Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini


🤣🤣🤣
Ila miaka inavyokwenda mambo yatabadilika Sana.
Yesu mwenyewe aliwahi kusema siku ukiujua ukweli utakuwa Huru.
 


UFUNUO 12:1-17
1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake.
5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.
16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
 
Mkuu inaeleza vizuri Kabisa.
Sasa tururdi kwenye swali la msingi.
Shetani vipawa vyake, nguvu zake, Akili zake, na kila Aina ya uwezo wake anautoa wapi?
😂 uwezo ndo asili ya kipawa chake yaani ndo maana hata tukisema material ya uumbaji wao ni asili ya moto wakati binadamu ni udongo.

Shetani wameumbwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi ya binadamu na wanaweza kumshawishi binadamu na binadamu ana akili ambaye anaanza kufikiria halafu ndo anatenda na binadamu huyo huyo anaweza kumkataa shetani kwa kutumia akili ...Huu ni uwezo pekee wa kila kiumbe .


Usifikirie hawa viumbe tunawachinja na kuwafuga ni kwamba hawa hawana uwezo dhidi ya binadamu hata wapewe maumbo makubwa kama nyangumi na Mungu amehalalisha wawe chini ya kiumbe mwanadamu na ulimwengu mzima kutumia akili mwanadamu atajua vyote vilivyopo pamoja na kuweza kuvicontrol...

Ndo maana ni haramu kumfananisha binadamu mwenzio kwa kumtusi jina la mnyama hata kumuita shetani kwani ni viumbe tofauti kama Mungu alivyoumba .


Sisi waislamu tuna sikukuu ya kuchinja si unaona hapa wanyama kama haki yao ya kuishi imedhalilishwa ili mwanadamu amle tu ...Hii ni kutokana na kipawa na heshima ya mwanadamu ipo juu dhidi ya wanyama.


The same shetani ana kipawa kikubwa kuliko mwanadamu kweny ushawishi except wanadamu amepewa akili ya kufikiria kabla ya kutenda..
 

Kipawa kapewa na Nani? Hilo ndio swali langu.
Shetani sio chanzo, naye ameumbwa kama Mimi na Wewe.
 

Mama mchungaji naomba uniache Kwanza.
Tupo kwenye Falsafa
 
Mama mchungaji naomba uniache Kwanza.
Tupo kwenye Falsafa

Haya mambo ya rohoni yanasumbua sana
Ila ijulikane kwamba mambo yote yawe mema au mabaya huanzia rohoni

Nimekuacha kwa muda ila nitakua karibu nafuatilia😅😅😅
 
Kipawa kapewa na Nani? Hilo ndio swali langu.
Shetani sio chanzo, naye ameumbwa kama Mimi na Wewe.
Mungu kwani si alikuwa miongoni mwa malaika ambaye kafukuzwa peponi ...
Mungu hakuwa na shaka juu ya ushawishi wa shetani kwani binadamu alimpa akili kubwa anaweza kumpinga shetani ..

Mbona hata sisi tumehalalishiwa kuchinja wanyama na kula kwa vile tuna kiwapa zaidi yao kwani wao hawataki kuishi?
 
Mambo ya kiroho ni magumu sana ndugu.Mungu yupo na shetan yupo .Cha msingi mtafute Mungu
 
Hujajibu swali huo uwezo WA shetani ameutoa wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…