Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Nafsi ni kiungo kati ya roho ya mtu na mwili wake,wewe unapata taarifa kutoka ulimwengu wa roho Kwa roho yako nafsi inakuwa daraja au kiungo kuzileta mwilini

Nafsi sio kiungo nawe. Acha Uongo.
Roho ni nishati, ni nguvu inayofanya kiumbe Aishi na afanye shughuli Fulani.
 
Roho yenyewe ni sehemu ya ndani ya utu wa mtu ,inahusika na mambo yafuatyo
Ibada ama worship
Hisia za rohoni
Ushirika
Dhamiri
Kupata taarifa kutoka ulimwengu wa Roho,Mungu anakutana na kutambulikana na watu kupitia Roho zao
 
Nafsi hai na Nafsi mfu.
Ili Nafsi iwe hai itahitaji Nishati iitwayo Roho.
Nishati ikitoka Nafsi inakuwa mfu.

Ukisikia MTU akisema Roho ya Mungu I juu yangu anamaanisha nguvu au Nishati ya Mungu Ipo katika Nafsi yake(software yake)

Sasa kuna mwili Kufa na Nafsi Kufa.
Kwenye computer hardware inaweza kids lakini software ikawa hai.
Computer tuna CPU hii ni ,
Lakini pia tuna operating software lakini pia tuna hardware component zingine
 
Haipo Kwa sababu haiwezi kuthibitika, Ila kifalsafa ipo.
Tafuta wanafalsafa wakubwa unaowajua watakuambia Roho ni nishati au nguvu inayompa kiumbe uhai.
Unaweza ku-google pia kama haukusoma Philosophy.
Uliza tuu spirit ni nini? Watakuletea
Hao wanafalsafa ni wapuuzi tuu,umeweza kuwaamini lakini umeshindwa kuniamini mimi
 
Haipo Kwa sababu haiwezi kuthibitika, Ila kifalsafa ipo.
Tafuta wanafalsafa wakubwa unaowajua watakuambia Roho ni nishati au nguvu inayompa kiumbe uhai.
Unaweza ku-google pia kama haukusoma Philosophy.
Uliza tuu spirit ni nini? Watakuletea
Hao wanafalsafa ni wapuuzi tuu,umeweza kuwaamini lakini umeshindwa kuniamini
 
Energy haziwezi kuwa na hisia ama kuzungumza,spirit beings zipo zinaongea,zinfanya kazi,zinahisi
 
Hiyo ya chini sikuungi mkono inakuja unakataa kukaa kichwani.

Kusema Mungu ndiye shetan and vice versa ni kufuru bro.

Mungu hawez kuwa shetan kwasababu wewe mwenyewe umethibitisha Mungu alimuumba shetani... Hivyo haiwezekan mtu kujitengeneza chenyewe mfano.

Mwalimu anatengeneza Daktar ambapo daktar atabaki daktar na mwalimu atabaki mwalimu
In fact hajailewa logic hapo
 
Roho ni zaidi ya nishati ,ni uhalisia ya uwepo wao katika ulimwengu wao
 
HAIWEZEKANI MUNGU ASIMUUE SHETANI ALAFU AAMURU WATU WAUE WANAOFANYA MAMBO YA KISHETANI; HAIINGII AKILINI!

Anaandika, Robert Heriel
Kuhani

Kwenye nyumba za ibada tangu tukiwa Watoto tulifundishwa kuna Wahusika Wawili mahasimu, wakwanza anaitwa MUNGU na wapili anaitwa SHETANI.

Mhusika Mungu huyu tuliambiwa ndiye Muumbaji wa Mbingu na Nchi, na ndiye Baba yetu (Chanzo chetu). Huyu tukaambiwa pia ni Mwema, mwenye upendo, nguvu na uweza. Chanzo chake hatujaelezewa, na hata wanaotuelezea habari zake hawajawahi kumuona. Hii ni kumaanisha hawajui anafananaje.

Mhusika Shetani huyu amepewa uhusika mbaya Kwa kusemekana alimuasi Mhusika MUNGU, asili ya Shetani wapo waliosema ni Jamii ya Malaika waitwao Makerubi, ambaye jina lake ni Lucifer. Wakati wengine wakidai Shetani au Ibilisi asili yake ni Kutoka Koo za majinni. Hii ni kusema Shetani ni kiumbe kilichoumbwa na Mungu. Ingawaje Stori hizi mbili hazijakamilika na zinaacha maswali mengi kuliko kilichoelezwa.

Lusifa kama aliasi, aliasi sheria ipi miongoni MWA sheria za Muumba wake huko Mbinguni?

Kabla hajaasi hiyo sheria ilitamka kuwa adhabu ya kuasi ni ipi?

Stori za Shetani zimeanzia juujuu na kuishia juujuu kama Stori za masela WA vijiweni. Yaani Stori imeanzia Kati na kuishi katikati.

Tukirudi kwenye Hoja.
Wasimulizi WA hizi dini zakuletwa na Waandishi wa vitabu vyao ambavyo vimeandika habari za huyo Mungu na Shetani Kwa uchache Mno, wakaja na sheria, ni kama sheria za biashara ya Market zile za Qnet. Unawekeza Kwa Imani pasipo kuuliza maswali yenye kufikiri, ATI hivyo ndio namna ya Kupata faida kwenye biashara.

Vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Shetani ndiye chanzo cha dhambi, inakazia zaidi kuwa kila dhambi ifanywayo na binadamu chanzo chake ni Shetani kwani Shetani ndiye anayeshawishi Watu au viumbe kufanya Uasi.

Ukisoma kwenye Quran au Biblia yapo Makosa MTU akifanya anatakiwa kuuawa kama adhabu.
Mfano WA Makosa hayo ni kama kuua, kuwa Shoga au msagaji, kulala na mnyama, kuzini na mama mzazi au Baba mzazi au mkwe au mtoto wako. Kumkufuru Mungu na kuwa mchawi au mshirikina. Na Makosa mengine mengi yenye kustahili adhabu ya kifo Kwa mujibu wa vitabu vya Dini.

Swali linakuja, Ikiwa mhusika Mungu wa kwenye vitabu hivyo vya Dini, aliamuru Watu kuwaua Watu wenzao wanaofanya Makosa au dhambi nzito kama zilivyotajwa, ni Kwa nini huyu Mungu asingeshughulika na Shetani mwenyewe ambaye ndiye anawafanya Watu WAUE, wawe mashoga, na kufanya zinaa chafu ya kiwango cha juu?

Kwa sababu kama kweli Mungu hakutaka Dunia iwe na uovu kama ni kweli Kabisa basi ni dhahiri angedili na chanzo ambacho vitabu vya Dini vinamtaja ni mhusika Shetani.

Haiingii akilini badala ya kumuua Shetani ambaye ndiye chanzo cha Watu kufanya uovu mkubwa, ATI uwaamuru hao Watu wawaue Watu wenzao wanaofanya Matendo ya kishetani yaani wanaomfuata Shetani ambaye wamezaliwa wamemkuta na watakufa watamuacha. Hakuna mantiki kabisa ya Jambo Hilo.

Nafikiri Vitabu vya Dini vinashindwa kueleza ukweli Kati ya huu;
1. Binadamu ndio Shetani wenyewe. Lakini wametafuta Shetani bandia asiyeonekana ili wamsingizie.
Hoja hii haina nguvu Kwa sababu Mwanadamu hawezi kupambana na Mungu au Shetani yaani hawezi kupambana na matamanio yake yaliyomo katika Akili yake. Kwani matamanio na utashi ndio humuongoza MTU.

2. Mungu na Shetani ni Mhusika mmoja. Yaani Mungu ndiye Shetani na Shetani ndiye huyohuyo Mungu.
Vitabu vya Dini vinashindwa kuelezea ukweli huu labda Kwa kuogopa kuyafanya Maisha yataonekana hayana maana. Jambo ambalo nikweli kuwa Maisha ni ubatili.

Kama Mungu ndiye muumba wa yote na muweza WA yote tafsiri yake Ipo wazi kabisa.
Hii ni kusema, Mungu hawezi kumuua Shetani Wakati yeye ndiye huyohuyo Shetani. Na Shetani hawezi kumuua Mungu Wakati yeye ndiye huyohuyo Mungu.

Hoja hii inanguvu Kwa sababu, hata vitabu vya Dini vinaeleza kuwa Mungu aliumba Mema na Mabaya (ushetani) lakini akamwambia Mwanadamu achague Mema ili aweze kuishi.

Kumaanisha upande mzuri au Mwema wa Muumbaji wetu ndio wanadini waliuita Mungu na upande Mbaya wa Muumbaji wetu wakauita Shetani. Ni kama vile USO na kisogo ambavyo vyote vipo Kwa mhusika mmoja.

Haiwezekani Lusifa Awe Muasi hivihivi, lazima tujiulize huo Uasi ulitoka wapi ikiwa sio Kwa Muumbaji wake? Kwa sababu kiumbe hakina uwezo wa kuumba Jambo lolote liwe zuri au liwe Baya.

Taikon pumzika sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Aisee
 
Hao wanafalsafa ni wapuuzi tuu,umeweza kuwaamini lakini umeshindwa kuniamini mimi

Kwenye falsafa hatuamini Ila tunatumia Logic/mantiki kukubali au kukataa Jambo Fulani.

Huwezi Kuta Roho ndio utu wa Mwanadamu Wakati huohuo hata kuku na mbuzi wanaroho(Nishati ya uhai).

Ikiwa umekubali Mwanadamu amegawanyika katika sehemu tatu ukaazifaja kuwa ni Mwili, Nafsi na Roho
Hata tuambie Kuku au hata kagawanyika katika sehemu ngapi?
 
Soma Biblia kijana acha Blah blah.

Biblia ina majibu yote.

Tatizo hamtaki kusoma Biblia ila mnakimblia kuandika blah blah tu
Biblia inajibu hayo kweli au wewe umelaza ubongo unampenda kurahisisha mambo kwa kujifanya kupata majibu kwa kitabu cha wenzako?
 
Back
Top Bottom