Ardhi ilikuwa ya wote. Zilifuatwa taratibu za kimataifa kupata Taifa la Israel, baada ya Waingereza kuamua kuondoka kufuatia resisitance ya kila mara ya Wayahudi. Waarabu wa Palestine wakaridhia. Lakini waarabu wa mataifa jirani wakapinga na kuwaambia waarabu wa Palestine wasikubali kuwa Taifa moja na Wayahudi. Tume ya Umoja wa Mataifa ikatumwa kupata maoni ya jamii husika. Wayahudi wengi na waarabu wachache wakaridhia kuwa kwenye Taifa moja. Waarabu wengi wakakataa, wakitaka kuwepo mataifa mawili, moja ni hilo la Israel, na la pili ni la Palestine. Umoja wa mataifa wakatengeneza mipaka ya mataifa hayo mawili, Taifa la Israel likipewa 52% na Waarabu wa Palestine 48%. Wapalestina wakaridhia lakini nchi za Kiarabu zikapinga. Kwenye Umoja wa Mataifa, nchi nyingi wanachama zikaridhia huo mgawanyo. Waarabu wa Palestine, badala ya kuchukua hiyo 48% waliyotengewa, wakishawishiwa na kusaidiwa na nchi za kiarabu, wakaivamia Israel na kuanzisha vita wakitaka kuwaangamiza wayahudi wote waishe eti ili wao wachukue eneo lote. Vita ilianzishwa na waarabu, siyo Wayahudi. Lakini bahati mbaya kwao, wakapigwa vibaya. Kanuni za vita vya kale, ukishindwa, inakuwa kama inavyofanya Russia huko Ukraine, maadui zako wanateka eneo lako, na ukishindwa kulirudisha kwa kupitia mapigano, ujue hilo eneo limekwenda.
Tatizo siyo waarabu wa West Bank na Gaza, tatizo ni Iran. Wakiachwa waarabu wa Palestine wenyewe kabisa na Israel, kwa usaidizi wa mataifa yenye dhamira njema, haitachukua muda Wapalestina na Waisrael ama watakuwa Taifa moja lenye jamii zinazoishi kwa amani au mataifa mawili jirani ambayo yana jamii zinazoshirikiana. Kabla tar 7 October mwakajana, kulikuwa na waarabu wengi wa Palestina wanaofanya kazi Israel, lakini pia ndani ya Israel kuna idadi kubwa ya waarabu waislam ambao wamekuwa wakiishi bila shida. Tatizo ni hao hamas wanapoingia na kujifanya watu wazuri, kisha wanashambulia na kuua wayahudi, hapo sasa na watu wengine wasio na hatia wanaanza kutiliwa mashaka.