Haji Manara nakuonya mapema usifanye hiyo Press Conference yako ya Kuwachafua Waandamizi wa Simba SC wiki ijayo

Haji Manara nakuonya mapema usifanye hiyo Press Conference yako ya Kuwachafua Waandamizi wa Simba SC wiki ijayo

Manara ana asili ya utapeli na kupenda pesa . Mbele ya pesa yupo tayari kufanya chochote. Nachowalaumu Simba ni kumchukua mtu mwenye historia hiyo na kumkaribisha jikoni, nani hajui sababu ya kuacha nafasi ya ukatibu mwenezi ccm mkoa wa Dar es sallam halafu leo analialiakujifanya anaonewa.
 
Ai mlikuwa mnamshangilia wakati anatukana ovyoovyo watu, mlikuwa mnamuona malaika, sasa amewazingua mnaanza kutoa mapovu, katukana waandishi kuwa ni takataka mkamshangilia, kamtusi Prisca kishamba mkamshangilia........sasa anamtusi demu wa mwamedi mnanuna.


NB:Jambo la Hajji ni conflicts of interest tu ,Na MO ndiyo anaengeneer japo kajificha.....anafanya matangazo kwa washindani wa mwamedi Azam.........
 
Nyie wanasimba acheni kujitikisa huku mitandaoni mwisho wa siku nyote mnaonekana kina manara tu. Kama mtu ndio tabua yake na hamumchukulii hatua yoyote ina maana mnamuogopa.

Hata kwenye hili ni ajabu mpaka sasa mnabwabwaja tu mitandaoni, hakuna chochote toka kwenu. Hii ishu ni nzito, ikiwa na maana kwamba wanasimba hamwalipi inavyostahili wafanyakazi wenu.

Lakini tuliiii eti wanasubiri kwanza mechi ya j2 ipite, hili jipya sasa huyu anasema sio mechi ipite ila ni mpaka manara aitishe press na waandishi.

SIMBA MNAMUOGOPA MANARA.
 
Nimesoma nyuzi zako kadhaa nimekunyoshea mikoni. Sema sisi wana simba tukitoaga maoni ya ukweli kabisa tunaonekana deportivo utopolo.
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Haji anaihujumu Simba...never ever.
Hivi ukimkuta mkeo guest na mwanaume halafu akwambiye hawajafanya kitu.
Walishinda chumbani kutwa mzima lakini hawajafanya kitu utaamini?

Manara ni msaliti.
Hawezi kushinda na kuwa na falagha na mahasimu wa SIMBA.

Manara must go,,

Utakuta yule Mzee mpili na manara lao moja.
 
Kwani kuna kitu gani ambacho unahofia atakisema hadi azuiliwe kuto kufanya press? Kuna madudu yanafichwa eeh??

Binafsi niseme tu ni upumbavu mkubwa sana kusema eti Haji anauza timu kwa yanga.

Haji Manara huyuhuyu anaye tukanwa matusi kila siku kwasababu ya Simba ?
Simba ikifungwa yeye ndio wakwanza kushambiliwa mara wamu edit Kama mwanamke mitandaoni mara wamuite Nguruwe.

Haji huyuhuyu anaye gombana na waandishi wa Yanga kina kitenge, Shafii Dauda prisca n.k wanao zusha uongo kila siku dhidi ya Simba.?

Haji huyuhuyu Simba inafungwa analia machozi anakuja mbele ya waadhishi wa habari na tv kuonyesha jinsi wavyo hujumiwa?

Eti leo yeye ndio anaambiwa anaenda kuuza timu.

Haji huyuhuyu Simba inaenda kucheza ndondo kipindi hicho yeye anakaa mlangoni kukusanya viingilio timu ipate pesa leo huyu auze timu huyu.

Tena anaye mtuhumu ni babra aliye kuja juzi tu kwenye timu heti yeye ndio kawa mfia timu kuliko Haji?

Huyu Honspopa huyu si ndio yeye aliye watuhumu kina chama na Zimbwe kuwa wanauza game hadi kulekea Simba kufungwa Leo kageukia kwa Haji??


Wamseme kwa mambo mengine ila si kuuza timu hiyo ni matusi makubwa sana kwa mtu kama haji ?
 
Nasikia unapanga kufanya Press Conference yako ya Kutapika Nyongo yako dhidi ya Simba SC hasa Watendaji wake kati ya Jumatatu au Jumanne ijayo.

Nami pia nakuonya mapema sana just ya hili kwani ukitekeleza hii adhma yako utakuwa umekaribisha Mashambulizi hatari ya Kiyahudi dhidi yako.

Wakati ukijiandaa Kutema Nyongo na Kuichafua Simba SC hasa Watendaji wake nami nakuambia tu ya kwamba tunamalizia Kuzipangilia Meseji zako zote za Kuihujumu Simba SC kwa Yanga SC kupitia Marafiki zako Watatu wa Yanga SC na Mmoja akiwa ni Mtoto wa Mstaafu Mmoja Tanzania.

Baada ya hapo tutaweka Ushahidi wa Kijiografia wa ulipokuwa Siku ya Jumanne na Jumatano eneo la Kigamboni na Maadui wa Simba SC.

Nakuomba mtafute Mtaalam yoyote kisha alikague Gari lako kisha utagundua kuna nini Kilifungwa bila Wewe Kushtuliwa ili ujue kuwa pamoja na kujifanya Kwako Mtoto wa Mjini ila bado ni Mngendembwe tu kwa waliokuzidi Akili.

Mwambie pia na Mkeo kuwa hizo Chattings zake na Waandamizi na Matajiri wa Yanga SC ili Wewe utumike kama Delilah kwa Mumeo Haji Manara tunazijua na zipo tayari tayari pia.

Jana umejifanya Kusambaza Voice Note Kisanii ukijifanya Unalia ili kutatuta Huruma kwa Watu kisha baada ya hapo ukawa unacheka na Watu Wawili mliokuwa nao hapo Mikocheni na baadae mkaenda Kugambeka eneo Jirani.

Na ulilolisahau ni kwamba hata huko Yanga SC ambako unatumika kuna Watu wa Simba SC ambao ni wana Yanga SC kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo Kaburu alikuwa Simba SC ila alikuwa ni mwana Yanga SC na Kifukwe alikuwa Yanga SC lakini Kiuhalisia ni mwana Simba SC.

Haji Manara umeshajiuliza ni kwanini ile Juzi ulipoenda Kisiri Kigamboni Avic Town walipo Yanga SC muda huo huo tu CEO wa Simba SC Barbara Gonzalez akakutumia Meseji fupi ya Kukuambia uache Ujinga, Unafiki na Usaliti?

Nina mengi juu yako Haji Manara ila nakuonya acha Kudanganyika na Kutumika na hao wanaokupa Kiburi na nakuambia usije Kuthubutu kufanya hiyo Press Conference yako Wiki ijayo kwani Simba SC haitokujibu na nawaomba Simba SC wasikujibu ila watuachie Sisi tunaokujua vyema ndani nje tuweze Kukuanika na najua hata hawa wanaokuamini na kukuonea Huruma leo hii watakuchukia.

Umeshatusaliti vya kutosha inatosha!!!!
Hakuna lolote,haji manara fanya tu hiyo press comference

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Utasemaje nimesahau hayo maneno ya huyo mzee bila kujua kama nimeyasikia hayo maneno?
Hvi Kuna tofauti Gani Kati ya mtu ambaye kafanya kitu ila amesahau kama alikifanya Na Yule ambaye hajawahi kukifanya kabisa?
 
Wewe shabiki wa ngongowazi mchukueni huyo Manara
Mimi ni Shabiki wa Simba kindakindaki.

Ila kama nilichokiandika kinaondoa uhalali wa kuwa Mshabiki wa Simba basi unajidanganya.
 
Nyie wanasimba acheni kujitikisa huku mitandaoni mwisho wa siku nyote mnaonekana kina manara tu. Kama mtu ndio tabua yake na hamumchukulii hatua yoyote ina maana mnamuogopa.

Hata kwenye hili ni ajabu mpaka sasa mnabwabwaja tu mitandaoni, hakuna chochote toka kwenu. Hii ishu ni nzito, ikiwa na maana kwamba wanasimba hamwalipi inavyostahili wafanyakazi wenu.

Lakini tuliiii eti wanasubiri kwanza mechi ya j2 ipite, hili jipya sasa huyu anasema sio mechi ipite ila ni mpaka manara aitishe press na waandishi.

SIMBA MNAMUOGOPA MANARA.
Baada ya match kigoma anakula umeme huyo naashachungulia amewahi kujitoa
 
Back
Top Bottom