Haji Manara nakuonya mapema usifanye hiyo Press Conference yako ya Kuwachafua Waandamizi wa Simba SC wiki ijayo

Haji Manara nakuonya mapema usifanye hiyo Press Conference yako ya Kuwachafua Waandamizi wa Simba SC wiki ijayo

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Nasikia unapanga kufanya Press Conference yako ya Kutapika Nyongo yako dhidi ya Simba SC hasa Watendaji wake kati ya Jumatatu au Jumanne ijayo.

Nami pia nakuonya mapema sana just ya hili kwani ukitekeleza hii adhma yako utakuwa umekaribisha Mashambulizi hatari ya Kiyahudi dhidi yako.

Wakati ukijiandaa Kutema Nyongo na Kuichafua Simba SC hasa Watendaji wake nami nakuambia tu ya kwamba tunamalizia Kuzipangilia Meseji zako zote za Kuihujumu Simba SC kwa Yanga SC kupitia Marafiki zako Watatu wa Yanga SC na Mmoja akiwa ni Mtoto wa Mstaafu Mmoja Tanzania.

Baada ya hapo tutaweka Ushahidi wa Kijiografia wa ulipokuwa Siku ya Jumanne na Jumatano eneo la Kigamboni na Maadui wa Simba SC.

Nakuomba mtafute Mtaalam yoyote kisha alikague Gari lako kisha utagundua kuna nini Kilifungwa bila Wewe Kushtuliwa ili ujue kuwa pamoja na kujifanya Kwako Mtoto wa Mjini ila bado ni Mngendembwe tu kwa waliokuzidi Akili.

Mwambie pia na Mkeo kuwa hizo Chattings zake na Waandamizi na Matajiri wa Yanga SC ili Wewe utumike kama Delilah kwa Mumeo Haji Manara tunazijua na zipo tayari tayari pia.

Jana umejifanya Kusambaza Voice Note Kisanii ukijifanya Unalia ili kutatuta Huruma kwa Watu kisha baada ya hapo ukawa unacheka na Watu Wawili mliokuwa nao hapo Mikocheni na baadae mkaenda Kugambeka eneo Jirani.

Na ulilolisahau ni kwamba hata huko Yanga SC ambako unatumika kuna Watu wa Simba SC ambao ni wana Yanga SC kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo Kaburu alikuwa Simba SC ila alikuwa ni mwana Yanga SC na Kifukwe alikuwa Yanga SC lakini Kiuhalisia ni mwana Simba SC.

Haji Manara umeshajiuliza ni kwanini ile Juzi ulipoenda Kisiri Kigamboni Avic Town walipo Yanga SC muda huo huo tu CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez akakutumia Meseji fupi ya Kukuambia uache Ujinga, Unafiki na Usaliti?

Nina mengi juu yako Haji Manara ila nakuonya acha Kudanganyika na Kutumika na hao wanaokupa Kiburi na nakuambia usije Kuthubutu kufanya hiyo Press Conference yako Wiki ijayo kwani Simba SC haitokujibu na nawaomba Simba SC wasikujibu ila watuachie Sisi tunaokujua vyema ndani nje tuweze Kukuanika na najua hata hawa wanaokuamini na kukuonea Huruma leo hii watakuchukia.

Umeshatusaliti vya kutosha inatosha!!!!
 
Kwa iyo haji aneuza match ya tareh 25 ,?
100% Yes na hata ile ya Kaizer Chiefs kuna Jambo baya la Kimkakati aliwashirikisha Yanga SC ambao nao kuna namna kwa Kumtumia Senzo Mazingiza walifanya kwa Kaizer Chiefs FC ila Kiongozi Mmoja wa Serikali mkubwa tu akamuombea Radhi.

Mtafuteni mumuulize juu ya hili kwani linajulikana ndani ya Kamati Kuu za Kimashindano za Simba SC isipokuwa Simba SC humalizana kimya kimya na pengine hata Kimafia kama ukijifanya ni Jeuri.
 
Acha kumtisha Haji.

Mimi ni MwanaSimba ila muumini sana wa ukweli. Kama kuna longolongo zinafanyika huko ndani, Haji aeleze ukweli.

Hatuwezi kuyakimbia matatizo kwa kujidanganya kuwa hayapo. Na bora yajulikane na kutatuliwa kwa muda huu, kuliko tuendelee kuyafuga baadae yatuharibie.

Muda pekee wa kuwekwa wazi ni sasa wakati tupo ukingoni mwa mechi za mashindano. Likizo iishe na varangati hili liishe. Tukirudi tupo fresh kabisa.

Kuna matatizo mengi Simba SC, ila kivuli cha kufanya vizuri kinayaficha hayo yaliyopo.

Ukweli ni kuwa, Haji kakosea. Lakini, hatuwezi kumtisha kwa kumzuia kusema uozo uliopo.
 
Nasikia unapanga kufanya Press Conference yako ya Kutapika Nyongo yako dhidi ya Simba SC hasa Watendaji wake kati ya Jumatatu au Jumanne ijayo...
Kumbe mmempigilia GPS haruki huyu jamaa
Na hiyo GPS ndiyo imemmaliza pamoja na Simu yake ambayo Watu wanaifuatilia 24/7 baada ya Zawadi Mauya kutulaza mapema tarehe 8 May, 2021 kwa Goli lake la dakika 11 tu ya Mchezo.
Na yeye atalala na viatu aisee
 
Na ulilolisahau ni kwamba hata huko Yanga SC ambako unatumika kuna Watu wa Simba SC ambao ni wana Yanga SC kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo Kaburu alikuwa Simba SC ila alikuwa ni mwana Yanga SC na Kifukwe alikuwa Yanga SC lakini Kiuhalisia ni mwana Simba SC.
Sasa unashangaa nini Manara kutumika wakati michezo hii unaijua
 
Back
Top Bottom