Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Hii ni makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Gazeti la NIPASHE la Jumapili ya leo
Kama kawa kila siku za Jumapili hutiririka na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa
zenye swali hoja majibu utayatoa wewe msomaji mwenyewe.
Swali la leo ni kuhusu haki nchini Tanzania na falsafa ya 4R za Rais Samia。
Rais Samia alipotwaa nchi, ameibuka na falsafa mpya ya 4R ambayo utekelezaji wake kikamilifu utaibadili kabisa Tanzania kuwa ni nchi ya Haki, Upendo, Ustawi, Mapatano, Maelewano na Maendeleo Endelevu, sasa je hizi 4R za Samia zinaleta mabadiliko ya kweli au 4R ni mahubiri tuu lakini tukija kwenye utekelezaji ni utekelezaji kiinimacho?.
Watanzania waelimishwe haki zao, 4R za Rais Samia zisiwe ni maneno matupu, jee sasa umefika wakati Watanzania tuombe kuona utekelezaji kwa vitendo wa hizi 4R au tuendelee kuridhika na haya maneno maneno na utekelezaji viini macho?.
Tumefundishwa kuwa na shukrani, hivyo naianza makala ya leo kwa pongezi na shukrani kwa Rais Samia kwa falsafa yake ya 4R na mahubiri yake mazuri kuhusu haki.
4R ni kifupisho cha maneno ya Kiingereza Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reform (Mabadiliko) na Rebuiding (Kujenga upya).
Makala hii inajikita kwenye R moja tuu ya Mabadiliko, tunataka mabadiliko ya kweli na sio mabadiliko kiinimacho!.
Tunawaomba watendaji waitafsiri kwa vitendo falsafa hiyo ya 4R, kwa kutenda kile kinachohubiriwa yasibaki kuwa maneno tuu ya mahubiri ya 4R lakini vitendo ni tofauti!.
Hakuna mashaka kabisa kuhusu nia ya dhati ya Rais kutaka Watanzania kutendewa haki, ana nia njema ya dhati na thabiti Watanzania wapate, haki zao, lakini anakwamishwa na baadhi ya Watendaji wake ndio wanao mwangusha!.
Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki ni stahili na stahiki inayopaswa kutolewa bila wewe kuiomba, na ikitokea haki haikutolewa au haikutendeka, haki haiombwi, bali inapaswa kudaiwa, sasa ukiwa mtu hujui haki yako, huwezi kudai kitu usichokijua!,ndio maana akina sisi,tumejitolea kuwaelimisha Watanzania haki zao。
Nikimuangalia na kusikiliza kauli zake kuhusu haki, kusema la ukweli kabisa, Rais Samia, ana nia njema ya dhati kutoka moyoni mwake kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki haya mambo ya ajabu ajabu yanayotokea ni uzembe na udhaifu wa baadhi ya watendaji wake, tunamshauri Rais Samia awe mkali kama Nyerere, kwenye ukiukwaji wa haki, ahakikishe hakuna Mswalie Mtume.
Nimekumbushia haki kufuatia kilichotokea hadi kifo cha huyu Mzee Kibao wa Chadema, ameuliwa kwasababu wananchi hawajui haki zao!. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao Mzee Kibao asingekubali kukamatwa na watu ambao hawatambuliki.
1. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, dereva wa basi la Tashrif asinge kubali kusimamishwa na watu wasiotambulika.
2. Kama Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, dereva wa Tashrif angekuwa anajua ile tiketi ya abiria, ni mkataba wa kisheria wa kumshusha abiria wake kituo alicholipia, dereva ana wajibu wa kisheria, duty of care, kuhakikisha usalama wa abiria wake na mali zake kwenye butt ya gari yake!. Mali pekee ambayo ni responsibility ya abiria ni mzigo wake wa mkononi, hand luggage anaoingia nao ndani ya basi, ndio "abiria chunga mzigo wako" lakini jukumu la abiria kufika salama anapokwenda, dereva wa basi ana wajibu wa kisheria kumfikisha salama.
3. Watanzania wangekuwa wanajua haki zao, abiria tuu wa kawaida akiwemo abiria aliyekaa seat no. 1 ya basi hilo ambaye ni traffic police, alikuwa na uwezo wa kuwabaini majambazi hao kuwa sio askari polisi wa kweli na kuwahamasisha abiria wengine wote wasikubali abiria mwenzao atekwe!.
4. Watanzania wangezijua haki zao, wangejua Polisi haruhusiwi kumkamata mtu yoyote bila kwanza kujitambulisha yeye ni nani na ametokea kituo gani kwa kuonyesha kitambulisho cha polisi.
5. Watanzania wangejua haki zao, wangejua mtu anayekamatwa ana haki ya kusoma number ya kitambulisho na kuihakiki number ya askari police kwenye mfuko wa kushoto wa nguo ya polisi.
6. Wakija polisi ambao ni askari kanzu, hawa hawana uniform hivyo hawavai numbers, hawaruhusiwi kumkamata mtuhumiwa bila kuandamana na polisi wenye uniforms!.
7. Mtu yeyote kabla hajakamatwa lazima awe na arrest warrant na lazima aripoti ofisi ya serikali ya mtaa husika!, aonyeshe arrest warrant atasibdikizwa na mtendaji wa mtaa kuja kukukamata.
8. Baada ya polisi kujitambulisha kwa kuonyesha kitambulisho, kitu cha pili ni kuonyesha arrest warrant na kukumbia unakamatwa kwa kutuhumiwa kwa kosa gani?.
9. Polisi kabla hajamkama mtu anatakiwa kumweza haki zake ikiwemo
haki ya kunyamaza kimya, chochote utakachosema kinaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na haki ya kuwakilishwa na mwanasheria.
10. Kisha polisi hao watawaeleza hao mashuhuda wanakupeleka kituo gani ili ndugu zako wakufuatilie!.
Na ukifikishwa kituoni kabla hujaandikishwa maelezo unaaelezwa haki zako ikiwemo haki ya legal representation.
Hitimisho
Haki hizi zikifundishwa kwa wananchi, 'wasiojulikana' watapungua, watabaki tuu wale wa pyu pyu kama wa Lissu.
Sote tunajua kwa kauli na matendo, Rais Samia ana nia thabiti na ya dhati watu wapate haki zao, amekuwa akilihubiri hili kwa maneno na vitendo, na kuanzisha vitendo, kikosi kazi, tume ya haki jinai.
Kwenye kikosi kazi, Watanzania walitaka tufanye mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms ili haki zilizoporwa kinyume cha Katiba zirudishwe, hili Rais Samia hajalitendea haki ila abebadili sheria ya uchaguzi na tume ya uchaguzi kwa mabadiliko kiini macho!.
Watanzania wametaka Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi, Rais Samia ameibadilisha jina Tume ya Uchaguzi kutoka NEC na kuiita jina jipya la INEC sasa inaitwa Tume Huru ya Uchaguzi, ila tume bado ni ile ile!. Watanzania hawakuomba jina la Tume ya Uchaguzi libadilishwe kutoka kuitwa Tume ya Uchaguzi na sasa kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi, Watanzania walitaka Tume ibadilishwe iwe ni Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi na sio kubadilishwa jina lakini Tume bado ni ile ile, watu bado ni wale wale na uchaguzi utaendelea kusimamiwa na wale wale makada kindakindaki wa chama kimoja kwenye kofia za wakurungezi wa Halmashauri!. Mabadiliko haya ni kiini macho!.
Watanzania walitaka sheria mpya ya uchaguzi yenye kutoa haki sawa kwa wote na uwanja sawa wa uchaguzi, kwasababu sheria ikiyokuwepo ilikuwa ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT, tumeletewa sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kwenda kinyume na katiba!, hivyo mabadiliko haya ya sheria ya uchaguzi pia ni mabadiliko kiinimacho!.
Rais Samia, Watanzania tunakupenda, tunakukubali, tunakuomba mahubiri yako ya falsafa yako ya 4R, yasiwe ni mahubiri ?ya maneno maneno tuu,? (preaching only), tunaomba wasisitize watendaji wako watekeleze kwa vitendo (put to practice what you preach)
Mungu Akubariki Uyaweze Yote Katika YEYE!.
Mungu Ibariki Tanzania
Nakutakia Jumapili Njema.
Paskali