Mtu yeyote anaeanza kufanya BIASHARA sidhani kama huaga anafikiria kwamba kuna kufirisika, hua ana focus kwenye mafanikio ya biashara yake; mwanafunzi anae join chuo, sidhani kama hua anafikiria habari ya ku disco, mwanamke anaeshika mimba nae sidhani kama hua anafikiria habari za mimba kuharibika au mtoto kufa kabla hajafikisha umri fulani, hata watu wanao jenga nyumba, kupanga mipango ya maisha, wote hawa sidhani kama huaga wanapiga HESABU ya KUFA na kuviacha walivyo jitafutia, ndio maisha yalivyo, ndio tulivyo binadamu wote tulio TIMAMU. Hata mtu anae OA au kuolewa, sidhani kama hua ana mawazo ya TARAKA kwenye hilo agano lake analokwenda kuliingia soon, bado najiuliza, wewe unaingiaje kwenye ndoa na mawazo haya? Mifano yote nilioitoa hapo ju, sio kwamba wote hua wanatoboa, kuna biashara zinakufa, kuna wanafunzi wanafeli mitihani na kurudishwa nyumbani, kuna wanao pata mimba na mimba hizo zinaharibika, kibaya zaidi wapo wanao haribu mimba hata 4 but hawaachi kushika mimba zingine, zipo pia TARAKA. But sina hakika kama kuna mtu hua anaingia kwenye ndoa halafu kabla hata hajaianza hiyo ndoa, fikra za TARAKA hua zinamkaa; i think unae muoa HUJAMPENDA, unataka tu kuoa but there is NO LOVE, sijui kwanini pia umuoe mwanamke usiempenda! Anyway, bado najifunza.
Jambo moja ninalo kubaliana na wewe ni kuhusu kuweka gharama kubwa kuliko uwezo wa wahusika, hili hata mimi nalipinga, linachelewesha vinaja wengi kuanza maisha, linasababisha hata mabinti kua na mtazamo usio rasmi, kwamba ndoa yangu ivunje record ya ndoa ya fulani, that is stupid, hapa nakubaliana na wewe kabisa.