Haji Manara amtuhumu Barbara kuwa na chuki dhidi yake. Amuahidi ataondoka Simba kwani amemkuta

Manara hafai kuwa msemaji wa Simba kwanza hajuwi mpira na hana akili. Yule ilibidi awe mwuimbaji bongo fleva tu au taarab maana hata singeli na muziki wa dansi hauwezi.
 
Manara hawezi kuendana na Simba ya sasa,sijawahi kumkubali ,kwenye uhamasishaji sawa lakini ana uswahili mwingi,Bidada amesimama kama CEO kwenye nafasi yake na kaachiwa asimamie mambo mengi kiasi kwamba hata mambo ya media yachujwe ndo Manara aongee ,Sasa manara hataki hivo anataka kila kitu awe wa kwanza .

Kwanza hata kama we ni Mo ingekuwa ngumu kumvulia Manara na matangazo yake ,amekuwa balozi wa karibia washindani wote Mo kibiashara. ASAS yeye ,GSM yeye ,Azam media yeye. Boss anakulipa halafu we una promote bidhaa za washindani wake ? Manara anawasifu GSM ila anawakejeli Yanga ,yeye hajui hata huo umaarufu amepata kupitia Simba hamna ambaye angemfahamu,atapiga kelele week nzima atasahaulika Simba itaendelea
 
Simba bingwa FA kilichowakuta yanga nusu fainali ya FA ndicho kitakachowakuta fainali, simba na yanga mechi zao zinachezwa sana nje ya uwanja

Hii mechi wanayanga wanamatumaini makubwa sana ya kupata ushindi, wamewafunga simba Mapinduzi na kwenye ligi pia, asikuambie mtu wanachokifanyaga simba caf champions leage ndicho walichokifanya kuelekea mechi hii ni kufuru. Kwa faida tu fuatilieni huyo mwamuzi wa hiyo mechi, nasema ivi hawatoki kivyovyote vile.
 
Manara amefanya kosa sana kuanzisha ugomvi sasa hivi.

Kwa nini asingesubiri mechi ijayo iishe kwanza?
Manara ni tatizo kubwa na aondoke tu
 
Hizi huu sio mpango wa CCM kututoa kwenye reli? Au sio mpango wa Simba kutaka kuichanganya Yanga kisaikologia?

Nitarudi Tena nione Kama ni ugomvi kweli
 
Atukua na shaka nayo tulikua na penati mbili ambazo zingekua magoli ila refa nae ni mwanadamu alipitiwa.
Ila Kigoma kitaeleweka tu mtani mtakaa mtake msitake.
Wana Simba wamechungulia wakaona tarehe 25 hawatoki, sasa wanatengeneza mlango wa kutokea. Nashukuru chuo cha Sanaa Bagamoyo kina wahitimu wengi.
 
Nilipenda san hamasa zake. Lakini tatizo la watanzania mafanikio kidogo anajiona ana uwezo sawa au kuliko taasisi. Haji amekuwa kama limbukeni wa umaarufu. Nadhani muda wa kutafuta changamoto sehemu zingine ni sasa.

Ni kama anataka awe untouchable hivi, yeye nani asiguswe au kuhojiwa? Kama mwajiriwa na binaadam huwezi kuwa sawa muda wote. Kuna muda utatoka nje ya mstari mwajiri lazima afanye wajibu wake.

Akiguswa anapeleka taarabu insta,anakuwa kama mwanamke mwenye kiranga, kifinyo kidogo tu mtaa mzima anajua. Mdomo mwingi huponza kichwa. Akibaki bila Simba akili itamrudia
 
Kikweli sijui undani wa sakata hii ila Haji amechoka, apumzike aje mtu mwingine mwenye uwezo zaidi. Ile press ya kabla ya game na Yanga ni ujinga mtupu alikuwa anaongea.

Unajiuliza hiki ndio ametumwa na klabu? au anajiropokea tu yeye. Simba wamemchoka Haji kitambo sana ila walikuwa wanamlia timing tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…