Haina haja ya Ufaransa, UK, Canada, Australia na nchi zingine za Magharibi kuitambua Palestina kama mambo haya matatu hayafanyiki

Haina haja ya Ufaransa, UK, Canada, Australia na nchi zingine za Magharibi kuitambua Palestina kama mambo haya matatu hayafanyiki

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
3,952
Reaction score
8,807
Niaje waungwana

Japo hatua ya mataifa ya Magharibi kama vile UK, Ufaransa, Canada, Australia, Spain, Ireland nk imeonesha kuwafurahisha wengi, na kuwapa matumaini ya kuona mwisho wa vita kati ya Israel na Palestina au Hamas umefika. Mimi binafsi naona hali haiwezi kuwa hivyo wanavyofikiria hadi mambo haya matano yatimizwe au yaende kutimizwa haraka iwezekanavyo.

1. Kwanza iundwe mipaka ile inayotambuliwa na Umoja wa mataifa ili kuhakikisha hakuna nchi inayojiongezea hata nusu ya hatua moja ya binadamu katika ardhi ya nchi nyingine.

2. Umoja wa mataifa utume vikosi vya askari wa kulinda amani katika mipaka inayogawa mataifa hayo mawili, ili kuhakikisha hakuna mlowezi yoyote wa kiyahudi, au askari wa Israel anavuka boda kuingia nchini Palestina bila kufuata utaratibu wa sheria na mipaka ya kimataifa.

Halikadhalika Hamas, na jeshi la Palestina pia wasiingie nchini Israel bila kufuata utaratibu wa sheria na mipaka ya kimataifa. Hili litaondoa mivutano na mapigano yoyote yanayoweza kutokea siku za mbele.

3. Kama ilivyo Israel ambayo imekuwa ikitetewa, ikisaidiwa na kupewa haki ya kujilinda na nchi za Magharibi hata pale inapoonesha uchokozi wa wazi kwa nchi nyingine.

Haki hiyo ya kutetewa, au kujitetea na kujilinda pia inatakiwa ipewe na Palestina, ili itapovamiwa na walowezi wa kiyahudi katika ardhi yake basi iwe na haki ya kujilinda kwa jeshi na silaha dhidi ya uvamizi huo.

Sio Hamas wakivamia Israel nchi za Magharibi zote ziipe silaha Israel ili ipambane na kuwauwa Hamas, lakin walowezi wakivamia Palestina nchi hizo za Magharibi ziishie kulalamika na Palestina ikichukua hatua ya kulinda ardhi yake waiwekee vikwazo kwa madai ya kukiuka haki za binadamu nk.

4. Wawe tayari kuiwekea vikwazo vya kiuchumi, kisilaha na kiutawala nchi yoyote itakayoivamia nchi nyingine, bila kujali kuwa nchi hiyo ni Israel au Palestina. Na wai support kwa nguvu zote nchi iliyovamiwa kama wanavyofanya sasa hivi huko Ukraine baada ya nchi hiyo kuvamiwa na Urusi miaka kadhaa uliyopita.

5. Mwisho kabisa itolewe amri kwa jeshi la Israel na HAMAS.
(a) Israel iamrishwe kuondoa jeshi lake mjini Gaza, otherwise nguvu za kijeshi zitumike kutoka ktk nchi hizo kuliondoa jeshi hilo la Israel ktk ardhi ya Gaza.

(b) Hamas nao waamrishwe kuwaachia kateka waliobaki, otherwise na wao wakumbane na mashambulizi ya kijeshi kutoka ktk nchi hizo. Japo nafikiri Hamas watakubali kuwaachia mateka wote baada ya jeshi la Israel kutimuliwa kutoka Gaza.

Kinyume na hayo mambo ma5 niliyoyaeleza hapo juu, basi itakuwa hakuna maana yoyote ya kulitambua taifa la Palestina, huku likiendelea kuachwa libaki kama nchi ya Haiti ambayo haina jeshi, polisi, migration wala mgambo.

Hii itapelekea walowezi wa kiyahudi kila siku kuendelea kuifanya Palestina shamba la bibi, kwa kuingia katika nchi hiyo kujichukulia ardhi na mali bila kufanywa lolote.

Wazungu wajanja sana. Wanajifanya kuitambua Palestina huku nyuma ya pazi wanajua wanachokifanya. So ili kuonesha kama wapo serious, hayo ndio mambo ya msingi kufanya ili kumaliza vita na kuleta amani ya kweli ya kudumu. Otherwise ni kudanganyana tu na kujaribu kuwaburuza watu wasioona mbali.
 
Mambo matano na sio matatu. Please moderator yoyote naomba arekebishe hapo kwenye matatu aweke matano.
 
Kila jambo linaenda kwa hatua,huko nyuma hawakutaka hata kuitambua Palestine ila hali ya kidunia na msukumo ndani ya mataifa yao vimechagiza haya yote.
 
Kila jambo linaenda kwa hatua,huko nyuma hawakutaka hata kuitambua Palestine ila hali ya kidunia na msukumo ndani ya mataifa yao vimechagiza haya yote.
Ni kweli hilo linawezekana kuja kutokea baadae, ila kama halitatokea basi utambuzi wa Palestina utakuwa hauna maana.
 
Israel na Palestina iwe nchi moja kama ilivyo Tanganyika na Zanzibar. Kuwe na rais wa Palestina na rais wa serikali ya muungano. Hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza mgogoro. Israel hatakubali Palestina iwe nchi huru maana ni kuhatarisha usalama wake.
 
Hamas waache Vita na wakati agizo la allah la kuwaangamiza Wayahudi halijatimia!. Mara zote nne Palestine ndiyo uvunja mkataba wa Two states solution si israel.
Hamas waache vita vipi na wakati kuna wazungu walitoka Ulaya kuja kuikalia na kiutawala nchi yao kwa nguvu?!
Hivi hawa wavamizi wanaouwa wapalestina huko West bank unawaona wana haki ya kuuwa wengine bila na wao kuuwawa?

Hiyo mara 4 uliyoandika hapa Iko wapi? Mbona umeandika bila kuweka facts (ushahidi) wa kile ulichoandika?

Kwa sasa kila mtu anafahamu na kuona kwamba Israel ndio inasitisha zoezi la kuwepo mataifa mawili. Hivyo unatakiwa uweke facts zinazoonesha kuwa Palestina na yenyewe ilikuwa inakwamisha mchakato wa kuwepo mataifa mawili ili kukubaliana na kile ulichoandika. Na sio porojo za kwenye kanga na vijiwe vya wanywa gongo.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hamas wajiindoe wawapishe PLO chini ya Mahamoud Abbas, nchi itatulia hata bila mipaka.

Lakini hata mipaka haitapatikani chini ya uwepo wa Hamas ni magaidi, wasemavyo Israel.

Maamuzi ya kuichukua Gaza ni kwasababu hamas hawataki kuwaachia mateka, na hawataki kuweka silaha chini, hivyo kuhalalisha vita!vyao dhidi ya Israel.

Sielewi kwanini hawa HAMAS hawajielewi, mateka wanawasaidia nini mpaka sasa Wapalestina wanakufa kwa magonjwa, njaa na vita.

Mateka wanafaida gani kwa HAMAS?

Binafsi napenda vita na acha watwangane mpaka tone la mwisho kisha tutajadili matakwa ya mshindi tu.
 
Hicho kitu hakitowezekana.
Gaza ndo ishachukuliwa hivyo.
 
Israel na Palestina iwe nchi moja kama ilivyo Tanganyika na Zanzibar. Kuwe na rais wa Palestina na rais wa serikali ya muungano. Hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza mgogoro. Israel hatakubali Palestina iwe nchi huru maana ni kuhatarisha usalama wake.
Sidhani kama Netanyahu anaweza kukubali hilo litokee hata siku 1.
 
Hamas wajiindoe wawapishe PLO chini ya Mahamoud Abbas, nchi itatulia hata bila mipaka.
Wewe unazungumzia Hamas peke yao, vipi kuhusu walowezi wanaovamia ardhi za wapalestina na kuwaua bila sababu kule West Bank?

Au wenyewe wana haki ya kuvamia ardhi za wenzao na kufanya chochote wanachotaka?
Lakini hata mipaka haitapatikani chini ya uwepo wa Hamas ni magaidi, wasemavyo Israel.
Siku zote ukipigania haki yako dhidi ya wazungu lazima uitwe gaidi kama ilivyokuwa kule bondeni kwa makaburu enzi za ubaguzi wa rangi. Hivyo sio kila gaidi ana tatizo. Muda mungine ni watawala ndio husababisha watawaliwa kuamua kufanya vitendo vya kujiokoa, na kujilinda, ambavyo baadae huja kuitwa magaidi.
Maamuzi ya kuichukua Gaza ni kwasababu hamas hawataki kuwaachia mateka, na hawataki kuweka silaha chini, hivyo kuhalalisha vita!vyao dhidi ya Israel.
Sio kweli.. Hamas walikuwa wapo tayari kuwaachia mateka wote awamu kwa awamu chini ya ule mkataba wa mwanzo ambao uliwataka waisrael waondoe jeshi lao katika ardhi yote ya Gaza, na Hamas waachie mateka wote wanaowashikilia, Netanyahu na genge lake wakagoma.
Sielewi kwanini hawa HAMAS hawajielewi, mateka wanawasaidia nini mpaka sasa Wapalestina wanakufa kwa magonjwa, njaa na vita.
Sababu ya hiki usichoelewa hapa, nishakupa hapo juu kwamba Netanyahu ndio chanzo cha hilo la mateka kutoachiwa wote.
Mateka wanafaida gani kwa HAMAS?

Binafsi napenda vita na acha watwangane mpaka tone la mwisho kisha tutajadili matakwa ya mshindi tu.
Obvious Israel inaweza kufanya kile inachofanya Gaza si kwa sababu wana nguvu, bali kwa sababu wana support kubwa mno kutoka kwa Marekani na nchi zingine za magharibi.

angalia ukubwa wa jeshi la Israeli ambalo limeita hadi wanajeshi wa akiba dhidi ya kikundi kisichofikisha hata vijana elf 5, angalia silaha za Israel dhidi ya kundi lisilokuwa hata na kifaru ki1

Leo hii jeshi la wananchi wa Tanzania liingie kazini kupambana na panya road wasiokuwa na silaha zozote za maana au waandamanaji alaf mtu mwenye akili ukae et ukisubiri kuona nani ataibuka mshindi!!
 
neta hataki mateka warudi na anafanya kila linalowezekana wasirudi
Anajua wakirudi na vita ikiisha, ile kesi yake ya ufisadi itaibuka tena na ataweza kufungwa
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Hamas waache vita vipi na wakati kuna wazungu walitoka Ulaya kuja kuikalia na kiutawala nchi yao kwa nguvu?!
Hivi hawa wavamizi wanaouwa wapalestina huko West bank unawaona wana haki ya kuuwa wengine bila na wao kuuwawa?

Hiyo mara 4 uliyoandika hapa Iko wapi? Mbona umeandika bila kuweka facts (ushahidi) wa kile ulichoandika?

Kwa sasa kila mtu anafahamu na kuona kwamba Israel ndio inasitisha zoezi la kuwepo mataifa mawili. Hivyo unatakiwa uweke facts zinazoonesha kuwa Palestina na yenyewe ilikuwa inakwamisha mchakato wa kuwepo mataifa mawili ili kukubaliana na kile ulichoandika. Na sio porojo za kwenye kanga na vijiwe vya wanywa gongo.
Kuna jamaa mmoja ni mpalestina sijui anaitwa Salim(if I'm not mistaken) huyu jamaa ni mpigania uhuru wa Palestine lakini anavyojenga hoja bila unafiki bila na kukataa facts za kihistori ni Mtu muhimu sana kwa kuleta aman kati ya israel na the so called Palestine Sadly watu ambao wapo logically ndiyo hawapewi nafasi ya kusikilizwa.
mfn; mtu kama wewe unaamini kuwa Kuna kundi flan la wazungu walihama kutoka Poland ama Ujeruman wakaenda kujipachika mashariki ya kati na kuanzisha taifa it so called Israel hupaswi kabisa kusogelea hata jumba mnamofanyika Mkutanao wa majadiliano ya aman kati ya Palestine na Hamas maana upo too illogical.
Four Times Palestinians Rejected a Two-State Solution | by Luisa Rodriguez | Medium https://share.google/8LiqRZCx18wKrIRAb
 

Attachments

  • Screenshot_20250925_090202_Chrome.jpg
    Screenshot_20250925_090202_Chrome.jpg
    235.7 KB · Views: 38
Two states solution kama ambavyo haikuleta aman na ikakataliwa uko nyuma zaidi ya mara Nne bado haitafanikiwa kuleta Aman mara hii ya tano. zaidi hicho kipande cha Ardhi watakachopewa Wapalestina kitaendelea kutumika kama buffer zone kati ya israel na maadui zake.
ni fact kuwa kupigana nq israel kwa njia ya proxy wars ni effective zaidi kuliko nchi adui wa israel kupigana na israel kupitia conventional warfare.
ndiyo maana leo ni mwaka wa pili israel bado inang'ang'ana na Hamas wakati israel hiyo hiyo imetumia siku 12 kuitepetesha Iran ambaye ndiye baba wa hamas na Hezbollah.
 
Back
Top Bottom