kali linux
JF-Expert Member
- May 21, 2017
- 2,192
- 5,685
All roads lead to Taoism.Napenda Oriental philosophy, Lao Tzu, Confucius, Buddha, Mencius, Zhuang Zhou, Sun Tzu, Tao Te Ching nimesoma sana vitabu vyao.
Nadhani ndio maana nimekuwa enlightened
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
All roads lead to Taoism.Napenda Oriental philosophy, Lao Tzu, Confucius, Buddha, Mencius, Zhuang Zhou, Sun Tzu, Tao Te Ching nimesoma sana vitabu vyao.
Nadhani ndio maana nimekuwa enlightened
Uki sahihi lkn Hili sio jambo la kiroho hata kidogo. It's just a matter of common sense.Tatizo ni moja , mambo ya kiroho umejarbu kutumia akili kujustfy
Shetani yupo makka kwenye jiwe jeusi kule ndugu zetu wanaendaga kumpiga na mawe wanakanyagana hadi wanauana wao kwa wao,,,,na kumbukumbu za Yesu kristo zipo israel huko na vatican,,,Watakatifu ni wao weupe,,,,Manabii wale wawili ni wakwao watu weupe,,, sehemu takatifu zipo kwao,,,Malaika pia ni weupe!!Waafrika tuna shida asee!!!
Hamna common sense hapo jombaa lazima uchochore tuuUki sahihi lkn Hili sio jambo la kiroho hata kidogo. It's just a matter of common sense.
Tunajua tusicho kijua , hizi dini hizi😭.
✊✊🤣🤣🤣
Ila miaka inavyokwenda mambo yatabadilika Sana.
Yesu mwenyewe aliwahi kusema siku ukiujua ukweli utakuwa Huru.
HAIWEZEKANI MUNGU ASIMUUE SHETANI ALAFU AAMURU WATU WAUE WANAOFANYA MAMBO YA KISHETANI; HAIINGII AKILINI!
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
Kwenye nyumba za ibada tangu tukiwa Watoto tulifundishwa kuna Wahusika Wawili mahasimu, wakwanza anaitwa MUNGU na wapili anaitwa SHETANI.
Mhusika Mungu huyu tuliambiwa ndiye Muumbaji wa Mbingu na Nchi, na ndiye Baba yetu (Chanzo chetu). Huyu tukaambiwa pia ni Mwema, mwenye upendo, nguvu na uweza. Chanzo chake hatujaelezewa, na hata wanaotuelezea habari zake hawajawahi kumuona. Hii ni kumaanisha hawajui anafananaje.
Mhusika Shetani huyu amepewa uhusika mbaya Kwa kusemekana alimuasi Mhusika MUNGU, asili ya Shetani wapo waliosema ni Jamii ya Malaika waitwao Makerubi, ambaye jina lake ni Lucifer. Wakati wengine wakidai Shetani au Ibilisi asili yake ni Kutoka Koo za majinni. Hii ni kusema Shetani ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu. Ingawaje Stori hizi mbili hazijakamilika na zinaacha maswali mengi kuliko kilichoelezwa.
Lusifa kama aliasi, aliasi sheria ipi miongoni MWA sheria za Muumba wake huko Mbinguni?
Kabla hajaasi hiyo sheria ilitamka kuwa adhabu ya kuasi ni ipi?
Stori za Shetani zimeanzia juujuu na kuishia juujuu kama Stori za masela WA vijiweni. Yaani Stori imeanzia Kati na kuishi katikati.
Tukirudi kwenye Hoja.
Wasimulizi WA hizi dini zakuletwa na Waandishi wa vitabu vyao ambavyo vimeandika habari za huyo Mungu na Shetani Kwa uchache Mno, wakaja na sheria, ni kama sheria za biashara ya Market zile za Qnet. Unawekeza Kwa Imani pasipo kuuliza maswali yenye kufikiri, ATI hivyo ndio namna ya Kupata faida kwenye biashara.
Vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Shetani ndiye chanzo cha dhambi, inakazia zaidi kuwa kila dhambi ifanywayo na binadamu chanzo chake ni Shetani kwani Shetani ndiye anayeshawishi Watu au viumbe kufanya Uasi.
Ukisoma kwenye Quran au Biblia yapo Makosa MTU akifanya anatakiwa kuuawa kama adhabu.
Mfano WA Makosa hayo ni kama kuua, kuwa Shoga au msagaji, kulala na mnyama, kuzini na mama mzazi au Baba mzazi au mkwe au mtoto wako. Kumkufuru Mungu na kuwa mchawi au mshirikina. Na Makosa mengine mengi yenye kustahili adhabu ya kifo Kwa mujibu wa vitabu vya Dini.
Swali linakuja, Ikiwa mhusika Mungu wa kwenye vitabu hivyo vya Dini, aliamuru Watu kuwaua Watu wenzao wanaofanya Makosa au dhambi nzito kama zilivyotajwa, ni Kwa nini huyu Mungu asingeshughulika na Shetani mwenyewe ambaye ndiye anawafanya Watu WAUE, wawe mashoga, na kufanya zinaa chafu ya kiwango cha juu?
Kwa sababu kama kweli Mungu hakutaka Dunia iwe na uovu kama ni kweli Kabisa basi ni dhahiri angedili na chanzo ambacho vitabu vya Dini vinamtaja ni mhusika Shetani.
Haiingii akilini badala ya kumuua Shetani ambaye ndiye chanzo cha Watu kufanya uovu mkubwa, ATI uwaamuru hao Watu wawaue Watu wenzao wanaofanya Matendo ya kishetani yaani wanaomfuata Shetani ambaye wamezaliwa wamemkuta na watakufa watamuacha. Hakuna mantiki kabisa ya Jambo Hilo.
Nafikiri Vitabu vya Dini vinashindwa kueleza ukweli Kati ya huu;
1. Binadamu ndio Shetani wenyewe. Lakini wametafuta Shetani bandia asiyeonekana ili wamsingizie.
Hoja hii haina nguvu Kwa sababu Mwanadamu hawezi kupambana na Mungu au Shetani yaani hawezi kupambana na matamanio yake yaliyomo katika Akili yake. Kwani matamanio na utashi ndio humuongoza MTU.
2. Mungu na Shetani ni Mhusika mmoja. Yaani Mungu ndiye Shetani na Shetani ndiye huyohuyo Mungu.
Vitabu vya Dini vinashindwa kuelezea ukweli huu labda Kwa kuogopa kuyafanya Maisha yataonekana hayana maana. Jambo ambalo nikweli kuwa Maisha ni ubatili.
Kama Mungu ndiye muumba wa yote na muweza WA yote tafsiri yake Ipo wazi kabisa.
Hii ni kusema, Mungu hawezi kumuua Shetani Wakati yeye ndiye huyohuyo Shetani. Na Shetani hawezi kumuua Mungu Wakati yeye ndiye huyohuyo Mungu.
Hoja hii inanguvu Kwa sababu, hata vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Mungu aliumba Mema na Mabaya (ushetani) lakini akamwambia Mwanadamu achague Mema ili aweze kuishi.
Kumaanisha upande mzuri au Mwema wa Muumbaji wetu ndio wanadini waliuita Mungu na upande Mbaya wa Muumbaji wetu wakauita Shetani. Ni kama vile USO na kisogo ambavyo vyote vipo Kwa mhusika mmoja.
Haiwezekani Lusifa Awe Muasi hivihivi, lazima tujiulize huo Uasi ulitoka wapi ikiwa sio Kwa Muumbaji wake? Kwa sababu kiumbe hakina uwezo wa kuumba Jambo lolote liwe zuri au liwe Baya.
Taikon pumzika sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
😂 uwezo ndo asili ya kipawa chake yaani ndo maana hata tukisema material ya uumbaji wao ni asili ya moto wakati binadamu ni udongo.Mkuu inaeleza vizuri Kabisa.
Sasa tururdi kwenye swali la msingi.
Shetani vipawa vyake, nguvu zake, Akili zake, na kila Aina ya uwezo wake anautoa wapi?
😂 uwezo ndo asili ya kipawa chake yaani ndo maana hata tukisema material ya uumbaji wao ni asili ya moto wakati binadamu ni udongo.
Shetani wameumbwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi ya binadamu na wanaweza kumshawishi binadamu na binadamu ana akili ambaye anaanza kufikiria halafu ndo anatenda na binadamu huyo huyo anaweza kumkataa shetani kwa kutumia akili ...Huu ni uwezo pekee wa kila kiumbe .
Usifikirie hawa viumbe tunawachinja na kuwafuga ni kwamba hawa hawana uwezo dhidi ya binadamu hata wapewe maumbo makubwa kama nyangumi na Mungu amehalalisha wawe chini ya kiumbe mwanadamu na ulimwengu mzima kutumia akili mwanadamu atajua vyote vilivyopo pamoja na kuweza kuvicontrol...
Ndo maana ni haramu kumfananisha binadamu mwenzio kwa kumtusi jina la mnyama hata kumuita shetani kwani ni viumbe tofauti kama Mungu alivyoumba .
Sisi waislamu tuna sikukuu ya kuchinja si unaona hapa wanyama kama haki yao ya kuishi imedhalilishwa ili mwanadamu amle tu ...Hii ni kutokana na kipawa na heshima ya mwanadamu ipo juu dhidi ya wanyama.
The same shetani ana kipawa kikubwa kuliko mwanadamu kweny ushawishi except wanadamu amepewa akili ya kufikiria kabla ya kutenda..
UFUNUO 12:1-17
1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Mama mchungaji naomba uniache Kwanza.
Tupo kwenye Falsafa
Mungu kwani si alikuwa miongoni mwa malaika ambaye kafukuzwa peponi ...Kipawa kapewa na Nani? Hilo ndio swali langu.
Shetani sio chanzo, naye ameumbwa kama Mimi na Wewe.
Jibu utalipata soon
Alafu wanamuita Great thinker [emoji23]
Hujajibu swali huo uwezo WA shetani ameutoa wapi ?[emoji23] uwezo ndo asili ya kipawa chake yaani ndo maana hata tukisema material ya uumbaji wao ni asili ya moto wakati binadamu ni udongo.
Shetani wameumbwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi ya binadamu na wanaweza kumshawishi binadamu na binadamu ana akili ambaye anaanza kufikiria halafu ndo anatenda na binadamu huyo huyo anaweza kumkataa shetani kwa kutumia akili ...Huu ni uwezo pekee wa kila kiumbe .
Usifikirie hawa viumbe tunawachinja na kuwafuga ni kwamba hawa hawana uwezo dhidi ya binadamu hata wapewe maumbo makubwa kama nyangumi na Mungu amehalalisha wawe chini ya kiumbe mwanadamu na ulimwengu mzima kutumia akili mwanadamu atajua vyote vilivyopo pamoja na kuweza kuvicontrol...
Ndo maana ni haramu kumfananisha binadamu mwenzio kwa kumtusi jina la mnyama hata kumuita shetani kwani ni viumbe tofauti kama Mungu alivyoumba .
Sisi waislamu tuna sikukuu ya kuchinja si unaona hapa wanyama kama haki yao ya kuishi imedhalilishwa ili mwanadamu amle tu ...Hii ni kutokana na kipawa na heshima ya mwanadamu ipo juu dhidi ya wanyama.
The same shetani ana kipawa kikubwa kuliko mwanadamu kweny ushawishi except wanadamu amepewa akili ya kufikiria kabla ya kutenda..