Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Hiyo ni law ya Energy conservation.
Hata hivyo inarejelea hoja ileile kuwa Roho huwezi kuiumba wala huwezi kuiharibu Kwa sababu Roho ni energy haifi wala haitengenezwi.

Nafsi umekumbwa Ila Roho haijaumbwa.

Bado hauelewi kuwa Roho ni nishati
Wewe nimekuuliza habari za roho umezitoa wapi?
 
Vitu vyote viliumbwa na Mungu
 
Soma Biblia kijana acha Blah blah.

Biblia ina majibu yote.

Tatizo hamtaki kusoma Biblia ila mnakimblia kuandika blah blah tu
Tuwekee hapa jukwaani hizo verse zinazojibu hoja kuntu zilizoletwa mwana Fasihi bila kuacha chembe ya mashaka. Usipozileta wewe ndo mwana bla blaa.
 
Robert unasema Roho haina utambuzi, unazungumziaje maandiko ya biblia yanaposema Mungu ni Roho wakati Roho haina utambuzi
 
Mkuu acha kusema hivo nakuomba 🙏 unafanya kufuru mbaya Sana!
Shetani anatoa wapi nguvu na utajiri?

Jibu lako ndio litahitimisha mada Hii kuwa Muumbaji ndiye huyohuyo Mungu na Shetani katika uhusika mbili tofauti ndani ya mhusika mmoja
 
Mungu ndio shetani acha kupoteza muda na hataweza kumuua shetani kwakuwa ndio yeye mwenyewe hivyo haiwezi jiua maana mambo ya dunia anapanga mungu conclusion mungu ndio shetani mwenywe 😁😁
 
Unaamini haya mambo mkui
Kama mungua alijua shetani ataasi why alimuumba, na kama aliasi why alimuua yesu badala ya kumuua shetani
 
Embu Anza na niliyemnukuu Huko juu, yeye ndiye kasema Shetani anavipawa, ndio nikamuambia hivyo vipawa alivyonavyo huyo Shetani kavitolea wapi kama sio Kwa muumba wake.

Ukikuta mjadala, jitahidi utafute ulipoanzia sio kudandia juu Kwa juu.
Kipawa cha shetan ni kuimba hayo mambo mengine umeongeza wewe kwa utashi wako
 
Wewe unaweza kutengeneza roboti alafu ukalipa mtihani kisha roboti likifeli unaliadhibu. Wakati huohuo unajua matokeo kuwa litafeli au litafaulu.

Hiyo kitu inakuingia akilini kweli?
Kwa akili yako unazan Mungu atawaza sawasawa na wewe mwanadamu hapa umeonyesha jinsi gani ulivyokua haya mambo huyajui

Kiongozi akiwa anafikiri sawasawa na anawaongoza huyo hafai kuwa kiongozi njia za Mungu anazotumia always zinamuacha binadamu kwenye dilemma
Unataka Mungu afikiri sawasawa na wewe utasubiri sana
 
Hii ni komenti Bora kabisa
Ubora wake ni upi
Kwakukusaidia
Kwa akili yako unazan Mungu atawaza sawasawa na wewe mwanadamu hapa umeonyesha jinsi gani ulivyokua haya mambo huyajui

Kiongozi akiwa anafikiri sawasawa na anawaongoza huyo hafai kuwa kiongozi njia za Mungu anazotumia always zinamuacha binadamu kwenye dilemma
Unataka Mungu afikiri sawasawa na wewe kuna haja gani ya yeye kuwa Mungu
 
Kumbukumbu la Torati 29:29 Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele,..."na ndio maana mambo mengine hayawezi kukuingia akilini
 
Umejuaje kwamba hawazi sawasawa na kundi lake?

Ikiwa viongozi wametokana na jamii hiyo hiyo?
 

Mungu sio Kiongozi.
Mungu Muumbaji hapati chochote Kutokana na maamuzi yako. Maamuzi yako hayamuumizi Kwa chochote.

Mwanadamu ni mfano WA Mungu, vile ujionavyo ndivyo Mungu alivyo, Ila vile alivyo Mungu sivyo tulivyo sisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…