Haji Manara amtolea uvivu Feitoto kwa kuomba pesa

Haji Manara amtolea uvivu Feitoto kwa kuomba pesa

Manara Si kafungiwa na TFF kujihusisha na chochote Kile kinachohusu soka.

Mnijuze
imekuaje Tena anaongelea hili suala?[emoji848]
 
Wengi wameniuliza maswali kama haya.

Na pindi napowajibu ndio hapo ambapo wewe unaanza kuniona mimi kama nina maslahi na hii kesi kwasababu nipo interested sana...
Haujajibu swali langu mkuu
 
Hii ajira mpya inayioitwa u chawa ni kazi moja ya laana sana unatumika Kama mbwa wa boss kubweka kwa kila anaemkaribia anaekufuga

huku ukijidai una umuhimu sana kwenye taasisi ya boss kumbe huna kazi yoyote zaidi ya kelele na hata akikuondoa hakuna pengo lolote kwake.
 
images (4).jpeg
 
Katika wote hao anayekera zaidi ni Jemedari bin Kazumari (the voice of voiceless)... 🤣🤣 yule jamaa huwa mada zake ni za upotoshaji mtupu ikiambatana na roho mbaya. Nadhani ni mtu ambaye hata Manara huwa anazima fegi. Huyo jomba ni mbishi Laana...
 
Post yake ina coments elf 13 ila kusema ukweli hakuna asiyeona uwezo mdogo wa kufikiri kwa Fei
 
Huyu jamaa kila kitu lazima atie neno hawezagi kukaa kimya ndio maana alitaka kuita mpaka press ya kutaka kumjibu mke wake wakubwa waka mkanya manara anajifanyaga much know sana.
 
Yuko sahihi kabisa Ingawa katumia maneno makali sana

Feisal Ni mpuuzi tu angeacha yanga wacheze kwanza huwa anaibuka muda yanga anacheza mechi za kimataifa Ni upuuzi na utoto
Lakin mbona Yanga ndio imeanza Kwa kumuita kamati ya nidhamu kwanini wasingesubiri mechi zipite ndio yaje mambo ya kuitana kamati ya nidhamu. Au Yanga kupiga hatua mbele Kwa fei kipindi hiki ni sawa na fei kupiga hatua sio sawa. Naona Yanga kama timu wangetulia finali zipite ndio waanze kumuita kamati ya nidhamu
 
Ndio mkuu ila Hajafungiwa kutumia mitandao ya kijamii mkuu.
Unajua huyu Manara anajaribu kutaka kutuaminisha yeye ana u chungu sana na Yanga wakati kiuhalisia yupo pale kama chawa wa Gsm
Manara yupo kimaslahi pale yanga,
Moyo wake uko Simba dam dam yule [emoji4]
 
Yeye kuchangisha pesa na mechi inayowakabili hujuma iko wapi? Hakuna uhusiano wowote...Nyie andaeni timu ishinde..
Yes, ni mtu mjinga pekee ndo ataamini maneno ya insta yanaweza kugharimu watu zaidi ya 50 kwenye timu. Ni kutafufa kiki tu. And he says kwamba wakipata ubingwa hata pata medali as if jamaa ni mwenye maamuzi ndani ya yanga.
 
Akimtolea uvivu Feisal Salum baada ya kiungo huyo wa Yanga SC kuomba kuchangiwa pesa kwa ajili ya kulipia gharama za kufungua jalada la kesi kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) Ni aibu kubwa kwa Nchi ni fadhaa na kulikosea Taifa hili, Kwa mara nyingine tena Fesal Salum anashiriki kuihujumu Yanga Waziwazi bila haya.

Tupo karibu kabisa na finali kubwa mbele yetu,Rais Wa Nchi yupo busy mara kwa mara kuhamasisha watanzania, Bunge kupitia Waziri Mkuu wanahamasisha, Wakuu wa mikoa ndio kama mnavyosikia.Kisha anatokea Binadamu anaepotoshwa na Watu wale wale kila tunapokaribia mechi kubwa kutuletea mjadala wa jambo lake binafsi lisilokuwa na chembe ya maslahi ya Taifa kutuletea choko choko.

Hivi hii sio hujuma ya kusudi kwetu na kwa nchi? Mawakili wake,Mameneja wake na hata Radio zinazopush agenda yake kipindi hiki tukisema wanatuhujumu kusudi tutakuwa tunakosea?Kwanza anachangisha nini wakati majuzi tu kaleta Milioni Mia ya kuvunja mkataba?

Kwa nn asichukue ile Vits Ya Dalali wake akauza ili aende CAS?Fesal unaendelea kutengeneza ufa ndani ya mioyo ya wengi, Yanga hii unayotafuta huruma mitandaoni ndio iliyokulea na kukupa jina unalosafiria nalo hivi sasa, Yanga hii hii ndio ilipokufanya uwe na hilo jina ambalo hao wanaokudanganya leo walikujulia hapa.

Mbaya zaid Mchambuzi mpumbav yule yule toka Radio ile ile yupo front kuendelea kukupotosha, Taifa linasulubiwa kwa sababu yako Fei, Nchi ipo katika vita ya ubingwa,wew unashiriki vita yako ya huruma za kinafik.Unasema eti mama yako alitukanwa, yy na Yanga nani kamtusi mwenzie?

Kutwambia ulikuwa unakula Ugali na Sukari sio matusi na dhihaka kwetu,Ni kweli mara nyingi umekuwa unatufanyia hv kila tunapokaribia mechi kubwa, lakini kwa mechi hii nathubutu kumwambia wazi wazi ww ni Mhujumu unaetumika bila kujijua,Ww ni Msaliti, Ww sio Muungwana hata chembe, unaihujumu Yanga na unawahujumu Wachezaji wenzio mlioishi naoWhy usisubiri mechi iishe? Why iwe leo?

Na kwa nn kila mechi yetu kubwa unarudia drama zako?Tushinde tushindwe hupati hata medali moja, mjinga sana ww Mtoto, unafanya hvyo kwa maslahi gani? Yanga imekukosea nn cha Ziada hadi uwe unatufanyia hvyo na huyo Shankupe wako muuza na nywele za maiti?Umetutafuta mara nyingi lakini hii ni too much, hujali kabisa kuhusu heshma ya nchi yako kisha eti unataja Team za Taifa! Zipi hzo wakati ww unahujumu maslahi ya Taifa kusudi.

Jemedari Said Kazumari mbwiga wa mbwiga ndo steering wheel wake.
 
kama kufungwa mtafungwa tu.muacheni adai haki yake.msitafute sababu.
 
Back
Top Bottom