Hajia Manara aonekana Mwanachi Day japo adhabu yake inaendelea

Hizo nguvu za kupambana naye mnazitoa wapi
 
Hiyo ndo maana ya Surprise. Hakuna ambacho hakikupangwa hapo.
 
Hata mwaka jana aliingia kwa style km ya leo, kuhusu mapengo uwanjani nadhani mchawi ni kiingilia mwaka jana kiingilio cha chini ilikuwa ni 5000/= na leo kiingilio cha chini ni 10000/=

Hakuna cha uchawi wa kiingilio!
Walituambia tiketi zote za VIP ziliisha ila upande wa VIP umetoboka kama chekecheke!
 
Kama amekata rufaa alikata rufaa kwa kutumia barua ipi?

Maana huwezi kukata rufaa pasipo kupokea barua/nakala ya hukumu.
Tatizo la makolo mnatumia mihemko badala ya kusikiliza facts . hebu nenda kaisikilize ile press ya manara vizuri na kwa umakini. Manara alisema ameshindwa kukata rufaa sababu hana nakala ya hukumu ambayo inatolewa na hiyo kamati uchwara na walikuwa hawataki kumpa . na kanuni inasema mtu ataanza kutumikia adhabu pindi anapopewa nakala ya hukumu. Ndo maana siku ile jamaa akasema yeye bado ni msemaji wa Yanga kwa sababu hajakabidhiwa nakala ya hukumu licha ya kwenda kuifuatilia Mara kadhaa jamaa wamekalia kumzungusha.
 
TANGAZO KWA WAJUMBE WOTE WA KAMATI YA MAADILI TFF.

Kesho mnamo saa 4 kamili ya asubuhi kutakuwa na kikao cha dharura kuhusiana mwenendo na mustakhabari wa mpira wetu.

Play fair

Wance Karia
Rais wa tff
Kweli kachafukwa hadi jina lake anakosea!
 
Sasa kwanini leo baada ya utambulisho wa wachezaji amesema hajihusishi na soka kufuatia adhabu aliyopewa na alialikwa kama MC tu hivyo anaondoka zake Kigogo kwenye shughuli za uMC?

Kama hakupata barua ya hukumu kwanini atamke yote haya?
 
Tff hakuna kufumbia macho upumbavu kama huu
 
Kasema ameajiriwa kama mshereheshaji na wala hajihusidhi na mpira.

Na kawakaribisha mlioko daslam muende kigogo sambusa kuna sherehe yeye ni MC 😃😃
 
Ni suala tu la kisheria mkurugenzi. Mimi sioni kosa lake kusherehesha hili tamasha. Ni moja ya shughuli zake hizo bila shaka.

Ni hivi mkuu, huyu Manara last press aliyoitisha alisema yeye bado msemaji halali
Wa Yanga… na leo kupanda jukwaani na kuwatambulisha wachezaji wa yanga ni kwamba anauthibitishia umma kwamba yeye bado msemaji wa Yanga.Ni dharau ya hali ya juu

Mbaya zaidi hapo uwanjani kuna mawaziri na viongozi wakuu wa chama,Yanga kumtumia Manara wanataka kuonesha kama vile wanaungwa mkono na viongozi wa chama na serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…