Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Iyakuze na Twaweza hawaingiliani na approval ratings za Mh. Rais, na wala sikumbuki ni lini waliwahi kufanya utafiti huo.
Basi hujui hoja mkuu, Waliendesha kura ya maoni na tukapata majibu mazuri tu , kilichotokea unakijua?
 
Sasa ni wakati wa kuibadirisha ili Mhe Rais aongezewe mitano tena
Hujaeleza hasa kwa nini aongezewe mitano tena.
Unazungukazunguka tu bila maelezo ya kina juu ya hilo.

Wasiopenda upuuzi wako wamekwishakupa sababu kwa nini mtu wako hafai, wewe unakazana tu..., "hujavunja sheria"!

Bado hujihisi kwamba hata kazi ya "kuuza mbuzi ndani ya gunia" huiwezi?
 
Hilo ndio jibu sasa mzee wa watu amesema akimaliza anapumzika , wanataka aendelee ili waweze kunufaika..
Kuna watu wanajijua, watapangiwa ukarani wa masijala halmashauri ambazo hakuna kiongozi anaenda, hao lazima wajipiganie SANA.
Kuna watu wanajua watakuwa na kesi za kujibu, na hakutakuwa na kuwatetea.

Mhm DR. Magufuli asikubali kuingia kwenye huu mtego. Kikundi cha wachache chenye maslahi binafsi!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hoja yako ni mufilisi, haina mashiko;

Umeelewa mada unataka kupindisha ukweli, yani herufi moja ndio ikitoe kwenye reli?

Duh
Wewe si umejitangaza ni "mfuata sheria"?
Utakana kosa ulilolifanya hapa kisheria?
 
Kwanini aongezewe muda?
Atakuambia anajenga reli, bwawa, daraja, anasimika nguzo za umeme,n.k. as if physically anafanya hizo kazi, wakati kuna kampuni za ujenzi zinajenga, na hiyo miundombinu iko chini ya wizara zenye watendaji, wanaosimamia!

Unajiuliza TRC, REA, TANESCO, wana kazi gani?

Hawa ndiyo watakuwa walimu wetu wa somo la historia.😅

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kuna watu wanajijua, watapangiwa ukarani wa masijala halmashauri ambazo hakuna kiongozi anaenda, hao lazima wajipiganie SANA.
Kuna watu wanajua watakuwa na kesi za kujibu, na hakutakuwa na kuwatetea...
Ni sawah mkuu , watu wanafanya maovu awamu hii halafu wanajificha chini ya mbawa za Raisi, kwamba aongeze muda wa kuongoza , ili maslai yao yaendelee kupatikana.

Kuna mambo mengi sana yanaendelea ambayo hata Raisi hajui ndio maana anapokuja kufahamu huwa anawafukuza mapema sana. Nampongeza kwa hilo.

Hivyo basi hawa viongozi uchwara hawa ambao hawana sifa ya kuongoza hujinyenyekeza sana kwa raisi wakipata madaraka , wanakuwa wapiga debe wakubwa sana kumsifia mzee wa watu, kumbe wanamambo yao.

Raisi nakushauri achana na hawa viongozi njaa wanaokuzunguka staafu kwa heshima. Usichafuliwe taswira yako na watu binafsi amabo wanajali matumbo yao.
 
Kwa hiyo tutaamini vipi kama na wewe haunufaiki na kubadilishwa kwa mamlaka ya juu?

Mimi siongelei maskahi binafsi,
its not about power sharing, its about the capabilities of leading a country with diligence and high discipline.

Over
Watanzania tuliowengi tumepevuka kiakili.

Logic inakataa ati nafaidika lakini nataka Magufuli aondoke!

Lazima kuvuka stage ya ubinafsi na kwenda na principles, katiba.

Magufuli kavuka stage hiyo ndiyo maana alisema hatagombea.

Hii issue ya ninyi mnaaofaidika sasa, mnataka asiachie kwa maana akiachia aijra zenu ni dhahiri zinaenda na maji.

Na hapo ni kama mtu uko mediocre, vyeti vya magumashi au hutoshi hapo ulipo.

Ukijimini na uko well qualified, aje Kikwete,aje Magufuli, Jafo au Palamagamba utaendelea kuwepo.
 
Katiba sio msahafu, inabadirishwa (kilwa inapoonekana inafaa.

Sasa ni wakati wa kuibadirisha ili Mhe Rais aongezewe mitano tena
Ni nani na taratibu zipi zinazotumika kubadili katiba na kwa manufaa ya nani?

Najua swali hili huwezi kulijibu hapa.

Mtapeleka mswada wenu wa kubadili katiba kwenye Bunge lenu ambalo mumelipanga maksudi kufanya kazi hiyo?

Kama hujui ninachoandika hapa ngoja nikurahisishie: Mmewanyima wananchi kuchagua wabunge wanaowataka; nyinyi mkaweka wa kwenu ili wawafanyie kazi yenu hii chafu, halafu unakuja hapa kujidai, eti "Katiba sio msahafu, inabadirishwa (kilwa?) inapoonekana inafaa"

Nyinyi ndio mnawaamulia waTanzania kuwa inafaa katiba ibadilishwe ili mtu wenu aendelee kuwanyima haki yao ya msingi kabisa waTanzania:
"HAKI YA KUWACHAGUA VIONGOZI WANOWATAKA WAO WENYEWE BILA YA KUINGILIWA NA MTU/TAASISI NYINGINE YEYOTE".
 
Nyie mnaotaka aongezewe muda ndio wenye haki ya kujieleza kulingana na katiba ya nchi. Akina Askofu Emmaus Mwamakula wanaotaka katiba mpya wao hawana uhuru huo.

Unahisi kwann?? Anza kujibu kwanza maswali yetu kabla hatujachangia mada yako.
 
Hawezi kujibu maswali kama hayo, praise and worship team haina power hiyo .

Aendelee na mchakato wake baadae atajua hajui
 
Kwa kuwa umeandika kwa hasira, acha nikujibu kwa akili..
Akili gani uliyonayo.

Acha wenye kuona una akili au huna akili wakuambie.Bado hutaki kujitambua kama huna akili.Wengi humu wameshakuambia kuwa,akili huna na ujitambue hivyo.

Kama jina kwako sio issue,Huo ndio ujinga wenyewe tena wa kwanza.Hujijui unamzungumza nani na unazungumza na nani humu.Ndio ujinga huo.

Ujumbe ungekuwa umefika sawa sawa hakuna mtu angekurekebisha kwa kucomment chochote humu.Mara nyingi mwenye akili ukisema chochote chenye kutumia akili watu hukaa kimya kwa maana ya kukichua na kukifanyia kazi.

Ukileta pumba ndio wenye akili zao wanakufundisha.Ni vizuri pia kufundishika.Ili siku nyingine unapoandika ujue kuwa kuna wenye akili watasoma na watakuchallenge.

Ujinga mwingine,bado hujajitambua kuwa tayari unapingana na katiba.Na kupingana na katiba ni kuvunja katiba na sheria za nchi pia.Nilishasema kutokana na jeshi la polisi kuwa na double standard,ndiyo maana bado uko nje wewe.Vinginevyo ungejikuta LOCK UP.Shukuru Police double standard.

Mimi sio mwanasiasa,na afadhali tangu mwanzo hukujitambulisha kama mwanasia.Ningeshafungasha virago kwani mimi na wao ni maji na mafuta.kumbe ndio maana unaandika upumbavu huku shauri tumbo lako lijae kisiasa.Nakukumbusha tena kundi la kujipendekeza kama kina musiba na wengine kama paschal wako wapi. Mwenye kutoa nafasi ameshawashtukia na zimeisha mwaka huu.Tafuta njia nyingine.

Ukweli gani unaoutoa hapo wakati ni rojo tu.hakuna mwanasiasa wa Tanzania.anayesema ukweli?wote ni waongo tu kama wewe,mawazo yako binafsi baki nayo kichwani kwako ndiyo maana unayaita mawazo yangu binafsi.Ni ya kwako.Ukishawashirikisha wengine ni ya kwenu wote. Otherwise ungeyaleta kwa kuomba ushauri kwa kuwa ni mawazo yako.Pole sana, ndivyo ujinga ulivyo hivyo,na mjinga huleta hivyo hivyo kama ulivyoleta.

Wajinga wenzako ndio watakaoshawishika.Pole.
 
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu...
Unataka kumlazimisha mtu ambaye kashasema hataki kuwa rais baada ya 2025?

Unaelewa kwamba hiyo katiba unayoishadadia ina term limits?
 
Ni nani na taratibu zipi zinazotumika kubadili katiba na kwa manufaa ya nani?

Najua swali hili huwezi kulijibu hapa.

Mtapeleka mswada wenu wa kubadili katiba kwenye Bunge lenu ambalo mumelipanga maksudi kufanya kazi hiyo?

Kama hujui ninachoandika hapa ngoja nikurahisishie: Mmewanyima wananchi kuchagua wabunge wanaowataka; nyinyi mkaweka wa kwenu ili wawafanyie kazi yenu hii chafu, halafu unakuja hapa kujidai, eti "Katiba sio msahafu, inabadirishwa (kilwa?) inapoonekana inafaa"

Nyinyi ndio mnawaamulia waTanzania kuwa inafaa katiba ibadilishwe ili mtu wenu aendelee kuwanyima haki yao ya msingi kabisa waTanzania:
"HAKI YA KUWACHAGUA VIONGOZI WANOWATAKA WAO WENYEWE BILA YA KUINGILIWA NA MTU/TAASISI NYINGINE YEYOTE".

Alieshinda kura za maoni Kawe alikatwa akapewa mtu ambae sio chaguo la wanachi

Alieshinda kura za maoni Vunjo hakupitishwa bali akapewa mtu ambae sio chaguo la wanachi

Hao wote walipitishwa ili waende kuunga juhudi za kubadilisha katiba.

Kuna siku aliwahi kusema hajawahi kuhubiri katiba mpya wala kwenye kampeni zake hajawahi kusema chochote kuhusu katiba mpya, nyie mnaetaka kipengele cha katiba kibadilishwe kisa matamanio ya wahuni wachache ni bora mrudishe rasimu ya katiba ya warioba ibadilishwe katiba yote na sio kipengele kimoja
 
Nyie mnaotaka aongezewe muda ndio wenye haki ya kujieleza kulingana na katiba ya nchi. Akina Askofu Emmaus Mwamakula wanaotaka katiba mpya wao hawana uhuru huo.

Unahisi kwann?? Anza kujibu kwanza maswali yetu kabla hatujachangia mada yako.

Askofu ameitisha maandamano. Kuna sehemu nimitisha maandamano mimi??

Nilichokisema ni kuwa, Mh. Rais bado tunatamani uongozi wake;

Hayo mengine mimi sijui.

Halafu, sio lazima nijadili issue ya Askofu hapa, sio mahala pake na kuna uzi wake.

Turudi kwenye mada kuu.
 
Akili gani uliyonayo.

Acha wenye kuona una akili au huna akili wakuambie.Bado hutaki kujitambua kama huna akili.Wengi humu wameshakuambia kuwa,akili huna na ujitambue hivyo.

Kama jina kwako sio issue,Huo ndio ujinga wenyewe tena wa kwanza.Hujijui unamzungumza nani na unazungumza na nani humu.Ndio ujinga huo.

Ujumbe ungekuwa umefika sawa sawa hakuna mtu angekurekebisha kwa kucomment chochote humu.Mara nyingi mwenye akili ukisema chochote chenye kutumia akili watu hukaa kimya kwa maana ya kukichua na kukifanyia kazi.

Ukileta pumba ndio wenye akili zao wanakufundisha.Ni vizuri pia kufundishika.Ili siku nyingine unapoandika ujue kuwa kuna wenye akili watasoma na watakuchallenge.

Ujinga mwingine,bado hujajitambua kuwa tayari unapingana na katiba.Na kupingana na katiba ni kuvunja katiba na sheria za nchi pia.Nilishasema kutokana na jeshi la polisi kuwa na double standard,ndiyo maana bado uko nje wewe.Vinginevyo ungejikuta LOCK UP.Shukuru Police double standard.

Mimi sio mwanasiasa,na afadhali tangu mwanzo hukujitambulisha kama mwanasia.Ningeshafungasha virago kwani mimi na wao ni maji na mafuta.kumbe ndio maana unaandika upumbavu huku shauri tumbo lako lijae kisiasa.Nakukumbusha tena kundi la kujipendekeza kama kina musiba na wengine kama paschal wako wapi. Mwenye kutoa nafasi ameshawashtukia na zimeisha mwaka huu.Tafuta njia nyingine.

Ukweli gani unaoutoa hapo wakati ni rojo tu.hakuna mwanasiasa wa Tanzania.anayesema ukweli?wote ni waongo tu kama wewe,mawazo yako binafsi baki nayo kichwani kwako ndiyo maana unayaita mawazo yangu binafsi.Ni ya kwako.Ukishawashirikisha wengine ni ya kwenu wote. Otherwise ungeyaleta kwa kuomba ushauri kwa kuwa ni mawazo yako.Pole sana, ndivyo ujinga ulivyo hivyo,na mjinga huleta hivyo hivyo kama ulivyoleta.

Wajinga wenzako ndio watakaoshawishika.Pole.

Mbona povu aisee, naona umepaliwa na mada imekuingia kisawa sawa.

Sasa sikiliza; nina nsingi thabiti wa kuandika nilicho andika, sasa kama umekereka shauri yako.

Huwezi kunipangia cha kuandika, kama kimekuudhi, utajijua.

As long as sijatukana, wala kuvunja sheria yoyote ya nchi, roho yangu na dhamira zangu ziko safi na wala havinihukumu.

So kaa kwa kutulia dawa iingie
 
A
Sawa, ni mawazo yake na tunayaheshimu.

Kwani kuna shida yoyote?
Ameleta ili iweje.Mawazo yake abaki nayo kichwani kwake.Ni ya kwake.Shida ipo.Shida hakutakiwa kuyaleta humu.Ni ya kwake.Ameyaleta kwa makosa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom