Haina haja ya Ufaransa, UK, Canada, Australia na nchi zingine za Magharibi kuitambua Palestina kama mambo haya matatu hayafanyiki

Haina haja ya Ufaransa, UK, Canada, Australia na nchi zingine za Magharibi kuitambua Palestina kama mambo haya matatu hayafanyiki

Wewe unazungumzia Hamas peke yao, vipi kuhusu walowezi wanaovamia ardhi za wapalestina na kuwaua bila sababu kule West Bank?

Au wenyewe wana haki ya kuvamia ardhi za wenzao na kufanya chochote wanachotaka?

Siku zote ukipigania haki yako dhidi ya wazungu lazima uitwe gaidi kama ilivyokuwa kule bondeni kwa makaburu enzi za ubaguzi wa rangi. Hivyo sio kila gaidi ana tatizo. Muda mungine ni watawala ndio husababisha watawaliwa kuamua kufanya vitendo vya kujiokoa, na kujilinda, ambavyo baadae huja kuitwa magaidi.

Sio kweli.. Hamas walikuwa wapo tayari kuwaachia mateka wote awamu kwa awamu chini ya ule mkataba wa mwanzo ambao uliwataka waisrael waondoe jeshi lao katika ardhi yote ya Gaza, na Hamas waachie mateka wote wanaowashikilia, Netanyahu na genge lake wakagoma.

Sababu ya hiki usichoelewa hapa, nishakupa hapo juu kwamba Netanyahu ndio chanzo cha hilo la mateka kutoachiwa wote.

Obvious Israel inaweza kufanya kile inachofanya Gaza si kwa sababu wana nguvu, bali kwa sababu wana support kubwa mno kutoka kwa Marekani na nchi zingine za magharibi.

angalia ukubwa wa jeshi la Israeli ambalo limeita hadi wanajeshi wa akiba dhidi ya kikundi kisichofikisha hata vijana elf 5, angalia silaha za Israel dhidi ya kundi lisilokuwa hata na kifaru ki1

Leo hii jeshi la wananchi wa Tanzania liingie kazini kupambana na panya road wasiokuwa na silaha zozote za maana au waandamanaji alaf mtu mwenye akili ukae et ukisubiri kuona nani ataibuka mshindi!!
Ushaanza kutupiga kamba na wewe, Hamas hawana hata kifaru 1?? Una maana Hamas hawana silaha, hawana makombora.

Oct 7 walitumia mawe??
Kama ni kweli Hamas hawana hizo zana si wangepukutishwa mapema sana.

Una hoja ila unazidisha ushabiki kwa Hamas mpaka unatia porojo.

Hamas na Israel wote ni wahalifu tu.
 
Ushaanza kutupiga kamba na wewe, Hamas hawana hata kifaru 1?? Una maana Hamas hawana silaha, hawana makombora.

Oct 7 walitumia mawe??
Kama ni kweli Hamas hawana hizo zana si wangepukutishwa mapema sana.

Una hoja ila unazidisha ushabiki kwa Hamas mpaka unatia porojo.

Hamas na Israel wote ni wahalifu tu.
Silaha kama vile makombora, rocket nk hizo wanazo ila swala la kumiliki kifaru sina uhakika.
 
Niaje waungwana

Japo hatua ya mataifa ya Magharibi kama vile UK, Ufaransa, Canada, Australia, Spain, Ireland nk imeonesha kuwafurahisha wengi, na kuwapa matumaini ya kuona mwisho wa vita kati ya Israel na Palestina au Hamas umefika. Mimi binafsi naona hali haiwezi kuwa hivyo wanavyofikiria hadi mambo haya matano yatimizwe au yaende kutimizwa haraka iwezekanavyo.

1. Kwanza iundwe mipaka ile inayotambuliwa na Umoja wa mataifa ili kuhakikisha hakuna nchi inayojiongezea hata nusu ya hatua moja ya binadamu katika ardhi ya nchi nyingine.

2. Umoja wa mataifa utume vikosi vya askari wa kulinda amani katika mipaka inayogawa mataifa hayo mawili, ili kuhakikisha hakuna mlowezi yoyote wa kiyahudi, au askari wa Israel anavuka boda kuingia nchini Palestina bila kufuata utaratibu wa sheria na mipaka ya kimataifa.

Halikadhalika Hamas, na jeshi la Palestina pia wasiingie nchini Israel bila kufuata utaratibu wa sheria na mipaka ya kimataifa. Hili litaondoa mivutano na mapigano yoyote yanayoweza kutokea siku za mbele.

3. Kama ilivyo Israel ambayo imekuwa ikitetewa, ikisaidiwa na kupewa haki ya kujilinda na nchi za Magharibi hata pale inapoonesha uchokozi wa wazi kwa nchi nyingine.

Haki hiyo ya kutetewa, au kujitetea na kujilinda pia inatakiwa ipewe na Palestina, ili itapovamiwa na walowezi wa kiyahudi katika ardhi yake basi iwe na haki ya kujilinda kwa jeshi na silaha dhidi ya uvamizi huo.

Sio Hamas wakivamia Israel nchi za Magharibi zote ziipe silaha Israel ili ipambane na kuwauwa Hamas, lakin walowezi wakivamia Palestina nchi hizo za Magharibi ziishie kulalamika na Palestina ikichukua hatua ya kulinda ardhi yake waiwekee vikwazo kwa madai ya kukiuka haki za binadamu nk.

4. Wawe tayari kuiwekea vikwazo vya kiuchumi, kisilaha na kiutawala nchi yoyote itakayoivamia nchi nyingine, bila kujali kuwa nchi hiyo ni Israel au Palestina. Na wai support kwa nguvu zote nchi iliyovamiwa kama wanavyofanya sasa hivi huko Ukraine baada ya nchi hiyo kuvamiwa na Urusi miaka kadhaa uliyopita.

5. Mwisho kabisa itolewe amri kwa jeshi la Israel na HAMAS.
(a) Israel iamrishwe kuondoa jeshi lake mjini Gaza, otherwise nguvu za kijeshi zitumike kutoka ktk nchi hizo kuliondoa jeshi hilo la Israel ktk ardhi ya Gaza.

(b) Hamas nao waamrishwe kuwaachia kateka waliobaki, otherwise na wao wakumbane na mashambulizi ya kijeshi kutoka ktk nchi hizo. Japo nafikiri Hamas watakubali kuwaachia mateka wote baada ya jeshi la Israel kutimuliwa kutoka Gaza.

Kinyume na hayo mambo ma5 niliyoyaeleza hapo juu, basi itakuwa hakuna maana yoyote ya kulitambua taifa la Palestina, huku likiendelea kuachwa libaki kama nchi ya Haiti ambayo haina jeshi, polisi, migration wala mgambo.

Hii itapelekea walowezi wa kiyahudi kila siku kuendelea kuifanya Palestina shamba la bibi, kwa kuingia katika nchi hiyo kujichukulia ardhi na mali bila kufanywa lolote.

Wazungu wajanja sana. Wanajifanya kuitambua Palestina huku nyuma ya pazi wanajua wanachokifanya. So ili kuonesha kama wapo serious, hayo ndio mambo ya msingi kufanya ili kumaliza vita na kuleta amani ya kweli ya kudumu. Otherwise ni kudanganyana tu na kujaribu kuwaburuza watu wasioona mbali.
Haya matakwa kutimizwa ni mambo yakufikirika tu hayawezi kuwekwa kwenye utekelezaji
 
Haya matakwa kutimizwa ni mambo yakufikirika tu hayawezi kuwekwa kwenye utekelezaji
Hilo linajulikana ndomaana wenye akili wanaona ni danganya toto.
 
Silaha kama vile makombora, rocket nk hizo wanazo ila swala la kumiliki kifaru sina uhakika.
Ni jeshi lile sema kwa kutafuta huruma ndio mnasema hivyo, ila wako vizuri ndio maana mpaka leo Israel haijafanikiwa kuwapata hao mateka.

Na sasa wanalipua majengo tu ambayo ndanimwe hamna wanamgambo wa Hamas.

Wako vizuri hao jamaa, sio wa kuwachukulia poapoa.
 
Hamas waache vita vipi na wakati kuna wazungu walitoka Ulaya kuja kuikalia na kiutawala nchi yao kwa nguvu?!
Hivi hawa wavamizi wanaouwa wapalestina huko West bank unawaona wana haki ya kuuwa wengine bila na wao kuuwawa?

Hiyo mara 4 uliyoandika hapa Iko wapi? Mbona umeandika bila kuweka facts (ushahidi) wa kile ulichoandika?

Kwa sasa kila mtu anafahamu na kuona kwamba Israel ndio inasitisha zoezi la kuwepo mataifa mawili. Hivyo unatakiwa uweke facts zinazoonesha kuwa Palestina na yenyewe ilikuwa inakwamisha mchakato wa kuwepo mataifa mawili ili kukubaliana na kile ulichoandika. Na sio porojo za kwenye kanga na vijiwe vya wanywa gongo.
Kwa Hoja zako hizi hiyo vita haitokaa iishe, never sahau akilini mwako, focus na nchi Yako Tanganyika
 
Kwa Hoja zako hizi hiyo vita haitokaa iishe, never sahau akilini mwako, focus na nchi Yako Tanganyika
Tanzania nisha focus sana tu. Labda wewe sio mfuatiliaji wa JF.
 
Mambo wasio yapenda kusikia ni hayo iliyoandikwa....
 

Attachments

  • free.palestine.kg_62a04f3969174165ab259afecc3d9e3c.mp4
    2 MB
Back
Top Bottom