Haji Manara apigwa chini idara ya habari Simba

Simba wamefanya kosa kubwa sawa na lile walilowahi kulifanya chama changu cha Chadema (samahani kwa kuleta mfano wa kisiasa hapa), KUMLETA VICENT MASHINJI AVAE VIATU VYA DR.SLAA.

Muamini,msiamini: Simba inaenda kuwa ya bariiiidiiii kama pipi kifua, sawa tu na Vyura FC.

Siyo mara zote professionals wanafanya vizuri, kuna wakati wanazidiwa kwa mbali sana na amateurs (e.g Haji Manara). Na jambo hili nimeliona sehemu nyingi tu.
 
Kapigwa chini au mkataba umeisha? Kwahiyo na magori nae kapigwa chini?
 
Lol! Nina Tiket Yako! Popote Ulipo Jitokezee
Daaah! Bahati mbaya niko mbali leo ningeijia Mtani. Niwekee ya mechi na Ud Songo ndio nimepanga niende nikawazomee.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Habari ya miaka ndugu yangu? 😜 Umejua kuadimika.
 
Ndio nasema kule ambapo mnasema tupo kunawakaribia Mtani. Na hapa napata shaka kama mtajaa Uwanjani hiyo mechi na Ud Songo.

Sababu mpiga kelele hatokuwepo.
Hivi watu walikuwa wanajaa kumfuata Manara au waliifuata Simba? Elewa Simba ndiyo ilikuwa inambeba Manara na sio yeye kuibeba Simba.
Binafsi nilikuwa simkubali Manara maana alishaanza kuingiza siasa na kutaka ionekane eti Simba nayo inamlamba miguu Makonda wakati sivyo hata kidogo.
 
Nadhani mko wachache Mkuu ambao mlikuwa hamumkubali.

Na huo upande wa kumbeba huenda ikawa ni kweli Simba inambeba ila upande wa kuhamasisha ye ndio alikuwa mpiga domo mkuu tena jumlisha na zile tambo zake basi kila mmoja anaona ni vyema aende Uwanjani akajionee yasemwayo.
 
Manara ataendelea kuwa msemaji wa club ila atakuwa chini ya Gift Macha.
Inaonekana anawanyanyasa sana kwasukwasu maana si kwa kumuogopa hivi
πŸ‘
 
ujanja mwingi mbele kizaaaa..

aliskika mlevi mmojaa...
 
Yule vuvuzela wa Simba,kapigwa chini ,nafasi yake imechukuliwa na Gift Macha.
Naamini Gift atakuwa kiprofeshenali zaidi,maana press conference za Haji zilikuwa ni full kuisema Yanga.
Jamaa hakuwa pfrofeshonel kabisa.
Manara ni mwana ngonjera, tapeli professional
 
Yule vuvuzela wa Simba,kapigwa chini ,nafasi yake imechukuliwa na Gift Macha.
Naamini Gift atakuwa kiprofeshenali zaidi,maana press conference za Haji zilikuwa ni full kuisema Yanga.
Jamaa hakuwa pfrofeshonel kabisa.

Huyo sijui Manara ingekuwa ni ulaya anefungiwa kwa kuonyesha disrespect (dharau/kutoheshimu) kwa timu nyingine..Mtu anabwabwaja eti watachukua ubingwa miaka kumi mfulululizo eti 'back to back'....hovyo kabisa...kwa mashabiki kutamba sawa lakini siyo kwa kiongozi.eti "nawachukia gongowazi"......hovyo..kabisa...
 
Daaah! Bahati mbaya niko mbali leo ningeijia Mtani. Niwekee ya mechi na Ud Songo ndio nimepanga niende nikawazomee.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Habari ya miaka ndugu yangu? 😜 Umejua kuadimika.
Ntaindaa Kwa Ajili Yako, Vipi Lakin Mpira Unaangalia!?

Nipo Mtani Wangu Mambo tu Ya Dunia Yanatupoteza Kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…