chakarikaji na wenziwe wanawake , waliunda Taasisi ya kijamii inaitwa GOIG, ilikuwa kule Mbezi Beach.
Mama mchakarikaji na wenzie waliagiza vyerehani zaidi ya 100 kutoka kwa wafadhili ili viwasaidie kina mama wahitaji.
Mama mchakarikaji akaona mambo si hayo?
Usiku mmoja akaamua kuiba zaidi ya vyerehani 50, na soko alisha lipata.
Hapo ikwa siku za mwizi arobaini, uchunguzi wa polisi ukaonyesha kuwa mama mchakarikaji ndiye mwizi.
Akapelekwa mahakamani na akafungwa miaka karibia mitano na aliamriwa kurudisha mali za taasisi.

Huo ndio uchakarikaji wa wanawake kiwizi.
Kama huibi weka mambo yako wazi.

Hii hadithi ni ya kweli.
 
Back
Top Bottom