Haiwezekani Mtumishi wa Serikali umiliki gari ya milioni 60, halafu unaendelea kuwa mtumishi

Haiwezekani Mtumishi wa Serikali umiliki gari ya milioni 60, halafu unaendelea kuwa mtumishi

Wakuu habari.

Msiseme naingilia maisha ya mtu. Hivi kweli Mtumishi wa serikali unamiliki gari ya milioni 60 na kuendelea, bado unataka kuwa Mtumishi.

Huo ni mtaji tosha, achia kiti wengine waajiriwe, ukafanye maisha mengine
Hatuwi watumishi wa Umma kwa sababu tunatafuta Mitaji au kwa sababu tuna shida ya Fedha...

tunatumika kwa sababu kuna Maarifa na Hekima Ambayo Mungu ameweka ndani yetu na tunapaswa kuitumia kwa uaminifu kuijenga nchi Yetu...

Ni hatari sana kutumika kwa sababu una shida ya kipato...kwa maana siku usipolipwa utakuwa tayari hata kuiba ili upate kipato..

Mshahara unaopewa ni mbegu kwa ajili ya kuwekeza ili ufanikiwe zaidi.
 
Wanajeshi Mimi sio mjeda Ila naweza kopa 40m kuanzia mwaka huu baada ya maza kutupandisha!tulia tu dogo
Umepanga nyumba, watoto 3 wapo private school, mchepuko hapohapo, maisha kwa ujumla kabla hujakopa mshahara hautoshi sasa jichanganye kanunue gari.

Gari litahitaji service na mafuta na wakati haliingizi kitu, majukumu ya hapo juu yapo palepale na mshahara umeupunguza hapo utakuta jirani yako analisubiri hilo gari uliuze kwa bei ya hasara hivyo kama umenunua gari nawe ni mjasiliamali hapo sawa ila kama mtumishi sasahivi utalipaki unasubiria daladala na ukiwa ofisini hata kikao cha 10000 hukaimishi mtu
 
Wakuu habari.

Msiseme naingilia maisha ya mtu. Hivi kweli Mtumishi wa serikali unamiliki gari ya milioni 60 na kuendelea, bado unataka kuwa Mtumishi.

Huo ni mtaji tosha, achia kiti wengine waajiriwe, ukafanye maisha mengine
Acha njaa
 
Kwa mshahara upi ukope hiyo hela. Hata iwe miaka kumi, halafu ubaki na kipi, ulNilit.
Na mimi nilitaka kushaangaa yaani ukope mil 60 mtumishi wa umma halafu ubaki na one third (theluthi moja) ya kula na kusomesha watoto? Daaah life is not fair
 
Wakuu habari.

Msiseme naingilia maisha ya mtu. Hivi kweli Mtumishi wa serikali unamiliki gari ya milioni 60 na kuendelea, bado unataka kuwa Mtumishi.

Huo ni mtaji tosha, achia kiti wengine waajiriwe, ukafanye maisha mengine
Kama kukopa kupitia kazi yake vipi, kwanini aache kazi iliyomfanya aipate hiyo gari!!?
 
Watu wana miradi inawanunulia magari na kuwajengea nyumba na hiyo miradi wala sio mikubwa sana, changamka kijana acha kulia lia 60 milion sio pesa nyingi sana.
 
Uchizi hivi mnajua mtu anaelipwa M3.3-M5 wanaweza kukopa sh.ngapi, mnajua mafisadi wanaiba ngapi, mnajua kuna watu wana project zenye net balance mgao hadi 50M-100, au mgao wa 25*4 kwa project collective and personal.

Ambao mnavijisent mtulie tu muendelee kujamba milioni 60 pesa gani hio ya kashata tu hio
Mtumishi mwenye mradi wa kueleweka anaipata hiyo hela ndani ya mwaka tu huku akiendelea na maisha ya utumishi wake.
 
Ati kashata ya milioni 60 yaani sidhani kama hata Mo Dewji anaweza tamka hii sentensi lakini hapa kwakuwa hatuonani unakuta mbugila flani wa kwamtogole kapiga SHING'WAA au mzinga wa K Vant halafu anatishia watu humu kuwa 60 milion ni hela ya kashata
Million 60 ni parefu mno na ni mtaji wa kukutoa kimaisha kabisa
 
Ni tabia ya ku-save tu.

Kama unaweka benki angalau 500,000 kila mwezi kwa miaka 10 unanunua gari ya milioni 60.

Ila kama kila mwisho wa mwezi unataka uende mlimani city na watoto zako na wapwa zako sahau kumiliki japo baiskeli.
 
Wakuu habari.

Msiseme naingilia maisha ya mtu. Hivi kweli Mtumishi wa Serikali unamiliki gari ya milioni 60 na kuendelea, bado unataka kuwa Mtumishi.

Huo ni mtaji tosha, achia kiti wengine waajiriwe, ukafanye maisha mengine.
Maisha ni fumbo kijana,kuna vitu kuvielezea ni ngumu sana,ridhki ni kitu cha ajabu sana na kinatoka kwa mwenyezi mungu pekee.
Kama wewe unaweza kupata kwa mwezi 60,000/=,yupo anayeweza kupata mara 10,100,1000,10000 yake etc.
Endelea kuangalia fursa,kuzipigania na kuziomba,usiwe na wivu juu ya ridhki za wenzako hasa za halali.
 
Sijawa na wivu, nimeshauri Kama una uwezo huo, si Bora ujiajiri, upishe wengine wapate mitaji
 
Back
Top Bottom