Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) leo imetoa maamuzi kuhusiana na sekretarieti kufungua kesi katika kamati hiyo dhidi ya afisa habari wa Yanga Haji Manara.

Kamati ya maadili ya TFF imemkuta na hatia Haji Manara na kumfungia miaka miwili kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi na faini ya Tsh milioni 20 kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF Wallace Karia

Haji Manara alipishana kauli ya Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia katika eneo la VVIP wakati wa mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GENTAMYCINE je ni ya kweli haya ???
Nilipoanzisha Uzi mapema leo nikiwa na uhakika wa 100% kuwa Haji Manara atahukumiwa Kifungo ( Mvua ) Wapumbavu kama akina sky soldier walinipinga na kuna wengine walitamani isiwe kama nilivyotabiri ili waje Wanishambulie na Wanicheke kuwa nimechemka.

MImi ndiyo GENTAMYCINE 'Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer' JamiiForums nzima na nimebarikiwa vingi na Mwenyezi Mungu.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa Tunu.
 
Wanayanga tuungane tumlipie Manara hii faini aliyotozwa na TFF!
Manara amekuwa mtu mwenye mapenzi mema na timu yetu ametutetea sana, na hata hiki kifungo alichopata ni kwa sababu ya mapenzi yake mema na Club yetu!
Hivyo tupitishe bakuli ndani ya siku chache million 20 tunapata, inalipwa!
Wengine nadhani wana wazo la kukata rufaa, sishauri rufaa kwa sababu ni bora apumzike tu ili akitoka kwenye kifungo awe na adabu pia!
Ila wanayanga tumsuport kwa kumlipia faini kama kumuonyesha fadhila, na pia tuwaombe wanasimba waliokuwa wakimpenda watusaidie katika hili!
Nawasilisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…