Haina haja ya Ufaransa, UK, Canada, Australia na nchi zingine za Magharibi kuitambua Palestina kama mambo haya matatu hayafanyiki

Umeandika ujinga mtupu. Na hii ni kwa sababu JF inaruhusu watu wajiunge bila kuhusisha elimu zao na taalum zao.

Hapo tayari na ww usiejua tayari ushajiona unajua kuliko sisi wenye kujua!!

Ukitaka kujua nguvu ya mtu angalia ghofu ya adui zake.
Unajua ni kwanini Israel, Marekani, UK, Ufaransa Ujerumani na mataifa mengine mnayosema yana nguvu yanaihofia Iran na kujaribu kila njia ya kuhakikisha haina uwezo wa kutengeneza hata kisu?

Au unajua ni kwa nini Iran pekee ndio iliyowekewa vikwazo vya silaha na sio Israel, Saudi Arabia, Jordan, Pakistan nk.

Jibu ni kwa sababu wanaijua Iran ina nguvu, na uwezo wa kutengeneza silaha zenye nguvu na ubora kuliko Israel na nchi nyingine nilizotaja hapo juu. Mfano ni kama siasa za kwetu, chama chenye nguvu na tishio kwa utawala ndio kinachozuiwa na kuwekewa vikwazo vya kufanya siasa zake, viongozi wao kufungwa, wafuasi kupigwa nk. Huku vile vyama dhaifu vikiachwa viendelee na shughuli zao kwa sababu ya kutokuwa na madhara yoyote kwa watawala.

So hao waoga ili ku limit nguvu hizo wakaamua bora waiwekee Iran vikwazo vikali vya kiuchumi na silaha ili kuidhoofisha, but still wameshindwa kuidhibiti ndomaana hata kwenye vita huwa wanaungana zaidi ya nchi 8 kuzuia na kuisaidia Israel kushambulia lakin wanatoka kapa.

Israel hata bila vikwazo, ikinyimwa silaha na fedha kidogo za kulipa wanajeshi wao Netanyahu anaitisha waandishi wa habari na kuanza kulalamika huku akitia huruma kama mtoto yatima alienyimwa chakula na mama wa kambo.

Je Israel akiwekewa vikwazo vya silaha hata vya miaka 5 tu ataweza kusavaivu kweli?

Iran ina vikwazo vikali vya kiuchumi, kijeshi, teknolojia kwa takriban miaka zaidi ya 60 na bado nchi mnazoita zenye nguvu zimeshindwa lengo lao la kuiangusha na kubadilisha utawala.

Narudia tena, Iran ikiondolewa vikwazo vya silaha na uchumi kwa miaka mitano au kumi tu. Nakuhakikishia kuwa hapo mashariki ya kati na Ulaya kwa ujumla watakuwa kama kuku jike ambae akimuona jogoo lazima alale chini ili apandwe.
 
Ile vita wala haipo kwenye udini,watu wa huko buza tu mmekua primitive na udini
Ni mshamba mno huyo jamaa. Kwenye comments zake kila akikosa hoja hukimbilia kujificha kwenye kichaka cha dini. Sijui udini unamsaidia nini kwenye dunia ya leo!
 
Iran anajua kuwa ana uwezo huu unaiopatia ama naye haijui?.
 
Kwa nini washirika Wahamas wasiwaambie warudishe mateka
 
Huyu alieandika hii habari hana tofauti na wew ambae unalazimisha uongo isiokuwa na tija.

Hata makaburu hujifanya kuwa wao ndio native wa Afrika Kusini, lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa jamaa ni wageni waliovamia ardhi ya wenzao.
Kwamba Israel ni ya wapalestina!
 
Ritz anafurahisha sana!
Huyo mtu aliyevow kuifuta Israel kwenye uso wa Dunia ndo asiwekewe vikwazo?
Kwamba kwake yeye kuifuta Israel ni hitaji la kiimani na kimaandiko huyo ndo aruhusiwe kuwa na nuclear?
Marekani na Ulaya wasimhofie mchina na Mrusi wamhofie muiran,are you serious?
Kutomuwekea Iran vikwazo ni sawa na kumpa kichaa rungu.
Kumbuka kuifuta Israel na kuua kila myahudi ni takwa la kimaandiko kwa baadhi ya Imani na hicho ndiyo kiini Cha mgogoro wa middle east zingine zote ni porojo!
 
Iran anajua kuwa ana uwezo huu unaiopatia ama naye haijui?.
US, UK, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Uholanzi nk wanalijua hilo, ndio maana wamekimbilia kuiwekea vikwazo vya uchumi na silaha mapema ili kuifunga mikono.

Kama haina nguvu kwanini wakose usingizi, waiwekee vikwazo na waichangie kwenye vita?

Leo hii mawaziri wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wanapanda na kushuka kila siku ili kuisihi isitengeneze silaha ambazo nchi zingine zisizokuwa na nguvu kama Israel zinaachiwa zitengeneze!

Ni wazi kuwa mwenye nguvu huwatia hofu wadhaifu.
 
Kwa nini washirika Wahamas wasiwaambie warudishe mateka
Mnazungumzia mateka wa makafiri, mbona hamuwazungumzii mateka waislamu, wengine wanafungwa wakiwa bado vijana, wanawatesa, kuwapiga na kuwauwa na wengine mpaka wanazehekea jela

Nyie watu hamuna imani wala huruma, na Qur’an tayari ilishawazungumzia.
 
Kwa nini washirika Wahamas wasiwaambie warudishe mateka
Warudishe mateka?!
Kwani Hamas haikurudisha mateka?
Au wewe mwenzetu haujui kinachoendelea duniani?

Anyway ipo hivi.. Acha nikueleweshe hapo chini.

Hamas na Israel kupitia wapatanishi wao yani Misri, Qatar na Marekani walikubaliana kwamba wasimamishe mapigano kwa awamu tatu.

1. Awamu ya kwanza Israel iwaachie wafungwa kadhaa wa kipalestina wanaozuiliwa katika jela za Israel bila makosa yoyote. Na Hamas iwaachie mateka kadhaa wanaozuiliwa na kundi hilo.

2. Awamu ya pili na kusimamisha kabisa vita na Israel kuondoa jeshi lao lote katika ukanda wa Gaza. Na Hamas iwaachie mateka wote waliobakia.

Awamu ya tatu ni au Gaza iwe chini ya Mamlaya ya Palestina au UN au Falme za kiarabu.

Sasa awamu ya kwanza ilikwenda vizuri kwa kusimamisha vita ambapo Israel iliachia wafungwa kadhaa. Na Hamas ikaachia mateka kadhaa.

Awamu ya pili Israel ikagoma kuacha mashambulizi na Ku withdraw jeshi lao kutoka Gaza. Na Hamas wakaona huo ni mtego kwamba kwanini waachie mateka wote, wakati Israel imekataa kutekeleza pendekezo la kuondoa jeshi lao Gaza.
 
read to understand without sounding Incoherently on my mention..swali ilikuwa Iran anajua kuwa ana nguvu hizo ama na yeye hajui kuwa anaogopwa na dunia nzima?.
 
Ritz anafurahisha sana!
Wewe una matatizo makubwa san kichwani kwako. Hiyo Ritz ndo kitu gani na kina uhusiano gani na uzi huu!!
Huyo mtu aliyevow kuifuta Israel kwenye uso wa Dunia ndo asiwekewe vikwazo?
Weka facts inayoonesha kuwa Iran inataka kuifuta Israel katika dunia, na sio utuwekee maneno ya kwenye kanga na vijiwe vya gongo.

dunia ya leo mambo yanaenda kielemu na ki ithibitisho thabiti, sio kuokota maneno na kuyaleta humu ukidhani kila mtu ni mjinga na mpumbavu wa kukubali maneno matupu.
Kwamba kwake yeye kuifuta Israel ni hitaji la kiimani na kimaandiko huyo ndo aruhusiwe kuwa na nuclear?
Japo mimi mambo ya imani siyapi sana nguvu lakini nafahamu Palestina, Egypt, Qatar, Jordan nk kuna raia wengi tu wenye asili ya Israeli wanaishi huko. So sijui hizo nchi ni za imani ipi?
Marekani na Ulaya wasimhofie mchina na Mrusi wamhofie muiran,are you serious?
Ndiomaana nimesema wewe una matatizo ya akili. Inamaana wewe haujui kuwa Urusi na China zinahofiwa?

Au ni wapi nilipoandika kuwa hizo nchi hazihofiwi?
Kutomuwekea Iran vikwazo ni sawa na kumpa kichaa rungu.
Kumbuka kuifuta Israel na kuua kila myahudi ni takwa la kimaandiko kwa baadhi ya Imani na hicho ndiyo kiini Cha mgogoro wa middle east zingine zote ni porojo!
Kuuwa kila myahudi ni takwa la kimaandiko?!!

Hivi unajua Iran ina raia wangapi ambao ni wayahudi?

Kwa taarifa yako Iran ni nchi ya 3 kwa wayahudi duniani.

Ya kwanza ni Israel, ya pili Marekani na ya tatu Iran.

Ina wayahudi wengi kuliko nchi yoyote ya Ulaya ukijumlisha na Russia.

Hii ni kwa mujibu wa Google ambayo ina milikiwa na hao hao wayahudi wenyewe.

Tatizo mmekuwa mkidanganywa na kulishwa matango pori huko vijiweni kwenu, kwa vile mshaonekana mko dhaifu mno kichwani.

Iran ina wayahudi kibao na hakuna hata mmoja anaeguswa aidha na raia au serikali. Wana haki sawa kama walivyo waajemi, waarabu, wahindi nk.

Ingekuwa ina lengo la kuuwa wayahudi. Wasingeenda mbali na wakati nchini kwao wapo. Wangewauwa hao hao waliopo kwao.

Lakini kwa vile ugomvi wao hauhusiani na wayahudi ndomaana mpaka leo wapo na wanaishi vizuri nchini kwao kama raia wengine na ukirusha kombora kuuwa myahudi hata mmoja nchini Iran, Ayatollah atakushugulikia kwa makombora kama kawaida bila kujali upo mbali kiasi gani.
 

Attachments

  • Screenshot_20250927_135044_Chrome.jpg
    147.5 KB · Views: 19
read to understand without sounding Incoherently on my mention..swali ilikuwa Iran anajua kuwa ana nguvu hizo ama na yeye hajui kuwa anaogopwa na dunia nzima?.
Iran ingekuwa haijui kama ina nguvu isingeingia vitani kupambana na nchi inayoshirikiana na Marekani, UK, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Saudi Arabia nk.
Hivyo inajua kama ina nguvu na inazitumia vizuri nguvu hizo pamoja na vikwazo vyote walivyo navyo.

Nchi ambayo haina nguvu na inajua kama haina nguvu ni Qatar ambayo imeshindwa kujitetea au Venezuela ambayo meli zake zinashambuliwa imeishia kulalamika huku ikishindwa kupiga hata kambi 1 ya Marekani iliyopo katika nchi yoyote ya jirani.
 
🤣🤣🤣🤣
 
Yani Israel ikubali magaidi yaunde Taifa huru ndani ya mipaka yake. Haiwezekani na Mwamba Netanyahu alishaapa kuhusu hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…