Nimesoma vizuri uzi huu changamoto kwamba auna elimu ya koroho ila umesoma sana theory. Watu wengi wanaopinga uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba mbingu na nchi(Simaanishi wewe ila ni baadha ya watu) cha hajabu hao watu wengi ni madevil worshiped waabuduMashetani. Wanakataa uwepo wa Mungu lakini wanakubali uwepo wa shetani ambaye ndie baba yao.
Ukisoma Biblia kwa theory hasa Agano la kale utakuja kuona Mungu ni katili sana. Changamoto inakuja pale neno moja limetumika kwa maana tofauti tofauti kwenye biblia za kishwahili na kingeleza Tofauti ukisoma Biblia ya kiebrania utakuja kuona tofauti mkubwa sana hasa neno Mungu. Kwa asilimia kubwa agano la kale liliongozwa na malaika ndio walikuwa wakihitwa nano Mungu au Bwana,Yehofa au elohiym. Hata Musa mwenyewe hakukutana na Mungu bali alikutana na Malaika uso kwa uso.
Agano jipya kwa njia ya Yesu Kristo ndio aliyekuja kumfunua Mungu halisi katika tabia zake. Ndio maana ukisoma Agano jipya unakuja kuona Mungu ambaye siye katili na ni tofauti wa agano la kale katika Tabia ambazo kristo Yesu alivomfunua.
Tunaposema Yesu atumaanishi mwili bali ni roho ya Mungu iliyokuja kuvaa mwili wa kinadamu kwaiyo aijalishi angekuwa mweusi au mweupe lakini utabaki kua ni mwili tu.
Tunaposema Mungu ni Mungu mwenye haki wala yeye sio kigeugeu wala ajipingi wala kubadilika. Sio Mungu aliyluhusu watu wauwane au watu wawauwe wale wanaompinga yeye na kumkubali shetani.
Mungu aliwaumba wanyama na malaika pamoja na mbingu na nchi kwa ajiri ya kumiliki na kutawala binadamu only. Malaika aitwae Lucifer kabla ajawa shetani alikuwa ni malaika mwema tu aliyemfanya Mungu kwa ajiri ya kumtumikia binadamu lakini kwa utashi wa lusifa aliasi yaani alitoka kwenye nafasi yake ya kutumika kwa wanadamu bali yeye ndio alitamani atumikiwe na viumbe vingine kitu ambacho akiwezekani.
Binadamu pekee ndio aliyepewa uwezo mkubwa wa akili kuliko viumbe vyote. Ndiomaana hao malaika walioasi yaani walioacha wajibu wao wa kumlinda binadamu wanatumia hila kumlubuni binadamu lakini kiukweli hata hao waabudu mashetani ni wajinga na wapumbavu sanaaana wanawaabudu wafanya kazi wao.
Shetani anauwezo wa kutoa utajiri isipokuwa anatumia uwezo wa mwanadamu uwo uwo kukutengenezea wewe utajiri.
Kwaiyo ndugu mtoa uzi tafuta biblia na tafsiri za kiebrania, kiyunani na kigiriki ndio utakuja kupata majibu kamili.
Sent from my SM-A105F using
JamiiForums mobile app