Haji Manara amtuhumu Barbara kuwa na chuki dhidi yake. Amuahidi ataondoka Simba kwani amemkuta

Jamaa mswahili sana atambue Simba ni kubwa kuliko yeye aondoke tu atuachie club yetu
 
Reactions: mmh
Wenyewe wanajiita ".......club kubwa.........club yenye uweledi wa hali ya juu.........club yenye hela......"

Sasa club yenye hela msemaji wao leo karopoka analipwa mshahara mia saba, ila akiwa kwenye press anavyotuna, ngano yenye amira inasubiri ,".......sisi tuna hela....😀😀😀😀😀😀😀😀"

Hapo sasa ndipo mnapoona IQ ya Manara, kwa club yenye uweledi jambo kama hili lisingefika kwenye social networks kwani linashusha hadhi ya club na uongozi mzima unaonekana hauna maana na ni wakipuuzi.

Sasa Manara naona anachambana na BEST WAKE Barbara, anashindana na mtoto wa kike.......ngojea tuangalie show dada CEO naye anaandaa MNYUKLIA WAKE.
 
Manara ameshajisahau kwamba yeye pale Simba au Nje ya Simba Hana lolote..Kupiga domo kila mtu anaweza....Kusema kwa Boss wako we Nani huo ni uswahili....Taasisi ina miiko na taratibu zake...Huwezi kumwambia Boss wako Koma..Na ndio mana sisi Watanzania hatuwezi kufanya kazi tuka excell vizuri kwenye international Level..

ujinga Kama Huu wa mipasho unakufanya wewe Haji utoe picha pana ya vijana wengi wa kitanzania...Nakuambia Haji Bila Simba wewe Ni Zero tena Minus Zero ..Sio lolote. SIMBA inakubeba wewe mana ni Taasisi wewe huna lolote...

NAWASHAURI simba baada ya Hii mfukuzeni Kazi huyu jamaa...Mpira sio ujinga ujinga wala sio siasa eti ukifukuzwa Chadema utaenda CCM....

MPIRA Ni tofauti sana. HUYU kajiona mkubwa kuliko Simba..Mfukuzeni Hana lolote..Kwanza Msemaji ndio nini???

Kule Al ahly mnamjua msemaji wao?? Je hawajachukua Ubingwa wa Afrika?? Kocha ndio anaongea kitalaamu sio bla bla...

Fukuza huyu mtu kazi mkimuacha mmeua team na atajiona mungu.
 
Haji Manara ni mshamba sana japo kila siku anajisifia kazaliwa kariakoo. Hajui taratibu za taasisi zinavyofanya kazi badala yake analeta uswahili kwenye mambo ya msingi kabisa. Ukiwa mfanyakazi wa taasisi yoyote ukizinguana na mwajiri au bosi wako mnamalizana huko huko ndani ya hiyo taasisi na mkishindwana mnaenda mahakama ya kazi mpaka mahakama ya rufaa huko. Sasa yeye anabwata bwata tu mitandaoni na kutisha watu huku anaomba huruma ya mashabiki aibu kubwa kwake kwa mtu anayejifanya mjuaji wa kila kitu.

Kwanza huyu ndiye afisa habari wa hovyo kabisa kuwahi kutokeaTanzania kwa sababu kila siku yeye ndiye anayeongoza kutukana na kutishia waandishi wa habari anaowaalika mwenyewe na wala huwa hajui kuwa anaharibu "brand" ya Simba na makampuni anayoyawakilisha kama balozi wa hayo makampuni. Pili muda wote yeye ni kuizungumizia na kuitukana Yanga wakati yeye kaajiriwa na Simba. Haji ni sawa tu yule shabiki wa Yanga aliyeibatiza jina la utopolo nawashangaa sana Simba kumpa hicho cheo na kumuacha nacho mpaka leo eti afisa habari wa timu. "Anyway" bodi ya Simba na Mo ndio wakulaumiwa jini wamelifuga wenyewe acha liwatafune kwani walitakiwa wawe wameshamfukuza siku nyingi sana.

Simba ni kubwa kuliko Haji Manara, Mo, Barbra, Kaduguda, Try Again na wengineo wote. Viongozi, wafadhili na wawekezaji wote watapita lakini Simba itadumu milele kwa hiyo mtu yoyote asijifanye eti yeye ni muhimu sana pale Simba.
 
Yan mnigga anaongeza kama chupi ..
Wanasutana Yan[emoji1]
 
Dah huyu Manara akikasirika huwa anakosa busara sana, Hakupaswa kumuongelea mkuu wake wa kazi hivi.

Nilimuona alivyomporomoshea maneno yule mtangazaji wa Clouds kwenye press yake na waandishi wa habari kabla ya game ya Yanga nikamtoa thamani.

Leo hii Haji hata kama umesingiziwa kitu, sio maadili mema kufanya hivi alichofanya. Mkuu wako wa kazi ana haki ya kukuonya iwapo amehisi umekosea, ila wewe wa chini yake hupashwi kumdindia na kumuwekea kibesi hivi, badala yake angepeleka haya malalamiko kwa viongozi wakubwa na sio kumwaga mboga hadharani.
 
Tatzo shule hamna kichwani
 
Fala Sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1483]
 
Ila simba nao wajinga sana, tangu lini afisa habari wa Coca cola akawa ambasador wa Pepsi?

Yaani Haji ni afisa habari wa Simba, ambayo ina dhaminiwa na bidhaa za Metl, hapo hapo ni balozi wa bidhaa za Asasi na GSM washindani wa Metl.

Haji ameitumia simba kupata umaarufu, kisha akautumia huo umaarufu kutangaza bidhaa za kampuni mshindani wa wadhamini wa simba......
 
Yeye mwenyewe analipwa jiwe saba bila mkataba ndio ataweza kumlipa mtu kweli?
 

Oscar Oscar kama angekuwa ni Simba. Angekuwa anasubiri simu sasa hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…