Haji Manara nakuonya mapema usifanye hiyo Press Conference yako ya Kuwachafua Waandamizi wa Simba SC wiki ijayo

Ni wapumbavu kupindukia ..unapoenda mahakamani jaji hua anatoa nafasi kwa mshtaki na mshtakiwa wote kuongea kila mtu kwa nafasi yake , tunataka kusikiliza anachotaka kusema Manara

Mbona alishakisema kwenye voice note ww bwimbi hakuna kipya
 
Hiyo press inatakiwa waandishi wamzilie, halafu ajue anacheza na hisia na imani za wengi. Akibugi itamgharim, simba na yanga ni dini za watu..
ila mjiandae kwa kesi pia maana hayo ya kutrace simu zake na location ni kuingilia faragha ya mtu hivyo yaishie hivyo hvyo sio kupelekana tena mahakamani
 
Msimtishe, Manara, kama mlijua tangu zamani mbona hakukuwa na reaction?
Hakuna cha GPS wala tracking yoyote. Sema amepiga kwenye Mshono tu.

Hapotezi chochote , Simba itawagharimu.
Muguseni muone nani atanuka
Wacha utoto wewe, Manara kaokotwa na Simba SC anazurura kariakoo amepauka vumbi leo ajifanye mjanja zaidi ya Simba?
 
Umefeli kwenye judgement, Barbara kuja juzi hakumuondolei nafasi yake na mapenzi yake kwa Simba, na wakati huo huo, huyo Manara unaemuamini ndio anaitumia imani uliyonayo kwake kuihujumu Simba, wake up.

Yale madai yake aliyoyatoa jana ni ya kijinga sana, na zaidi kuyatoa kwake wakati huu tukielekea kucheza na Yanga SC mechi ya fainali ya ASFC, wakati ambao Manara ana uhusiano na viongozi wa Yanga SC, na zaidi kwanini hakupeleka madai yake kwa uongozi wa Simba akakimbilia Kitenge Tv ya yule yule mchawi wa Simba?

Manara simuamini tena, ni ndumilakuwili mnafiki, anatumiwa na Yanga kuleta mgogoro Simba SC kwa maslahi ya Yanga SC, kwa ujinga alioufanya jana sitegemei aendelee tena kuwa msemaji wa Simba come next season.
 
Kwa lugha nyingine kusaidia polisi ni kuwa wewe ni mtuhumiwa na unapelekwa kituoni kuhojiwa. Ni ukweli kuna ugumu wa kuwapata wahusika, ila mtoa mada kasema watabainisha vitu walipachika kwenye gari na simu ya Manara ili kunasa mawasiliano yake, akisema hadharani hili ni ikionekana ni ukweli, huyu unasukuma ndani fasta.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Si uje useme uozo wa nyumbani kwako kwanza kabla ya kutaka uozo wa Simba usemwe
 
Unataka Simba ichambane na Manara?
Hii ni Simba siyo utopolo.Simba haiwezi kumjibu manara kama unavyotaka,sisi wapenzi wa Simba ndio tutamjibu
 
Semeni yote ila kitendo cha Haji kuvujisha zile clip ni ishara tosha kuwa ni mbinafsi,msaliti,na ana agenda ya kuihujumu Simba.Kama angekuwa anaioenda Simba yote hayo angeyatoa baada ya mechi.

Kutukanwa kwake Simba ikifungwa ni kwa sababu alipenda mwenyewe.Maana yeye naye ana matusi na gubu sana.Si wote tuliyapenda maneno yake ijapo ni wapenzi wa Simba.

Msimtetee Haji ni mnafiki.
 
Hiyo press inatakiwa waandishi wamzilie, halafu ajue anacheza na hisia na imani za wengi. Akibugi itamgharim, simba na yanga ni dini za watu..
Wandishi wakatae kwenda?wakati hiyo ni habari?!!Yaani mechi ya YANGA, na SIMBA inavyokuzwa utadhani kuna mpira basi kumbe ni butua butua tu! Yaani mtu anaweza kuhisi ni bonge la mechi kama la brazil na argentina miaka hiyo ya 90!!
Waafrika bwana, kwa hiyo haji kosa lake ni kuonekana na watu wa yanga, na kufanya nao biashara?kwanza msemaji wa timu na kuihujumu timu wapi na wapi?au mimi ndio sielewi yaani anawezaje kufanya hadi timu ikafungwa?
 
Unataka Simba ichambane na Manara?
Hii ni Simba siyo utopolo.Simba haiwezi kumjibu manara kama unavyotaka,sisi wapenzi wa Simba ndio tutamjibu
Kwani kawaatack wapenzi wa simba au viongozi wa simba!? Na sio mara moja anaaibisha brand yenu ila anakaliwa kimya tu. Nyie mashabiki mtamuandama mitandaoni lakini hamuwezi kutoa uamuzi wowote juu ya hatma yake.

Mo akisema na abaki/aende hakuna wa kumpinga kati yenu, kwahiyo kelele zenu hazina impact sana. Tumsubiri Mo tu
 
Hapo ndo mtajua kuwa manara ni mkubwa kuliko mkia FC
 
Na utakuwa mpumbavu sana kuamini Manara ana nia njema na Simba kwa kuvujisha clip zile kabla ya derby
Ile ni attitude ya Manara ambayo mashabiki wa Simba mmekuwa mkiipraise kila siku kwamba "Semaji La Dunia Limesema"..mara ngapi amekuwa akitukana na kudhalilisha watu? Waandishi? Etc na mishabiki ya Simba mmekuwa upande wake na kumtetea? Tulieni dawa iwaingie sasa, endeleeni kumtetea.
 
Kama una uozo wake basi kuwa mpole akisema ukweli kuhusu uozo wa wakubwa wa simba na wewe umripue sasa iwe bila bila,sio kuanza kumtisha .....hii ni vita na kwenye vita hakuna huruma akimwaga mboga nawe mwaga ugali kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…